Radio ya Idhaa ya Kiswahili ya France International kufunga ofisi zake Wiki ijayo. Ushoga na Shirika la TBC vyatajwa kuwa visababishi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Idhaa ya Kiswahili Ya Radio France International Wiki ijayo itafunga ofisi zake Tanzania na kuhamishia Nairobi Nchini Kenya.

Sababu Ni kushindwa kukubaliana Kuhusu mkataba mpya Baina ya RFI Kiswahili na serikali kupitia Shirika la utangazaji TBC baada ya ule wa awali Wa miaka kumi kumalizika.

Inaelezwa TBC walitoa pendekezo la kulipwa kiasi kikubwa Cha fedha jambo ambalo halijakubaliwa na uongozi wa RFI Wenye Makao yake makuu Paris Ufaransa.

Wafanyakazi Tisa raia wa Tanzania wataathirika kwa kukosa kazi huku Mtanzania mmoja tu akiwa amechukuliwa kwenda Nairobi.

RFI Kiswahili ilianza kurusha matangazo kwa lugha ya Kiswahili Julai mwaka 2010 Kupitia Kituo Cha TBC FM.

Madai Mengine ni baadhi ya waliokuwa wafanyakazi kumchongea bosi wa Kituo hicho raia wa Ufaransa kujihusisha na ushoga na kupelekea ofisa huyo kuzuiwa Katika uwanja wa ndege February 2019 Wakati akijiandaa kuondoka Nchini na baadaye Kuamriwa asirejee tena Tanzania
 
Wasituretehe laana za Sodoma na Gomora hao wazibua mitaro! Asante serikali ya JPM kusimamia kile unachokiamini na sisi tuko nyuma yako!
 
Back
Top Bottom