Rada kuu ya Tanzania ni mbovu.

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
549
Wakati Tanzania ikiwa tayari kutaka kuingia vitani dhidi ya Malawi, Ile rada kuu inayotegemewa kwa mambo ya anga, mawasiliano, kijeshi na kutua kwa ndege iliyopoko Dar kwenye uwanja wa zamani wa ndege imeharibika kwa karibu mwezi mzima sasa.

Hii ndio rada iliyonunuliwa kutoka uingereza na kuzaa kashfa ya ufisadi.

Sababu kuu ya kuharibika kwake ni matatizo ya kukatikakatika umeme nchini.

Matengenezo yake yatahitaji vifaa na wataalam kutoka kwenye kampuni ileile ya uingereza uliyotuuzia rada hiyo.

SOURCE: BBC
 
danganya toto iyo mkuu! intellegencia iko kazini hapo, sasa ole wao hao wamalawi wajidanganye wakizania kweli, imekula kwao.
 
Wangalizi wa hiyo Rada ndio matatizo Rada imekabiziwa kwa Tanzania ikiwa nzima
 
Wakati Tanzania ikiwa tayari kutaka kuingia vitani dhidi ya Malawi, Ile rada kuu inayotegemewa kwa mambo ya anga, mawasiliano, kijeshi na kutua kwa ndege iliyopoko Dar kwenye uwanja wa zamani wa ndege imeharibika kwa karibu mwezi mzima sasa.

Hii ndio rada iliyonunuliwa kutoka uingereza na kuzaa kashfa ya ufisadi.

Sababu kuu ya kuharibika kwake ni matatizo ya kukatikakatika umeme nchini.

Matengenezo yake yatahitaji vifaa na wataalam kutoka kwenye kampuni ileile ya uingereza uliyotuuzia rada hiyo.

SOURCE: BBC

Rada ya Chenge!!! Ina maana hakuna reliable standby generator za kuiendesha hadi iwe inatumia umeme hata ukiwa na voltage ndogo? Hapo ndiyo deal lingine limeanza, sikilizia!!!! Na waingereza wenyewe wako behind malawi scum!!!
 
ni kweli ndugu yang habari hizo ni za kweli kuhusu radar kwani hata bbc wametangaza hivyo na wakadai kuwa kuna uwezekano mashirika makubwa ya ndege kama qatary na mengineyo yatashindwa kutua kwenye uwanja wetu
 
Mh kazi sasa imeanza upya, waswahili wanasema "Mali ya Dhuluma"... Lakini Chenji si lazima watakua wameingia mkataba ambao una guarantee ya Maintanance.. Na hivi ukiangalia Chenji imerudi na ishapigwa mapanga na huo ununuzi wa vitabu..
 
SiShangai watu wakijichubua, wengine wanaona waukimbie uafrica, mana kama akili zetu watu weusi ndo zinatupeleka huku! Mmmmh, haya ndo imetoka iyo, ndege zitatuwa kwa uzoefu sasa, bongo ubabaishaji mwingi
 
mkuu hii newz ni kweli hata dg wa mamlaka ya anga amekiri kuwa rada ni mbovu. watu wa ndani wanenitonya kuwa sbb rada ni ya kizamani, kifaa kilichoharibika hakitengenezwi tena na waingereza kwa hiyo kuna uwezekano rada yetu ya bei ghali lakini ya kizamani ikawa ni km pambo tu au tembo mweupe. hii ndo bongoland.
 
mkuu kwani rada mnayoiongelea ni ile tuliyoshawishiwa na Toni blea aah sore alishawishiwa ANBEN
 
rada.jpg

Hii wiki ya pili

nadhani mnajua kama BAE SYSTEMS wanataka ma bilioni kuja kuifanyia marekebisho

uzuri rada tuliuziwa na wawekezaji ambao tunawapenda na tunawaona sio matapeli (wazungu)

Ingekuwa tumeuziwa na Waarabu naona kungekuwa kunawaka moto sasa

Kazi kwenu na nchi yenu ya kufikirika. Of course waziri husika hawezi kulaumiwa for obvious reasons ( mtu wenu).

Najua uwanja wa ndege umebadilishwa jina lakini silipendi kulitumia hiyo jina kipya linantia kichefu chefu na naomba uamuzi wangu uheshimiwe
 
Hii wiki ya pili

na nadhani mnajua kama BAE SYSTEMS wanataka ma bilioni kuja kuifanyia marekebisho

uzuri rada tuliuziwa na wawekezaji ambao tunawapenda na tunawaona sio matapeli (wazungu)

Ingekuwa tumeuziwa na Waarabu naona kungekuwa kunawaka moto sasa

Kazi kwenu na nchi yenu ya kufikirika

Najua uwanja wa ndege umebadilishwa jina lakini silipendi kulitumia hiyo jina kipya linantia kichefu chefu na naomba uamuzi wangu uheshimiwe

Mkuu, unaonekana umeingiwa ghafla na msongo wa mawazo...
 
Back
Top Bottom