Rafiki mwenye msongo wa mawazo muepushe na pombe

Sky Eclat

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,439
Msongo wa mawazo kwa kupoteza kazi au kufiwa na mtu wa karibu unaumiza sana. Rafiki yako au ndugu yako akiwa katika hali hii, ukimfariji na pombe kuna hatari ya kuifanya pombe pombe kuwa tegemezi la furaha yake.

Chakula ni kitu ambacho kila mwanadamu anakihitaji. Fikiria chakula anacho kipenda, nunua na umshirikishe katika mapishi. Zoezi hili litasaidia kuchangamsha akili.

Baada ya kula mnaweza kucheza karata, chase au kuangalia mpira. Akiwa ameweka mawazo yake huko, unaweza kwenda chumbani anako lala na kumsaidia kubadilisha shuka, kumfanyia usafi.

Mnaweza kuandaa picnic na kuwa na mpira wa mazoezi au kutembea ufukweni.

Watu wenye msongo wa mawazo wako katika hatari ya kujiua wasipopata msaada.
 
Kama ni rafiki wa jinsia za tofauti.. Ukifata hizo hatua lazima mengine yatokee
 
vipi kuhusu wewe unayeanzisha uzi usiku huu unasumbuliwa na msongo wa aina ipi?
 
Umenigusa hapa sasa hivi nipo location na'prove ya mshkaji wangu, ngoja tuyasovu kwanza mamaaa
 
Yani kati ya hayo mambo kuna ishu zilitesha, one day nimelewa buguruni hadi nafika kwangu tabata sikujua nimefikaje? Tena nilikuwa naendesha boxer
 
Mnapenda kuweka uhai rehani
 
Hakika umenena, kuna tofauti sana mtu anayekunywa pombe kujifurahisha na aliyekatika msongo wa mawazo.

Wa kwanza atakunywa kistaarabu na kiasi ambapo atachangamka kidogo tu na kujipimia kiasi tosha na anaacha baada ya chupa kazaa.

Wa pili ( mwenye msongo) hataweza kujicontrol, atakunywa hadi atakapo zima. Au hadi pale pesa itakapoisha na pia hapo atakuwa kajitengenezea tatizo la kiuchumi.

Na kama kiuchumi hayupo vizuri basi kama alikuwa mtumiaji wa bia kawaida atahamia kwenye pombe kali ili awahi kulewa...

So sure.... Mtu mwenye msongo akitegemea pombe imuliwaze ghafla itageuka kuwa addiction hata akisolve tatizo lake hali itabaki hivyo hivyo MLEVI.

Na tatizo la kiuchumi litakuwa limetengenezwa hivyo... Hamna kitu kinamaliza hela kama mtu kuwa addicted... Atakunywa hadi ahakikishe pesa aliyobeba imeisha mfukoni hata kama alikuwa na laki 3 yote itaishia huko. Plus kuibiwa akiwa chakali kazima.

Ushauri mzuri.

TUPE MFANO HAI WA YALIYOTOKEA HADI UKAANZISHA UZI HUU ILI TUJIFUNZE VIZURI.
 
Kuna hatari ya kuingia madeni ili anunue pombe au kuuza mali alizonazo. Ukisha kuwa alcoholic hata mwenyeewe huamini kuwa unaweza kuishi bila pombe.

Kuna hatari pia ya kuharibu internal organs.
 
Sky eclat una mada nzuri lakin kila siku najiuliza, kwanini huna mume? kukosa mtu umpendae na kwenyewe kumekupa msongo wa mawazo
 
Back
Top Bottom