R. Kelly anaweza akawa ana matatizo ya kingono!

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,232
113,610
R. Kelly ni mwimbaji aliye gwiji. Ana kipaji kikubwa sana. Binafsi nazipenda sana nyimbo zake.

Ila, huyu jamaa huenda akawa ana matatizo ya kingono. Tuhuma za yeye kujihusisha na visichana vidogo hazijaanza leo wala jana.

Kwa kumbukumbu zangu, tuhuma hizo nilianza kuzisikia tokea 1994 pindi Aaliyah alipoibuka.

Baadaye akaja kutuhumiwa kujirekodi kwenye video akifanya ngono na kasichana kengine kadogo 'teenager' mwaka 2003 kama sijakosea.

Hiyo ilipelekea hadi yeye kushitakiwa kwa kutengeneza video za ngono na mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18. Hiyo kesi alishinda ingawa ilimgharimu sifa yake kwenye jamii.

Sasa jana kukaibuka na tuhuma zingine tena za yeye kuwanyanyasa wanawake wenye umri mdogo kwenye nyumba zake za Atlanta na Chicago.

Mwenyewe kazikanusha hizo tuhuma. Hilo ni suala la kutegemewa maana sidhani kama anaweza tu kukiri bila mshikemshike kuwa hizo tuhuma ni za kweli.

Kiunganishi cha hiyo habari ya jana hiki hapa: R. Kelly accused of abusing women, running 'cult' in Johns Creek

Jana, familia ya mmoja wa hao wasichana [Joycelyn Savage] wanaodaiwa kuwa ndo wamewekwa ndani na R. Kelly huko Johns Creek, GA, waliitisha mkutano na waandishi wa habari.

Na hivi ndivyo walivyosema.

Baba wa huyo Joycelyn ndo huyo jamaa anayezungumza. Anaitwa Timothy Savage.

Fast forward mpaka leo [tarehe 18 July], binti mtu, Joycelyn kajibu mapigo kwa kurusha hii video huko YouTube.

Joycelyn anadai baba'ake kamuaibisha na pia kaiaibisha familia nzima kwa kufanya mkutano na waandishi wa habari hiyo jana.

Polisi wa Johns Creek nao wamesema hawana la kufanya kama hao wadada wanaishi hapo nyumbani kwa R. Kelly kwa ridhaa yao wenyewe hususan kama wapo na umri zaidi ya miaka 18.

This thing is so bizarre. And R. Kelly has been dogged by these allegations of him liking young girls for decades now.

With him I definitely think there is fire behind or underneath the smoke!
http://www.ajc.com/news/local/kelly...ning-cult-johns-creek/ZejyB7KbyykVWptYuw5ZNP/
 
Nakumbuka nikiwa sekondari "kipindi shule zikiwa shule elimu ikiitwa elimu" nilikuwa na rafiki yangu alikuwa akimuita bwana R.Kelly mzee wa bikra (mpenda vibinti vibichi).

Lakini kwanini matukio/kafsha hizi zinamkumba bwana huyu ...? Kwanini wasiwe wengine...? Na kwanini iwe maranyingi kiasi hicho..?

Tuamini kwamba Kuna watu huwa wanamchafua bwana huyu..?

Mimi naamini kunaukweli kiasi flani bwana huyu kupenda damu mbichi!!
 
Fataki la karne ya 21 hilo.... Sema mvua za ng'ambo hazinaga mashiko,, Ingekua bongo angepata ujirani na babu Sea na kazi ngumu.. Watengeneze bendi huko jela wakibonda kokoto

Ila jamaa mwisho wake unaweza kuja kuwa mbaya sana.

Mwaka 2008 aliponea chupuchupu kula mvua ndefu.

Inavoelekea hajajifunza....kama vile ambavyo OJ hakujifunza.
 
Nakumbuka nikiwa sekondari "kipindi shule zikiwa shule elimu ikiitwa elimu" nilikuwa na rafiki yangu alikuwa akimuita bwana R.Kelly mzee wa bikra (mpenda vibinti vibichi).

Lakini kwanini matukio/kafsha hizi zinamkumba bwana huyu ...? Kwanini wasiwe wengine...? Na kwanini iwe maranyingi kiasi hicho..?

Tuamini kwamba Kuna watu huwa wanamchafua bwana huyu..?

Mimi naamini kunaukweli kiasi flani bwana huyu kupenda damu mbichi!!

Hata mimi naamini kuna ukweli kiasi chake juu ya hizo tuhuma dhidi yake.

Tokea 1994 jamaa anatuhumiwa na hayo mambo na kuhusu visichana tofauti tofauti.....

He needs help.
 
Ila jamaa mwisho wake unaweza kuja kuwa mbaya sana.

Mwaka 2008 aliponea chupuchupu kula mvua ndefu.

Inavoelekea hajajifunza....kama vile ambavyo OJ hakujifunza.

Ni kweli kabisaa

Siku itakuja atanutana na kiboko yake na mengine mengi... pesa ataiona karatasi as haitamsaidia kuzima chochote.

Leo nakupa huo my kaka enjoy

Visichana ni vidogo vidogo ni vitamu balaa, ukionja huwezi acha

sent from Sanduku la Posta using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli kabisaa

Siku itakuja atanutana na kiboko yake na mengine mengi... pesa ataiona karatasi as haitamsaidia kuzima chochote.

Leo nakupa huo my kaka enjoy

Shukran jazilan my Coco.

Nami nakupa huu.

Usikilize kwa makini. Sikiliza maneno yake.

Napapenda zaidi hapo mwisho...booty..boooty...booohoooty....:p.

Ila kwa kweli Kells ana kipaji cha uimbaji na utunzi.

Kwa hilo nitampa sifa zake.

Haya iangalie video sasa.....
 
Na Aaliyah, of course kutokana na mikono ya Kelly mwenyewe, wakaamua ku-confirm na Age Ain't Nothing But A Number!!

Kwa kweli jamaa mimi nadhani ana matatizo.

Kuna taarifa kuwa yeye na Aaliyah walifunga ndoa kabisa.

Sad,
 
Kwa kweli jamaa mimi nadhani ana matatizo.

Kuna taarifa kuwa yeye na Aaliyah walifunga ndoa kabisa.

Sad,
Aaliyah kagonga kagonga kabisa... tutashindwa kulitolea ushahidi tu lakini wala halina mjadala! Tena aligonga wakati Aaliyah akiwa U-16 huku Kelly mwenyewe akiwa anaitafuta 30! He's nearly twice Aaliyah's age!

In short, jamaa is kind of pedophile kama sio pedophile kabisa!
 
Ila jamaa mwisho wake unaweza kuja kuwa mbaya sana.

Mwaka 2008 aliponea chupuchupu kula mvua ndefu.

Inavoelekea hajajifunza....kama vile ambavyo OJ hakujifunza.
hivi hana mke ? akatibiwe huenda kuna chanzo cha haya anayofanya may be alikuwa abused utotoni
 
Back
Top Bottom