Radio Station name

Wana jamvi poleni na shughuli zenu za kimaisha. Niko kwenye hatua za mwisho kufungua kituo cha radio, hivyo naomba mawazo yenu wanajamvi kuhusu jina zuri la kutumia. Nitashukuru kwa mawazo yenu tafadhali.

Nakushauri upate jina la kizalendo yani la kiswahili achana na haya maredio yenye majina ya kingereza wakati 100% ya matangazo yake ni kiswahili!napendekeza iitwe YETU FM
 
Asante sana Nasakadoo

Mkuu hapa utashauriwa majina mengi hasa ya kejeli na mizaha.
nakushauri na napendekeza fuata ushauri wa Nasakadoo. ameshauri vizuri sana,jina lolote utakaloamua kuchagua linauzika na kuvutia hadhira.
All the best mdau DATOGA
 
Wadau nawashukuruni kwa msaada wenu hasa kwa Nasakadoo coz amenipa picha angalau, nitalifanyia kazi
 
Binafsi ningeshauri uiite jina la wilaya iliyomo. Mfano, Kilosa Fm, Mikumi fm,au Mvomero Fm.

Huu Ushauri ni Mzuri Mkuu Lakini Nadhani Ni Vyema Ukaangalia Coverage ya Matangazo Yako. Majina ya Wilaya au Maeneo Ambayo Purely ni ya Morogoro, Yanaweza Kufanya Redio Yako Iwe Kama ya Morogoro tu. Kwa Mfano, Kule Mahenge Kuna Ulanga Fm. Mimi Nikiwa Tanga Kwetu Huku Nikatune Frequency Halafu Inakuja Ulanga Fm, Sitasikiliza Mana Ntahisi ni Redio ya Wapogoro. Hii ni Assumption Mkuu Sio Lazma Iwe Hivi.

Hivyo Mimi Nadhani Angalia Coverage ya Matangazo Yako. Kama Unalenga Tanzania Nzima Basi Nashuri Usitumie Majina Hayo. Tumia Jina Lisilo Maanisha Mkoa au Wilaya Flani Moja kwa Moja.

Au Iite Pride Radio, Sauti Radio, City Fm Radio, na Radio Star Fm....
nimeishia hapo

City Fm Radio Nadhani Ipo Tayari.

Nashauri Utumie Majina ya Kiswahili/Kiingereza Ambayo ni Rahisi Hata Kutamkika. Kwa Mfano Aliyekushauri Uluguru Fm Nakubaliana Naye.

Japo Kwa Kiasi Kikubwa Namna Utakavyopangiria Mfumo na Ubora wa Vipindi Vyako Pia Kwa Kiasi Kikubwa Itafanya Jina la Redio Liwe Maarufu na Kuzoeleka Sana.

Kaa na Uchunguze Kwa Makini What Makes these Radio Brands to be popular in a country? RFA, Radio One, Clouds Fm, E-Fm, Radio Five, Na Nyinginezo. Unaweza Kupata Chemistry Nzuri ya Jina Lako.

Observe Kwa Makini Jinsi E-Fm Ilivyoibuka na Kuwa Redio Inayosikilizwa na Watu Wengi Sana Dar. Itakusaidia Mkuu.

Labda na Mimi Nipendekeze Machache Hapa.

Uluguru Fm.
Info Fm.

Kila la Kheri Mkuu.
 
Dah!we jamaa utakuwa mfuasi wa Rungwe tu si bure!

Hahahaha,aisee umenichekesha kweli.
Huyu Jamaa kampeni zake akifika hata stand ya daladala anasimama na spika yake anapiga kampeni dakika kumi kisha anasepa.
Akifika mtaani akikuta watu mmekaa anawapiga somo anasepa,hahaha,
 
Wana jamvi poleni na shughuli zenu za kimaisha. Niko kwenye hatua za mwisho kufungua kituo cha radio, hivyo naomba mawazo yenu wanajamvi kuhusu jina zuri la kutumia. Nitashukuru kwa mawazo yenu tafadhali.
Jina la kituo cha redio inategemea na kusudi kuu la redio hiyo. Unapenda redio iwe ya mchepuo gani; dini, michezo, movie, au mambo yote kwa ujumla kama ambavyo karibu vituo vingi vipo hivyo? Pamoja na kuwa kituo kitarusha matangazo kwa ujumla, bado unaweza kusisitizia eneo kuu km elimu, sayansi, nk
 
Back
Top Bottom