BongeMwepesi
Senior Member
- Aug 13, 2013
- 125
- 83
Habari wana Jamvi,nina mpenzi ambaye tu wapenzi kwa muda sasa na tunatarajia kuoana soon,sasa nina rafiki yangu wa karibu tu ambaye pia tumeanzisha biashara pamoja .Sasa huyu rafiki yangu anamtongoza mpenzi wangu sikuweza kugundua hicho kitu mpaka mpenzi wangu aliponiambia sababu alianza mtongoza na huyu mpenzi wangu akamkatalia na kumtishia akiendelea ataniambia mimi,lakini rafiki yangu hakuelewa na mpenzi wangu akanambia na kuna siku alipiga simu mpenzi wangu akamuweka loudspeaker nikawa namsikia akimuambia mpenzi wangu mambo mengi ya uongo kuhusu mimi ikiwepo kuwa nina mahusiano na wapenzi wengine wengi na ni kitu sio cha kweli.Kwa kweli hasira kali zimenikamata na sijui nifanye ninikwa haraka nimefikiri kufuta ukaribu naye kabisa na nimuite nimuambie na kuanzia hapo urafiki ufike mwisho na pia kuacha kufanya nae hiyo biashara tumeanzisha pamoja maana Napata wasiwasi kama mtu anathubutu kutaka kukusaliti kwa kuwa na mahusiano na mpenzi wako basi hata anaweza kukusaliti au kukuuua kwenye biashara au pesa.....Naombeni tu ushauri wenu maana pia naona naweza fanya kitu kibaya kwake bure.