Nilivyomuona mimi mengi ni mfanya biashara per se mwenye sifa zote za ubepari. Narudia huo ni muono wangu. Sina shida na yeye kuwa bepari. Na ndio maana nikaona ni bora aendelee kwenye channel ya biashara. Nilivyompima nilimuona ana uwezo mkubwa wa kumanage biashara kuliko watu. Ndio maana nina wasiwasi iwapo ataweza kutumanage kama akiwa rais
jmushi1 heshima yako kaka!
hivi leo hii wakisimamishwa mengi na dr slaa nani anaweza kupata kura yako?...ni mfano tu naomba jibu tafadhali
ngoja nikusaidie kitu kimoja, si kila unayemuona anasimama mbele za watu na kuongea na kupigiwa makofi ukahisi anaweza siasa auanaweza kuongoza.
mfano mzuri kwa rais wenu kikwete, alikuwa anajaza watu kwenye mikutano mpaka anakosa hewa anaanguka na kupoteza fahamu, lakini leo hii kila kona ya serikali yake ina uozo. so mi nahisi hata huyo mengi akipewa nafasi sidhani kama ataitumikia kama unavyohisi ukizingatia hajawahi kuwa hata katibu tarafa.
MFANO...marekani kuna wafanyabiashara wakubwa wanaokubalika wenye uwezo wa kusimama na kuongea wakasikika but kwa nini hawajihusishi na siasa?
sasa hapa ndo utapogundua kuwa siasa ni wito...so muache mzee mengi adili na kile anachokiweza
Alitaka kununua Kilimanjaro hoteli akanyimwa na Mkapa
"I have a dream that one day Tanzania will be free from corruption," alisema Mengi kwa Kiingereza akieleza namna anavyotamani kuiona Tanzania ikiwa taifa lisilo na rushwa siku moja.
Hivi kweli Watanzania wenzangu ni kiongozi gani aliyeko in touch na wananchi ambaye ameshawahi kusema maneno kama haya....?
Mbona hayo maneno hata miemi ninayasema almost everyday na nadhani hiyo ni dream ya kila mmoja wetu. Kama Mengi anafaa kuwatumikia wananchi (kama yuko msafi kiasi anachofikiriwa yupo) basi akagombee ubunge, ni nafasi nzuri ya kuwapigania wananchi kuliko hata urais.
jmushi1: Mengi anaweza akawa amefanya mazuri mengi kwa nchi yetu na tunahitaji kumthamini kwa yale aliyotenda, lakini kukimbilia kutaka kumpa urais si suluhisho. Bill Gates ni bepari na amesaidia sana nchi ya Marekani na dunia kwa ujumla, lakini humwoni anakimbilia kugombea, ditto for Rupert Murdoch au Donad Trump. Mi nadhani it is healthy to be discussing this lakini mimi ningemshauri huyu mzee abaki kuwa respeted elder and member of the society, he can do much more like this kuliko kama angekuwa rais.
Also kumbuka kwamba utajiri wake alioupata enzi za Mwinyi, and it was not a clear cut path, I do not judge him, but he does have a number of skeletons in his closet, so akitaka kugombea ajitayarishe for those skeletons come flying out.
Political situation yetu tuliyonayo hivi sasa ni nani msafi kuliko yeye?
Ni vigezo gani kuwa hawezi kutuongoza?
Je una amini kuwa hana kipaji cha uongozi?
Je hauamini kuwa amekuwa jemedari wetu msitari wa mbele kwenye vita dhidi ya umasikini na UFISADI?
Ni mambo gani yanayomkabili Mtanzania wa kawaida kwenye historia karibu yote ya Taifa?
Bill Gates naye ameshawahi kupata tuzo ya MLK?
Hivi umezisoma sababu zote zilizotumika kuwapa both R.Kawawa na R.Mengi tuzo maarufu ya MLK?
Alisema mbali ya kuwezesha vyombo vyake vya habari kufanya habari za uchunguzi, balozi huyo alisema Mengi kama Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT), amewezesha hata waandishi walio nje ya vyombo vyake kuibua habari za ufisadi.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Dk. Salim Ahmed Salim, mzee Rashid Mfaume Kawawa, Jaji Joseph Warioba, Idd Simba, Joseph Butiku, Askofu Kakobe, Askofu Method Kilaini, Sheikh Othman Matata na Askofu Alex Malasusa. Mbali ya Mengi, Watanzania wengine waliokwisha kuzawadiwa tuzo hiyo na miaka yao kwenye mabano ni Rashid Kawawa (2007), Salim Ahmed Salim (2006), Gertrude Mongella (2005), Mama Justa Mwaituka (2004), Profesa Geofrey Mmari (2003), Jaji Francis Nyalali (2002), Jaji Joseph Warioba (2001) na Mwalimu Nyerere (2000).
Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Dk. Salim Ahmed Salim, mzee Rashid Mfaume Kawawa, Jaji Joseph Warioba, Idd Simba, Joseph Butiku, Askofu Kakobe, Askofu Method Kilaini, Sheikh Othman Matata na Askofu Alex Malasusa. Mbali ya Mengi, Watanzania wengine waliokwisha kuzawadiwa tuzo hiyo na miaka yao kwenye mabano ni Rashid Kawawa (2007), Salim Ahmed Salim (2006), Gertrude Mongella (2005), Mama Justa Mwaituka (2004), Profesa Geofrey Mmari (2003), Jaji Francis Nyalali (2002), Jaji Joseph Warioba (2001) na Mwalimu Nyerere (2000).