Radio Times FM yatanguliza mbele maslahi ya Taifa, yawakaribisha manguli kusaidia Taifa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,660
119,278
Wanabodi

Tanzania tuna vituo vingi vya redio, kila kituo kina mambo yake na mchango wake kwa Taifa.

Miongoni mwa vituo hivyo ni kituo cha Radio Times FM inayopatikana 100.5 ambacho pamoja na mambo mengine, kimejibainisha ni moja ya vituo vimavyotanguliza mbele Maslahi ya Taifa kwa kutangaza live mambo yenye Maslahi kwa taifa.

Radio Times FM ndani vipindi vyake mbalimbali, imeanzisha segment mpya iitwayo, "Zaidi ya Kawaida". Kwenye segment hiyo, wanawaalika Watangazaji, ma dj au wasanii wa zamani kwenda kutoa uzoefu wa enzi zao kwa kilinganisha na sasa, kisha wanawapa fursa za kutoa somo lolote kuhusu uzoefu wao.

Leo mimi ni miongoni mwa waalikwa wa leo na nikaanza kwa kujikumbusha enzi zangu za utangazaji wa redio ambao nilianzia RTD miaka ya 90s, nikapigiwa miziki ya zamani ukiwemo wimbo wa Georgina wa Marijani Rajabu na bendi ya Safari Trippers, nikapagawa na kujikuta ghafla nimerudia utangazaji wa redio na kulipuka. ..
Kwenye kutoa somo nimetoa somo linaloitwa Uzalendo na Rasilimali Zetu.

Nikasisitiza hatua alizochukua rais Magufuli kwenye sakata la mchanga wa dhahabu ni Uzalendo wa hali ya juu na anapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania mzalendo wa kweli.

Japo Tanzania tumeingia mikataba na wawekezaji hao lakini mikataba yote huingiwa kwa hiyari na utekelezaji mkataba huo hutegemewa kutekelezwa kwa kitu kinachoitwa goodwill na good faith. Ukitokea upande mmoja unaiba na kufanya udanganyifu hii ni cheating, sio goodwill na haina goodfaith hivyo mkataba anaweza kuvunjwa na Tanzania kudai kulipwa fidia.

Unaweza kufuatilia hiyo mada hapa

Leo katika maisha Mseto ni zaidi ya Kawaida
LEO KATIKA MAISHA MSETO NI ZAIDI YA KAWAIDA
Created by ADAM KEFA on Fri, 06/02/2017
no comments
DBSxvVzUAAALEYD-559x520.jpg

kupitia vipindi mbalimbali leo katika redio ya 100.5 Times Fm utapata vitu tofauti tofauti ikiwemo kuwasikiliza watu mbalimbali ambao watakupa fursa mbalimbali katika kutambua mambo mengi .

maisha-800x450.jpg

Picha ya Pamoja ya watangazaji wa Times fm wakiwa na mtangazaji mkongwe wa zamani Pasca Mayala (katikati), wa kwanza kushoto ni Stanslaus Lambat,wa pili kushoto ni Dj-DSlash,wa kwanza kulia ni Dkt. Kumbuka na wapili kulia ni Fredrick mabula.

Leo katika kipindi cha [HASHTAG]#MaishaMseto[/HASHTAG] tumeungana na Mtangazaji mkongwe wa zamani Pasco Mayala ambaye ameweza kutujuza mengi licha ya kuwa na watangazaji wa kawaida wa 100.5 Times Fm Stanslaus Lambat na Dkt.Kumbuka.

Times Fm TZ - [HASHTAG]#ZaidiYaKawaida[/HASHTAG] hewani Pascal Mayalla ndani...

Paskali
 
Asante Mr. Pascal

Zaidi ya kipindi cha Dida Mchops sidhani Kuna kitu kingine cha kusilkiliza kwenye hiyo station
Ni mfu kama RTD au whatever inavyojiita siku hizi
 
Pascal, this is very funny! Ulipotaja "watangazaji wakongwe wa RTD" kwa haraka nilifikiri ni watangazaji kama akina S.S. Mkamba, Chama Omari Matata, Erasto Mbwana, Jim Ndoe, Abdul Baker, Godfrey Mgodo, Steven Mlatie na Enock Ngombale (wengi wa hawa bado wako hai). Kumbe unazungumzia "kijana" aliyeanza kazi ya utangazaji miaka ya 90!

Ama kweli neno "mkongwe" ni relative kulingana na unapeleka ujumbe kwa nani. Na utakuwa sahihi kujiita "mkongwe" kwa kuchukulia labda kuwa wengi wa watumiaji wa JF na watangazaji wa radio hapa nchini ni vijana wenye umri wa chini ya miaka 30.

Hata hivyo kilicho dhahiri ni kwamba kipindi cha kati ya miaka ya 90 hadi sasa kipo katika zama tunazoziita za mageuzi (kisiasa na kiuchumi) na matumizi internet. Na waliofikia utu uzima katika kipindi hiki kwa ujumla wao wanaitwa wa kizazi cha "dot.com" (millennials). Hiki ndicho kipindi kilichoshuhudia uanzishwaji wa vituo binafsi vya radio na tv nchini pamoja na kuanza kwa vipindi vipya vya talk/talk-back live shows na kwa kiasi kikubwa upigaji muziki wa nchi za Magharibi au wa staili na ladha ya hizo nchi.

Pia ukiangalia watangazaji wengi wa radio na tv kwa sasa ni hawa hawa vijana millennials; tena wa "age group" moja (kama picha inavyoonyesha) kitu ambacho chenyewe ni tatizo katika kukuza ubora wa utangazaji na hivyo kupanua soko la wasikilizaji (target market/audience). Kungepaswa kuwepo pia watangazaji "wakongwe" wa kuwaongoza hasa ikizingatiwa kuwa vituo binafsi vya utangazaji havina utaratibu wa kuwaendeleza kimasomo (kitaaluma na kiujuzi).

Kwa vile ni dhahiri vituo karibu vyote vya radio na tv nchini (ukiondoa vya dini na TBC) havina sera na mkakati wa kimasoko (wa kuhakikisha soko lote la wasikilizaji - audience - nchini linalengwa), vituo vyote hivi vinajikuta vinalenga sehemu moja tu ya soko (market segment) la wasikizaji: vijana chini umri wa miaka 35, tena wale wenye elimu ndogo na hivyo uwelewa mdogo wa mambo na pia uwezo mdogo wa kiuchambuzi. Hili ni tatizo kubwa linalotakiwa kushughulikiwa haraka.

Haishangazi vipindi vingi vya hizi radio ni vya majadiliano (talk shows) na vimejikita kwenye porojo za vijiweni zisizo na kichwa wala mguu; mipasho na vijembe. Taarifa za habari zinalenga tu katika kutukuza wanasiasa na hakuna uchambuzi wowote wa maana wa habari unaofanyika. Kwenye burudani vituo vyote vinapiga muziki wa aina mbili tu: hip hop (Bongo Flavour) na taarab (rusha roho), kama kwamba hizi ndizo ladha pekee za muziki wanazopendelea wasikilizaji wote hapa nchini. Kwa wapenzi wa muziki tuseme, aina wa Raggae, Rumba, Jazz, Country, Zouk nk (ambao hapa nchini wako mamilioni), hawana lao!

Kiufupi ni kwamba "wakongwe' wanatakiwa kuingilia kati na kuokoa jahazi.
 
Mkuu umeongea mengi mazuri nitumie lugha ya malkia kidogo I prefer to differ on your definition of millenials. Millenials sio walifikia umri wa utu uzima mid 90's bali waliozaliwa wakati huo. Yaani toka Mid 80's hadi 2000 ndio millenials ambao kwa wakati huo(mid 90's) walikuwa bado kuingia umri wa utu uzima.
Millennials (also known as Generation Y) are the demographic cohort following Generation X. There are no precise dates for when this cohort starts or ends; demographers and researchers typically use the early 1980s as starting birth years and the mid-1990s to early 2000s as ending birth...
 
"Ukitokea upande mmoja unaiba na kufanya udanganyifu hii ni cheating ... sakata la mchanga wa dhahabu ni Uzalendo wa hali ya juu na anapaswa kuungwa mkono".

Kwa kauli hii mkuu Mayalla you are being intellectually dishonest. ACACIA wamefanya cheating kwa ushahidi upi? Kwa ushahidi wa report ya tume ya Mruma? Unafahamu kwamba ile tume haikuwa tume huru. Pia unajua kwamba suala la mkataba ni suala la kisheria; ni mahakama ndo inapaswa kusema kama ACACIA wamedanganya ktk makubaliano yao ya kimkataba na serikali, siyo Mruma wala Magufuli.
 
Mkuu umeongea mengi mazuri nitumie lugha ya malkia kidogo I prefer to differ on your definition of millenials. Millenials sio walifikia umri wa utu uzima mid 90's bali waliozaliwa wakati huo. Yaani toka Mid 80's hadi 2000 ndio millenials ambao kwa wakati huo(mid 90's) walikuwa bado kuingia umri wa utu uzima.
Millennials (also known as Generation Y) are the demographic cohort following Generation X. There are no precise dates for when this cohort starts or ends; demographers and researchers typically use the early 1980s as starting birth years and the mid-1990s to early 2000s as ending birth...

Uko sahihi. Cheers!
 
Radio hii sijui inakua au ndio imedumaa,ni ya muda lkn inasikika Dar na pwani ,sidhan km inasikika maeneo zaid ya hayo..
 
Back
Top Bottom