Rafiki wa mtoto wako

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
Kuna kilio katika Jamii nzima juu ya mromoko wa maadili tunaoushuhudia ambao kwa kiwango kikubwa umebebwa na vijana. Kitu cha msingi kujiuliza ni Je? wakati kijana huyu anaharibika namna hii wazazi au walezi wake walikuwa wapi? au hawakuwa na weredi wa kumuongoza?

Katika kulitafakari hili, nimekuwa nikiangalia namna vijana wanavyoshawishiana katika mambo yao, ambayo katika macho ya jamii yanaonekana kama ni tabia mbaya. Kuanzia ulevi wa pombe, ngono za makundi, mahusiano ya jinsia moja, matumizi ya dawa za kulevya, lugha chafu, n.k

Je? unamfahamu rafiki wa mtoto wako? unajuwa anaishi wapi? unawajuwa wazazi wake? wazazi mnafahamiana? na je haya ni mambo ya muhimu kufahamu katika jitihada za kumkuza kijana wako kuwa mtu mwenye tabia njema?
 
Mada nzuri sana hii Sangarara. ni muhimu sana kumfahamu rafiki wa mwanao ila wakati mwingine mazingira yanatoa nafasi finyu ya kufanya hivyo
 
Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
KUMCHA BWANA NDICHO CHANZO CHA MAARIFA (Mithali 9:10)


Sio siri kwamba tumeingiziwa kwa siri mawazo haya potofu na nchi za magharibi,na sisi kwa upumbavu wetu,tena kinyume kabisa na utamaduni wetu,tumeyakubali.Katika kitabu cha Mithali22:15,Agano la kale, tunasoma maneno haya:"Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali." Maneno haya maana yake ni kwamba, asiyemchapa mwanae anamfanya awe mjinga,kwa vile hatma ya kutomchapa ni kubaki na ujinga wake.Maandiko mengine ya Biblia pia katika kitabu cha Mithali 23:13 yanasema "Usimnyime mtoto wako mapigo,maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa." Katika kitabu hicho hicho cha Mithali(23:14) pia tunasoma maandiko haya "utampiga mtoto kwa fimbo na kumuokoa nafsi yake na kuzimu."Katika maandiko yote haya Mungu anasisitiza umuhimu wa adhabu ya fimbo kwa mtoto.Yeye anajua kwamba fimbo kwa mtoto ni lazima.
 
Ni wazo zuri na jema. Ingawa kwa maisha ya mijini (na hasa Dar), pengine hilo linaweza kuleta changamoto sana. Wengi tunatoka nyumbani alfajiri na kurudi nyumbani jioni kabisa (wengine kiza). Muda wa kukaa na watoto tu na "kuwafahamu" wao wenyewe tu ni shida sembuse hilo la kutaka kuwafahamu na marafiki zake au wazazi wa marafiki zake!

Lakini pamoja na changamoto hiyo, kama wazazi tunao wajibu wa kuhakikisha kutanapata muda wa kukaa na familia. Muda mdogo tunaoupata wa kukaa na watoto tuutumie effectively.
 

Bujibuji
Hii ni issue ingine tata zaidi. hapa naona unachallenge juu ya haki za watoto, nakumbuka enzi hizo niko lake secondary pale mwanza, kutokana na kuwa na wanafunzi wengi kutoka jamii ya kihindi ilifikia point ikapigwa marufuku mwalimu kumtandika mwanafunzi na kama ikifikia hatua hiyo basi muwe mmekubalina kwa maandishi. Matokeo yake, mji wa mwanza ukashuhudia wanafunzi wakaidi, wakorofi, wahuni, majambazi (yes, wanafunzi majambazi) na mpaka hapa napoandika post hii kama wapo wanaoweza kusimamia maisha yao wenyewe inalazimika kumrudishia Mwenye Mungu sifa zote ni utukufu.

Nakumbuka namna nilivyovutishwa bangi nikiwa form one.
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
shule za boarding, vyuoni, kwenye vikundi vingine mbalimbali

Lakini wakitoka Boarding si wanatembeleana? vyuoni ni tricky lakini tusubiri wadau washauri the best way to handle this. haya makundi mengine kama ni mtaani yako ndani ya uwezo wako kuyafahamu. kwa mfano ni makundi yenye sifa gani? age distribution ndani ya kundi ikoje? urafiki wa vijana wenye miaka 15 na 25 ni salama wakati wote?
 
kumbuka mzazi na wewe una biashara au umeajiriwa, so unabanwa na majukumu muda mwingi wa wiki
 
kumbuka mzazi na wewe una biashara au umeajiriwa, so unabanwa na majukumu muda mwingi wa wiki

Inabidi kubalance kazi na Familia, ama sivyo utaharibikiwa
 
umeuliza maswali muhimu sana, bu tnadhani haya "matatizo ya maadili" tunayo yaona leo yalikuwepo kila siku. sema leo watu ni wengi zaidi, na info inatembea haraka zaidi. sijafanya utafiti wowote, ila vile vile sijaona tafiti inayo sema hizo tabia zimeongezeka lately.
 

Mwali
Uwezekano wa mmomonyoko wa maadili kushamili zaidi nyakati hizi ni mkubwa kwa sababu moja ya kitu kinachokoleza saba mabadiriko katika jamii ni muingiliano wa watu hasa mijini. Unakuta mtaa umejaa familia zenye background tofauti kabisa.
 
Mwali
Uwezekano wa mmomonyoko wa maadili kushamili zaidi nyakati hizi ni mkubwa kwa sababu moja ya kitu kinachokoleza saba mabadiriko katika jamii ni muingiliano wa watu hasa mijini. Unakuta mtaa umejaa familia zenye background tofauti kabisa.
Inawezekana lakini tutapata uhakika pale tutakapo fanya utafiti
na tafiti zenyewe zitaanza kwa ku-define nini maadili na nini mmomonyoko wa maadili
then katika ripoti lazima waangalie na huko vijijini watu hao walikotoka wamekuacha kusafi?
kwa mujibu ya hypothesis yako ni kwamba muingiliano wa watu ndio unasababisha
basi kama ni kweli tafiti itaonesha kua kule vijijini things haven't change or have improved
 

Agreed.
 
Watu wana muda wa kushinda baa na saluni lakini hawana muda wa kufahamu watoto , let alone marafiki zao? Mkijipanga yote yawezekana.
 


Mada muhimu sana hii,.
Ukweli ni kwamba UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU:Ki ujumla tatizo la kuporomoka kwa maadili ya watoto kumeanza miongo michache sana iliyopita hapa Tanzania.Malezi ya watoto ktk miaka ya 1980s kurudi nyuma yalikua ni ya kushirikiana,(jamii nzima) mtu mzima alikua na sauti ya kumkanya mtoto yoyote pale mtaani,nyumbani nk,wazazi hawakua na ubinafsi/ujuaji wa kujifanya wao ndo wanaweza kulea watoto wao peke yao (mzazi hawezi kutekeleza majukumu ya hatua zote za kulea mtoto peke yake,hasa mambo ya kijamii na elimu).Wazazi na jamii inabidi kubadilisha mitazamo yetu ya kulea wototo.

UTEKELEZAJI WA HOJA MUHIMU ALIOITOA BUJIBUJI HAPO JUU INAHITAJI USHIRIKIANO WA JAMII KIUJUMLA {Ila sijaelewa vizuri hapo kwenye blue}

Kumbuka:Siku hizi watu wazima hawawezi kulea/kukanya watoto wa wenzao ni kwa sababu ya upungufu wa maadili na ubinafsi.Serikali inatakiwa kuweka mwongozo mzuri na kuufuatilia,maana kutatua tatizo kama hili kupitia jamii iliyoporomoka maadili bila mkono mkali wa serikali tutatesa watoto.
 

Utashi
Hakuna chombo kibovu katika usimamizi wa makuzi ya watoto kama serikali, hata haya matatizo tunayoyaona sasa ni kwa sababu tumeiachia serikali na vyombo vingine vya kibishara nafasi kubwa sana katika usimamizi wa wa makuzi ya watoto wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…