Rafiki yangu amenichongea kwa mke wangu

Rafiki yangu amenichongea kwa mke wangu

Joined
May 18, 2015
Posts
83
Reaction score
95
Juzi jumanne baada ya Dk slaa kuongea, jioni yake nilipitiliza moja kwa moja Bar kutokana na kuchanganyikiwa, hiyo ilikua ni baada ya kutoka kazini jioni.

Tulikua wakereketwa wawili tulioamua kwenda bar Ku digest that day's chain of events, mimi na Dada na mmoja tupo pamoja hapo kazini, tukawa tunakunywa hapo mimi na huyo binti. Baadae Rafiki yangu wa karibu akatujoini tukaendelea kunywa hadi saa mbili usiku tukatawanyika, jamaa akaondoka mwenyewe, mimi nikaenda na binti nikamshusha kwake.

Nashangaa nilipofika home wife kakasirika ile mbaya kwamba nilikua na mwanamke bar na baadae nikaenda nae gesti, nikajaribu kumwelewesha kuwa ni kweli nilikua bar na tulikua na work mate kwa maongezi ya kawaida tu, mwisho akanielewa yakaisha, ingawa nililazaimika kumuomba baba yangu mkubwa tunaeishi nae hapo nyumbani kutusuluhisha na kwa msaada wake jana jambo hilo limeisha.

Ndipo nikajaribu kumdodosa wife umejuaje kuwa nilikua bar flan na mtu flani, akasema Rafiki yangu niliyekua nakunywa nae ndio alimtumia msg baada ya sisi kuondoka, na wife akanionesha hiyo whatsaap msg nikashangaa sana, mshkaji wangu anawezaje kunifanyia hivyo, ina maana yeye jamaa alidhani yule binti ni bibi yangu? Kwa nini hakuniuliza?

Leo asubuhi nimempigia simu kumtega tu, nikamuuliza kwa mawazo yako unadhani nani kamweleza wife kuwa nilikua bar na mwanamke? Akajifanya kushangaa na kumlaani huyo mtu aliyefanya kitendo hicho.

Wadau nimfanyeje huyu mtu?
Huyu jamaa ni family friend, Nina namba ya mkewe na yeye ana ya mke wangu, na huwa tunashirikiana vitu vingi.

Sasa wadau huu ni ungwana kweli? Alikua na lengo gani hasa? Au anataka na mimi ndoa yangu ivurugike kama yake maana ni juzi tu wamepatana na mwenzie baada ya yeye kushikwa live na mkewe akiwa na bibi mwingine!

Yaani ameniudhi sana, mtu bado tunahangaika na haya ya Dk slaa kuasi halafa anataka kunifitinisha na wife, nonsense!
 
Huo ni urafiki wa kikuda na kuna uwezekano anamtaka mkeo hivyo anatengeneza mazingira au tayari kuna kauhusiano ka kipumbavu kanaendelea baina yao. Mtu hawezi kukurupuka tu kumweleza mkeo ujinga kama hakuna mazoea ya kuzungumzia ujinga yaliyoanzia kitambo.
Hiyo ni meseji moja uliyoisikia, je kuna mangapi ambayo wamekuwa wakizungumza? Piga chini huyo rafiki.
 
Sitaki mazoea ya rafiki zangu na mke wangu.
Kama ameweza kumtumia huo ujinga hashindwi kumtaka na kumtongoza.
Anawagombanisha ili apate upenyo wa kujiingiza.
 
piga chini na mpe mke wako ukweli yani muonye kama hasikii shauri zake...watu wapo kuharibu ya watu tu...sio rafiki huyo
 
Simpo..Msamehe tu. Msamehe huyo rafk ako Msamehe pia Dr Slaa..Kuhusu huyo rafiki ako unatakiwa ufikiri kwa mapana au uwe na Mawazo chanya pia badala ya kuwa na Mawazo hasi pekee.. Mfano: Chochote kibaya kingekupata usiku huo Mkeo angekuwa na taarifa na angejua ataanzia wapi. Kingine baada ya wewe kuhakikisha Moyoni mwako kuwa umemsamehe na huna kinyongo nae.. Muite make Chini wewe na yeye Muongee kiutuuzima mueleze Kilichopo Moyoni ili upate Amani. Kuhusu Dr Slaa vile vile Msamehe hunabhaja ya kujipa maumivu moyoni kwa Mtu Uliyemuona Msaliti.. Pia ukifiri kwa Makini Watu wengi especially Vijana na Wasomi wamempuuza na Zaidi sana kampigia kampeni Mgombea wako na kazidi kumpa umaarufu.
 
Mi nikikukuta na namba ya my wife wangu hatuwezi kuelewana abadani. Ni marufuku yaani.
 
Tatizo ni imani yako ya magwandwa, hebu badili kidogo tu u join gambas afu utaona neema ya milele. Hapa kazi tuuuuuuuuu! Mrudie Mungu wako ukatubu kwa ulabu wa padlocks huyo jamaa atakuwa amefungwa five years next!
 
Wrong information inasaidia nini niko dar halafu mtu aseme ameniona moro wapi na wapi!

Simpo..Msamehe tu. Msamehe huyo rafk ako Msamehe pia Dr Slaa..Kuhusu huyo rafiki ako unatakiwa ufikiri kwa mapana au uwe na Mawazo chanya pia badala ya kuwa na Mawazo hasi pekee.. Mfano: Chochote kibaya kingekupata usiku huo Mkeo angekuwa na taarifa na angejua ataanzia wapi. Kingine baada yawewe kuhakikisha Moyoni mwako kuwa umemsamehe na huna kinyongo nae.. Muite make Chini wewe na yeye Muongee kiutuuzima mueleze Kilichopo Moyoni ili upate Amani. Kuhusu Dr Slaa vile vile Msamehe hunabhaja ya kujipa maumivu moyoni kwa Mtu Uliyemuona Msaliti.. Pia ukifiri kwa Makini Watu wengi especially Vijana na Wasomi wamempuuza na Zaidi sana kampigia kampeni Mgombea wako na kazidi kumpa umaarufu.
 
Chukua simu ya mkeo ushinde nayo. Halafu, ukikutana na huyi jamaa muonyeshe hiyo meseji.

Halafu muulize, unadhani anayoyafanya dr slaa hayajulikani hata kama yuko states?
 
alijaribu kuwa mwema kwa mke wako sema ndo akawa mbaya kwako
 
..............................................................................[deleted]
Wadau nimfanyeje huyu mtu?
Huyu jamaa ni family friend, Nina namba ya mkewe na yy ana ya mke wangu, na huwa tunashirikiana vitu vingi

Mkubwa, hukujua kuchagua rafiki. Kuna watu siyo maadui lakini hawafai kupewa nafasi ya kuitwa marafiki.

Kama wengine walivyohisia, huyo anamtaka mkeo. Kwa kuwa mkeo kakuonyesha msg ni ishara bado hajafanikiwa maana angeitunza iwe siri yake. Achana na mtu mwenye IQ ndogo.
 
Ikiwa unataka kuendeleza urafiki nae, mkae wewe, mkeo, mke wake, huyo mfanyakazi mwenzio mumueleze ukweli na mwambie aache kuhisi mambo na kuyasmbaza bila kujua ukweli, vinginevyo punguza urafiki nae na asimzoee mkeo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom