R.S.V.P kwenye kadi ya mwaliko etc.


Pearl vipi ile ya kwenda na kimywaji chako? Naifagila sana ile nasikia Ujerumani baadhi ya place wanayo. Unakwenda na aina na idadi ya kinywaji utakachotumia ukifika unakabidhi kwa wahudumu wanalabel ukitaka viwekwe kwenye friedge poa tu. Ukikakaa unaanza kuhudumiwa kikiisha hakuna cha ziada Lol!
 
Kwa bongo naona watu huwa hawatilii maanani sana wanaandika kwa kutimiza wajibu tu.
 
mm nadhani tuanze na watoto wetu dia maana kwa sisi wengine ni ngum sana,kwanza hatuna utamaduni wa kurudisha feedback,pililugha inatakiwa kutumika ya kwetu zaidi maana kwenye matamshi ndo kazi sasa,no za cm zinazowekwa pale mostly wanakuwa wanakupigia kuuliza kuhusu deni ninalipwa lini na si zaidi ya hapo so wale pia wapewe elimu ya kuuliza kama mtu atafika au hafiki sio kuuliza lini mtu anamaliza mchango pekeyake.
 
Lily Flower, ni kweli kabisa imefika wakati inabidi tuwe tunaweka msisitizo maana unakwenda kwenye mialiko watu wapo nusu ukumbi! Kama wangesema mapema gharama zingepunguzwa. Pengine Ni vyema sasa tuanze kuweka kwenye kadi: Tafadhali tuma sms au piga simu # ikiwa utahudhuria, kwa vile ukisema ikiwa hutahudhuria watu hawatasema. Hii iandikwe kwa namna mtu anayepokea kadi hatakosa kuiona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…