Mimi ni msikilizaji mzuri wa RFA. Nimefika hapa Iringa na kukuta katika masafa yake ya 89.9 haisikiki, nilipowauliza wenyeji wakasema haijawa hewani kwa kama wiki mbili hivi. Nauliza imekuwaje? Mji wa Iringa nadhani uko nafasi ya pili kwa nchi hii kwa kuwa na vituo maarufu vya redio za FM zinazosikika (isipokuwa Radio One) ikiwa ni pamoja na kuwa na vituo vingi (local) vilivyopo hapa mjini. Kama wahusika wa RFA wapo hapa mtandaoni mnijuze.
Kitu kingine nilichogundua ni kwamba mji wa Iringa kati ya nyumba tatu mbili zina madishi ya satelite, na hata kufikia nyumba nyingine kuwa na madishi mpaka manne kutokana na wingi wa wapangaji wake, ni stesheni tatu tu ndio ziko hewani yaani Star TV ,TBC pamoja na IMTV inayomilikiwa na manispaa, wengine vipi? ITV au niseme IPP Media ina ugomvi gani na Manispaa hii? Na Mhaville ni jina la mkoani hapa (au Njombe) ndugu zako vipi huwapendi?