Nilikuwa na ishu inafanania na yako miaka kadhaa imepita.
Nilienda hospital moja inaitwa St.Joseph mkoa mmoja,,,pale maness wote ni masister,,,halafu ni wazuri sana,,sasa kuna mmoja nilimkubali mno,,mpaka nilibidi nirudi pale baada ya siku mbili nikijifanya bado naumwa lakini ni yule nesi alinifanya nikapagawa,,,ila Nilikuwa na demu wangu na anaenipa kila kitu.....Nikamwomba appointment akawa ananipiga tarehe Baadae miezi kama mitatu nikaenda nae chakula cha mchana....nilimuuliza vingi ila kikubwa ni nini kilimfanya awe sister??? Nikamwambia toka nimuone imeniwia vigumu kumtoa kwenye mawazo yangu,,,ila aliniambia mengi na hakuwa tayari,,,,,ila ni best counsellor niliowahi kutana nao....Basi nimekuwa nae karibu baadae zile hisia ziliniisha na bado alikuwa akinikumbusha kusali na hadi leo ni sister alie na msimamo na aliesimamia misingi..Kwa kifupi alinisaidia sana maana alijenga ukaribu na mimi na kunijengea mtazamo kwamba nifocus kwenye dini kwamba Maarifa ninayojaza kwenye fahamu zangu ndo hudetermine direction yangu..books na mafundisho na aina ya miziki ninayosikiliza ni vitu vya kuzingatia sana.