Ndugu yangu Radio Producer, juzi juzi ulikuja humu kwa utambulisho wa kitafuta kazi baada ya kuhitimu kozi ya Radio Producer.
Tukakuelejeza sehemu za kuomba kazi lakini kutokana na elimu yako ya vyuo vya uchochoroni, hukujisumbua hata kutafuta hiyo kazi japo upate experiance.
Sasa leo ndio yamekuwa haya!? yaani ghafla umekuwa mwalimu?! au na wewe baada ya kihitimu uchochoroni sasa nawe umefungua uchochoro wako kutaka kuwalia watu pesa zao?!.
Kama wewe ni mkweli na sio tapeli naomba ueleze tuu hayo mafunzo mtayaendeshea wapi ili nijitolee kuwafanyia due diligence wana jf kabla hawajaingizwa mkenge.