Rafiki yangu amevunja uchumba wangu

Rafiki yangu amevunja uchumba wangu

Mshukuru Mungu kwa jambo hilo kutokea mkiwa kwenye uchumba. What if ungekuwa umeshafika kwenye ndoa?
wakikufuata kukubembeleza washauri aolewe na huyo rafiki yako.
Kweli kabisa mkuu nawaza tu ndio angekua kashaoa alafu anamkuta mkewe hivyo uuhhh mbaya sana maskini, kikubwa mtoa mada amshukuru sana Mungu kumfunulia haya mapema ili ajiepushe
 
shida ya huyo binti ni harusi sio wewe..
waambie hao wazee hiyo mahari wafanye kama umemtolea mgoni wako wamwozeshe kwake...easy
 
Unamfanyia demu/make surprising? kweli una roho ngumu sie wanaume tulishaachaga huo ujinga huwa tunawafanyia surprising babu zetu tu huko bush na si Bibi zetu maana nao hawavumi lakini....
 
Hbr wana MMU ?

Bila kupoteza muda niende kwenye mada. Naandiki nikiwa na uchungu mkubwa sana moyoni mwangu.

Ilikuwa tarh 2/1/2019 siku moja tu baada ya mwaka mpya nilirudi nyumba nikitokea Nairobi nilipokwenda kwa shughuli zangu binafsi, nilipofika home nikaoga na kuamua kutoka kwenda nyumbani kwa mpenzi wangu. Huyu mpenzi wangu tulikuwa tumeshaenda mbali sana kiasi cha kuwa nimeshalipa na mahali kwao.

Sikutaka kumpa taarifa kama nimerudi ili nimfanyie surprise kama mjuavyo tena surprise ni kitu cha kawaida kwa wapenzi.

Nilibeba vijizawadi ambavyo nilimnunulia nilipokuwa Nairobi, nikashika njia huyo mpaka home kwake, ilikuwa inaelekea saa tatu usiku Mara huyo nikafika. Nilipokelewa na house girl.

Nilipoingia sebuleni tu house girl akaninong'oneza kuwa mtu yupo chumbani na mpenzi wangu.
Sikuamini Maneno yake nikaelekea chumbani kwa speed kujaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa nafunguo, nikaamua kugonga ilichukua muda kidogo mpaka mlango unafunguliwa.

Alipofungua mlango tu mm nikamsukuma nakuzama ndani, wakati huo yeye alikuwa na kanga moja tu, mara nikakutanisha uso na rafiki yangu kipenzi akiwa kajilaza kwenye Kitanda cha mpenzi wangu huku akiwa kajifunga taulo ambalo huwa nalitumia mm nikilala kwa mpenzi wangu.

Sikuamini macho yangu, nilisimama kwa dakika kadhaa nikiwa sijui cha kufanya baadae nikaamua kuondoka bila ya kusema neno.

Baada ya kuondoka mpenzi wangu alinipigia simu kwa kweli sikupokea alipiga mpaka akachoka. Siku moja baada ya tukio aliamua kunifuata home hakuja peke yake alikuja na wazazi wake kwa kweli niliwafukuza sikuwa tayari kuongea lolote.

Baada ya wiki kupita niliitwa na mshenga akaniuliza kilichotokea nilimueleza kila kitu alichonijibu kama hayo ni kweli huyu hakufai tena .

Alinishauri nikutana naye mbele ya wazazi wake nimpe msimamo wangu, sikusita nilikutana nao nikawaeleza kuwa sitaweza kuendelea tena na binti yao. Mambo yakawa mengi wakaanza kunisihi nisamehe kwa kweli nilishindwa nikainuka na kusepa zangu.

Tangu siku ile wananisumbua sana kila siku kunitumia watu ili niendelee na binti yao kiukweli siwezi kuwa mnafiki moyo wangu hauwezi hili kbsa. huwa sina unafiki kabisa.

Mimi ni mwamnifu sana sijawahi kuwa na mahusiano nje yake iweje Leo yeye anifanyie hivi?

Rafiki yangu kweli umeamua kunifanyia unyama huu woote? Hukumbuki fadhira zangu? Bila Mimi ungekuwa hivyo? Ungekuwa hapo ulipo?

Nimeandika haya kwa lengo la kuwashirikisha ili nitue mzigo wa uchungu nilionao moyoni mwangu.

Sina mpango naye tena hata aje nani.


Sent using Jamii Forums mobile app
MAHUSIANO BILA MATUTA MATUTA HAYAENDI, MATENDO MENGINE YANAUMIZA KULIKO UMIZA YENYEWE, MTU ANAYEKUJUA NDIO ATAKAYEKUUA, HAKUNA MCHAWI WA MBALI ANAYEKUJA KUWANGA KWAKO BILA KUPEWA MNARA NA ANAYEKUJUA, POLE SANA NDUGU.
 
Muulize why ujue kilichompelekea kufanya hivyo! Bila ya kujuwa sababu inaweza ķuja kutokezea tena kwa mchumba wako mwengine.
Hakuna sababu za mtu kuchepuka kama kuna tatizo mahala vunja mahusiano
 
Hii story naijua! Umeipindua pindua flani hivi kuficha uhalisia! Naifahamu fika Na hata sehemu ya mazungumzo yenu ni nanayo! ..si alikanusha lakini Huyo "mpenzi" wako Na akakuapia nothing happened?
We nae! Nothing happened huko chumbani wakikuwa wanafanya maombi uchi?
 
Alipofungua mlango tu mm nikamsukuma nakuzama ndani, wakati huo yeye alikuwa na kanga moja tu, mara nikakutanisha uso na rafiki yangu kipenzi akiwa kajilaza kwenye Kitanda cha mpenzi wangu huku akiwa kajifunga taulo ambalo huwa nalitumia mm nikilala kwa mpenzi wangu.
kaka una ujasiri na self control,amekosea na inawezekana sio mara ya kwanza usingewafumania wangeendelea kukuchora,,,kwanza msamehe na ukumbuke jina lake tuu,sikushauri urudiane nae kamwe ,songa mbele pambana na maisha,tafuta watu wa psychology upate cancelling maana iyo hali itakupelekea uchukie wanawake na marafiki kwakilichotokea..
 
Hbr wana MMU ?

Bila kupoteza muda niende kwenye mada. Naandiki nikiwa na uchungu mkubwa sana moyoni mwangu.

Ilikuwa tarh 2/1/2019 siku moja tu baada ya mwaka mpya nilirudi nyumba nikitokea Nairobi nilipokwenda kwa shughuli zangu binafsi, nilipofika home nikaoga na kuamua kutoka kwenda nyumbani kwa mpenzi wangu. Huyu mpenzi wangu tulikuwa tumeshaenda mbali sana kiasi cha kuwa nimeshalipa na mahali kwao.

Sikutaka kumpa taarifa kama nimerudi ili nimfanyie surprise kama mjuavyo tena surprise ni kitu cha kawaida kwa wapenzi.

Nilibeba vijizawadi ambavyo nilimnunulia nilipokuwa Nairobi, nikashika njia huyo mpaka home kwake, ilikuwa inaelekea saa tatu usiku Mara huyo nikafika. Nilipokelewa na house girl.

Nilipoingia sebuleni tu house girl akaninong'oneza kuwa mtu yupo chumbani na mpenzi wangu.
Sikuamini Maneno yake nikaelekea chumbani kwa speed kujaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa nafunguo, nikaamua kugonga ilichukua muda kidogo mpaka mlango unafunguliwa.

Alipofungua mlango tu mm nikamsukuma nakuzama ndani, wakati huo yeye alikuwa na kanga moja tu, mara nikakutanisha uso na rafiki yangu kipenzi akiwa kajilaza kwenye Kitanda cha mpenzi wangu huku akiwa kajifunga taulo ambalo huwa nalitumia mm nikilala kwa mpenzi wangu.

Sikuamini macho yangu, nilisimama kwa dakika kadhaa nikiwa sijui cha kufanya baadae nikaamua kuondoka bila ya kusema neno.

Baada ya kuondoka mpenzi wangu alinipigia simu kwa kweli sikupokea alipiga mpaka akachoka. Siku moja baada ya tukio aliamua kunifuata home hakuja peke yake alikuja na wazazi wake kwa kweli niliwafukuza sikuwa tayari kuongea lolote.

Baada ya wiki kupita niliitwa na mshenga akaniuliza kilichotokea nilimueleza kila kitu alichonijibu kama hayo ni kweli huyu hakufai tena .

Alinishauri nikutana naye mbele ya wazazi wake nimpe msimamo wangu, sikusita nilikutana nao nikawaeleza kuwa sitaweza kuendelea tena na binti yao. Mambo yakawa mengi wakaanza kunisihi nisamehe kwa kweli nilishindwa nikainuka na kusepa zangu.

Tangu siku ile wananisumbua sana kila siku kunitumia watu ili niendelee na binti yao kiukweli siwezi kuwa mnafiki moyo wangu hauwezi hili kbsa. huwa sina unafiki kabisa.

Mimi ni mwamnifu sana sijawahi kuwa na mahusiano nje yake iweje Leo yeye anifanyie hivi?

Rafiki yangu kweli umeamua kunifanyia unyama huu woote? Hukumbuki fadhira zangu? Bila Mimi ungekuwa hivyo? Ungekuwa hapo ulipo?

Nimeandika haya kwa lengo la kuwashirikisha ili nitue mzigo wa uchungu nilionao moyoni mwangu.

Sina mpango naye tena hata aje nani.


Sent using Jamii Forums mobile app
Dah hapo hakuna ndoa, huyo rafiki ako si amuoe akurudishie mahari
 
Huu ndiyo uamuzi wa kiume sasa, hongera sana na usirudi nyuma na uamuzi wako.
 
Siku zote jua unapofnya surprise kun mawili uka msurprise mwenzako au ukaji suprise mwenywe.
Lingine mahusiano ya mbali na haswa kama hamjakaa na mwenzako kwa mdaa flan huwaga ni ngumu sanaa kudumu.
Poleeee sanaaa kijana
Surprise yako itakuwa umejisurprise mwenywe tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom