R.I.P Al-Baghdad

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Kifo cha al-Baghdad: Marekani imeufunga ukurasa wa kitabu chake yenyewe.

Ibrahim Awad Ibrahim Ali al-Badri al-Samarrai huwenda likawa jina jipya kabisa kwa wasomaji na wafuatiliaji wa siasa za kimataifa.

Huyo ndiye aliyejulikana pia kwa majina ya "Abu Bakr al-Baghdad", "Caliph Abu Bakr al-Baghdad", "Caliph Ibrahim", " The Invisible Sheikh", "Al-Shabah (The ghost)", " Abu Du'a" n.k

Ibrahim alizaliwa katika kitongoji cha Samarra kilichopo ukingo wa mashariki wa mto Tigris katika jimbo la Saladin lililopo kilometa 125 kaskazini mwa jiji kuu la Baghdad, nchini Iraq. Ibrahim anatokea kabila la Banu Badri. Alikulia na kusomea jijini Baghdad.

Hii ndio ilipelekea katika utambulisho wake ajitaje kama "al-Badri" (mtu wa kabila la Badri), "al-Samarrai" (mtu kutoka kitongoji cha Samarra), "al-Baghdad" (mtu kutoka Baghdad) kama hiyo haitoshi akajipachika pia wadhifa wa Khalifa (kiongozi wa Juu wa Dola) n.k

Ni kawaida kwa waarabu wanapotaja utambulisho wao basi hujimwambafy pia kwa kutaja makabila yao, vitongoji vyao, miji yao, asili zao, sifa zao n.k

Ibrahim alikuwa muumini wa madhheb ya Salafi na ni msomi aliyejikita kwenye fani za Sheria, Elimu ya Sayansi, Lugha na Sharia za Kiislamu. Elimu yake ya Juu aliipata katika Chuo Kikuu cha Baghdad (University of Baghdad), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Baghdad (Islamic University of Baghdad) na Chuo Kikuu cha Saddam (Saddam University of Baghdad). Anatajwa kuwa na Shahada (BA), Shahada ya Umahiri (MA) na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani zilizotajwa hapo juu.

Asubuhi ya Jumapili 27/10/2019 Wamarekani na Dunia kwa ujumla waliamshwa na ujumbe kutoka ukurasa wa Tweeter unaotumiwa na Rais Donald Trump uliosomeka "Jambo kubwa limefanyika", wengi walipata shauku ya kutaka kujua kumefanyika nini? Baadae taarifa zikaanza kuenea kuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu (IS) Abu Bakr al-Baghdad ameuawa katika operesheni ya kijeshi ya vikosi vya Marekani huko Syria.

Muda mfupi baadae Rais Donald Trump alijitokeza mbele ya kamera za vyombo mbalimbali vya habari akauthibitishia Ulimwengu kuwa Abu Bakr al-Baghdad ameuawa na akaongeza kuwa amejilipua mwenyewe kwenye handaki pamoja na watoto watatu akiwa mtu dhalili mwenye kutapatapa huku akikimbia na kulia kama mbwa.

Huko nyuma imewahi kuripotiwa zaidi ya mara nne kuwa Al-Baghdad aliuawa kwenye mashambulio yaliyofanywa na vikosi vya Marekani lakini baadae akaibuka, akatangazwa kuuawa tena kisha akaibuka, akauawa na kuibuka. Ni wazi safari hii ndio mwisho rasmi wa sinema ya Abu Bakr al-Baghdad kufa na kuibuka.

Hivi ndivyo Marekani ilivyoamua kuufunga ukurasa wa kitabu chake yenyewe.

Kwa nini kitabu chake yenyewe?

Taarifa zinaeleza kuwa, baada ya kuhitimu elimu yake ya Juu, Ibrahim alipata kuajiriwa kama afisa kwenye kikosi maalumu cha kijasusi cha Ulinzi wa Jamuhuri (Republican Guard) wakati wa utawala ulioangushwa wa Rais Saddam Hussein. Kikosi hicho kilikuwa chini ya uongozi wa Uday na Qusay ambao walikuwa watoto wa marehemu Rais Saddam Hussein waliouawa wakati wa uvamizi wa majeshi ya Marekani nchini Iraq.

Ibrahim alikuwa mmoja wa wapiganaji waliokamatwa na vikosi vya Marekani April 2003 vilipouteka mji wa Baghdad katika zile siku 21 za Mpambano wa Baghdad (The Battles of Baghdad) na mji huo kutekwa na Marekani. Ibrahim alikamatwa na akapelekwa kwenye jela ya siri ya Marekani nchini Australia ambayo ilikuwa maalumu kwa ajili ya wafungwa wa kivita na wapiganaji wa makundi ya kigaidi.

Miaka kadhaa baadae 2011 nchini Tunisia liliibuka vuguvugu la mapinduzi ya tawala mbalimbali za kiarabu za muda mrefu (Arab Spring) ambalo baadae lilisambaa kwenye nchi kadhaa za kiarabu huku likipelekea tawala kadhaa kuanguka kama vile Tunisia, Libya na Misri.

Kwa Marekani, Arab Spring licha ya kupelekea washirika wake muhimu kama Hosni Mubarak wa Misri kutupwa nje ya mamlaka lakini pia iligeuka kuwa fursa muhimu kwake kuitumia dhidi ya viongozi na watawala ambao kwa muda mrefu wamekuwa kikwazo ama hatari kwa maslahi ya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Hivyo Marekani ilimtuma Seneta John McCain aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Seneti ya Bunge la Marekani inayohusika na masuala yote ya huduma za Jeshi, Ulinzi na Usalama (Senate Armed Services Committee -SASC) kwenda eneo la Mashariki ya Kati ambapo alifanya vikao mbalimbali vya siri na vya wazi na maafisa wa jeshi la Marekani walioko huko pamoja na makundi ya wapinzani na yale ya wapiganaji dhidi ya tawala ambazo zimekuwa kikwazo au kitisho dhidi ya maslahi ya Marekani katika eneo hilo. Lengo kuu likiwa ni kupanga mikakati na kuitumia fursa ya vuguvugu la Arab Spring kuziadabisha tawala hizo. Syria ya Bashar al-Assad ilikuwa moja ya waliolengwa na mkakati huo wa Marekani.

Moja ya matunda ya kazi hiyo ni upinzani ulioibuka 18/04/2011 katika mji wa Homs huko nchini Syria dhidi ya utawala wa Bashar al-Assad. Japo upinzani huo ulibeba anuani ya madai ya demokrasia, haki za binaadamu, ukosefu wa ajira, kukidhiri kwa rushwa na ukiukaji wa misingi ya utawala bora lakini nyuma ya pazia kulikuwa na ajenda iliyojificha ya kuuadabisha na kuung'oa utawala wa Bashar al-Assad ulioonekana kama kikwazo na kitisho dhidi ya maslahi ya Marekani.

Serikali ya Syria ilipojaribu kuuzima upinzani huo ndio kama ilikuwa imemwagia mafuta kwenye pipa la petrol maana upinzani ulipamba moto na kugeuka ghasia za umwagikaji wa damu zilizobadilika na kuwa mapambano kamili ya silaha baina ya vikosi vya Serikali na Wapiganaji.

Marekani kuona hivyo ikawakusanya haraka nchi washirika wake na wakaunda umoja wao waliouita Marafiki wa Syria (Friends of Syria). Umoja huu lengo lake likawa ni kuwasaidia makundi ya wapiganaji ili kumporomosha Bashar al-Assad.

Friends of Syria walifanya vikao vyao Doha, Qatar kisha Paris, Ufaransa na kingine London, Uingereza. Wakakusanya michango ya fedha, Silaha na ahadi ya mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya vikosi vya wapiganaji dhidi ya utawala wa Bashar al-Assad.

Kwa kuwa wapiganaji wengi waliojitokeza kupambana na utawala wa Assad walitokea kwenye makundi ya wapiganaji wa Jihad ambayo yaliunda umoja wao yaliouita Majeshi ya Ukombozi wa Syria (Free Syrian Army - FSA). Baadhi yake makundi hayo yalishakuwa yameorodheshwa na Marekani kama makundi ya kigaidi Duniani hivyo iliwabidi Friends of Syria (Marekani na Washirika wake) kuwa makini katika kutoa misaada yao ya fedha, silaha na mafunzo. Waliamua kupandikiza kundi la wapiganaji ndani ya wapiganaji hao wa FSA ili misaada yao ifikie mikono salama.

Wakati hali ikiwa ya sintofahamu huko Syria kuna jambo lisilo la kawaida lilikuwa linaendelea katika viunga vya Baghdad.

Afisa wa zamani wa kikosi katili cha utawala Saddam Hussein cha Republican Guard na mfungwa wa jela ya siri ya Marekani huko Australia Ibrahim Awad Ibrahim Ali al-Badri al-Samarrai alikuwa mtu huru akirandaranda kwenye viunga vya Baghdad huku akiandikisha wapiganaji. Wengi walishangaa vipi mtu huyu amekuwa huru na vipi anaweza kujiamini na bila woga kuandikisha wapiganaji mbele ya vikosi vya Marekani vinavyoudhibiti mji wa Baghdad?

Jibu la alichokuwa anafanya Ibrahim lilifahamika pale alipotangaza kuwa yeye pamoja na wapiganaji wake wamevuka mpaka na kuingia Syria kuungana na wapiganaji wa Free Syrian Army ili kumkabili na kumuondoa mamlakani Rais Bashar al-Assad.

Machi 2013 Seneta John McCain katika mlolongo wa shughuli zake katika eneo hilo aliingia Syria kwa siri akitokea Uturuki na kupiga kambi katika mji wa Idlib ambapo alifanya kikao cha siri na viongozi waandamizi wa wapiganaji wa FSA. Wakapanga mikakati ya namna kundi hilo litakavyopokea msaada wa Fedha, Silaha na Mafunzo ya kijeshi unaotoka kwa Nchi za Friends of Syria ili kumkabili Rais Bashar al-Assad.

Taarifa kuhusu kikao cha Seneta John McCain na viongozi waandamizi wa muungano wa wapiganaji wa FSA zilibaki kuwa siri mpaka aliporejea Washington. Na picha iliyotolewa na kusambaa mitandaoni (nimeiambatanisha) ilimuonesha Seneta John McCain akizungumza na viongozi hao wa FSA akiwamo mkuu wao Amir Idris Salem (Brigadier General Salem) lakini pia alikuwapo Mouaz Moustafa msemaji wa kundi la FSA, alikuwepo Mohammed Nour aliyekuwa msemaji wa Al-Nusra Front Brigade, alikuwepo Abu Mosa aliyewahi kuwa mpiganaji wa al-qaeda tawi la Iraq na pia alikuwepo Ibrahim Awad Ibrahim Ali al-Badri al-Samarrai (Abu Bakr al-Baghdad).

Msemaji wa Ikulu ya Marekani wakati huo Jay Carney alipoulizwa kuhusu safari hiyo ya Seneta John McCain nchini Syria alikiri kuwa Ikulu inafahamu tangu mwanzo mipango ya safari za Seneta McCain nchini Syria ingawa alikataa kusema kama safari hizo zinabeba ujumbe maalumu wa Ikulu ya Marekani kwenda huko Syria.

Miezi kadhaa baadae kundi la FSA lilijikuta kwenye mgongano na mparaganyiko wa ndani na sababu hasa ilikuwa ni Ibrahim Awad Ibrahim Ali al-Badri al-Samarrai (Abu Bakr al-Baghdad) aliyekuwa anataka yeye ndio awe Amir (kiongozi mkuu) wa FSA.

Wenzake walimkatalia baada ya kumtilia shaka hasa kutoka na ukaribu aliokuwa akiuonesha na kuaminiwa zaidi na Nchi za Friends of Syria zilizoongozwa na Marekani kama mpokeaji wa misaada yote inayoletwa kwa FSA ilihali hakuwa na nafasi yoyote kubwa ya uongozi ndani ya kundi hilo. Kundi la Ibrahim likaasi FSA na kutwaa baadhi ya miji na kuitangaza kuwa chini ya udhibiti wake.

Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya Syria, huko Iraq nako kulikuwa na jambo lingine likiendelea. Wananchi wengi wa Iraq walianza kuchoshwa na uwepo wa muda mrefu wa vikosi vya kigeni nchini mwao. Hivyo wakaanza kumshinikiza Waziri Mkuu wao Nour al-Malik wakati huo avitake vikosi vya Marekani viondoke nchini Iraq.

Waziri Mkuu wa Iraq Nour al-Malik katika kuitikia wito wa RAIA wa Iraq akavitaka vikosi vya Marekani vifungashe virago viondoke nchini humo. Marekani ikamwambia Iraq sio salama lakini kwa kuwa ametaka waondoke wataondoka ila lolote litakalotokea basi atawajibika mwenyewe.

Ibrahim Awad (Abu Bakr al-Baghdad) akaongoza vikosi vyake vya Jamaat Jaysh ahl-Sunnah wal-Jamaah kutoka Syria na kuvuka mpaka na kuingia Iraq akiteka miji na vijiji mpaka akautwaa mji wa Mosul na kupanga vikosi kutishia kuiteka Baghdad. Hofu kubwa ikatanda nchini Iraq na vikosi vya Iraq havikuweza kuvimudu vikosi vya Ibrahim vilivyoonekana kusheheni silaha za kisasa (vifaru na magari ya deraya) na wapiganaji kwenye mafunzo makali ya kivita. Marekani ikamwambia Nour al-Malik ulitaka tuondoke sasa pambana na hao wavamizi kama una uwezo.

Marekani ikampa masharti al-Malik kama anataka imsaidie na pia kuwasaidia jamii ya Yazid waliokuwa wamezingirwa milimani kwa siku kadhaa basi ajiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu achaguliwe mwingine nao wataisaidia Iraq dhidi ya wavamizi hao.

Nour al-Malik chini ya shinikizo la Marekani na kitisho kutoka kwa vikosi vya Ibrahim Awad vinavyojongea kutaka kuiteka Baghdad akalazimika kusalimu amri akajiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu. Marekani ndio ikaamrisha vikosi vyake kuvidhibiti vikosi vya Uvamizi.

Ni wakati huo, 29/06/2014 ndipo Ibrahim Awad akitumia mimbari ya msikiti wa Ijumaa wa Mosul alitangaza kuwa ameunda Dola ya Kiislamu katika eneo lote analolidhibiti la Iraq na Syria (Islamic State of Iraq and Lavent - ISIL) na akajitangaza kuwa yeye ndio kiongozi Mkuu wa Dola hiyo yaani Khalifa na kujitambulisha kuwa yeye ndie Khalifah Abu Bakr al-Baghdad (Khalifa Abu Bakr wa Baghdad).

Katika Uislamu, Seyyidina Abu Bakr Sadiq (r.a) ndiye alikuwa Khalifa wa kwanza wa Dola ya Kiislamu baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad (saw). Hivyo Ibrahim Awad nae akajinasibisha kwa kuchukua jina hilo.

Uislamu kama dini unataratibu zake za kuunda Dola na kuchagua Khalifah wa Dola. Alichofanya Ibrahim ilikuwa ni kinyume cha sharia na mafundisho ya Uislamu. Ndio maana Ulimwengu wa Kiislamu ulijitenga mbali na ukhalifa wake aliojitangazia mwenyewe Ibrahim Awad (Abu Bakr al-Baghdad).

Kundi la ISIL (Islamic State of Iraq and Lavent) lilibadili jina lake na kuwa ISIS (Islamic State of Iraq and Syria) na baadae IS (Islamic State) ama pia likiitwa "Daesh".

Wachambuzi na watafiti wa siasa za kimataifa na hasa masuala ya vita dhidi ya ugaidi wanalitazama kundi la Dola la Kiislamu (IS) kama "kikaragosi" kilichotengenezwa maalumu, kwa ajenda maalumu na kwa kazi maalumu ili kutimiza malengo maalumu.

Mara kadhaa kundi hili limekuwa likifanya mashambulizi na mauwaji ya kikatili dhidi ya wasio na hatia. Wakati mwingine limekuwa likitengeneza video za kurekodi studio zikionesha wapiganaji wake wakiwachinja mateka wao. Lengo ni kuibua hali ya taharuki na hofu katika jamii kisha ajenda fulani zinatekelezwa nyuma ya kivuli cha vita dhidi ya ugaidi.

Lakini pia kundi hili limekuwa likitumika kuwavuta na kuwanasa vijana wenye hisia na misimamo mikali ya Dini ambao wamekuwa wakivutiwa na matukio yake na wakiaminishwa kwamba linauwakilisha Uislamu na wengi waliokurupuka na kwenda kujiunga nalo wamejikuta wakiishia kukamatwa na kufungwa kwenye jela za wapiganaji au kuuawa kama mbwa.

Hivi karibuni Rais Donald Trump alifanya maamuzi ya kuyaondoa majeshi ya Marekani nchini Syria akitaja kwamba Marekani haiwezi kuendelea kufanya kile alichokiita "vita isiyokwisha".

Kitendo cha kuyaondoa majeshi ya Marekani katika miji ya mpakani ya Syria kiliipa Uturuki nafasi ya kuivamia na kuishambulia kijeshi Syria ikidai kuwa inawalenga wapiganaji wa Kikurdi wa YPG ambao kwa muda mrefu walikita maskani na kuendesha harakati zao katika maeneo hayo wakiwa sambamba na Majeshi ya Marekani.

Syria na Urusi nazo zilianza kusogeza majeshi yao hapo mpakani. Huenda kwa kufanya hivyo wangeweza baadae kumkamata Ibrahim (Abu Bakr al-Baghdad) kutoka kwenye maficho yake hapo Idlib. Kama angekamatwa na kushikiliwa na wasio Wamarekani huwenda siri nyuma ya pazia ingefahamika. Jambo ambalo lingeweza kuifedhehesha Marekani.

Ni katika muktadha huo inawezekana Marekani ilibaini kuwa kuna jambo imeliacha bila kulikamilisha. Kuna ukurasa wa kitabu chake yenyewe imeuacha wazi bila kuufunika. Nao ni kuondoa ushahidi wa uwepo wa Ibrahim Awad (Abu Bakr al-Baghdad). Sio jambo la ajabu watu kufuta ushahidi pale wanapoona hawana haja nawe tena. Unakuwa ni rafiki na mtu wao katika kipindi kile tu wanakutumia kwa maslahi yao lakini wakishaona hauna tena msaada kwao au wakiona hawana tena haja nawe basi wanakupoteza tu inabaki historia.

Ibrahim (Abu Baghdad) ameuawa akiwa dhalili anatapatapa, anakimbia na kulia kama mbwa kisha kujilipuwa mwenyewe ndani ya handaki.

Ifahamike kuwa mpaka anajilipuwa mwenyewe kwenye handaki katika kijiji cha Barisha jimbo la Idlib nchini Syria (mahala alipokutana na Seneta John McCain mwaka 2013), baada ya kuona amezingirwa na washirika wake wa zamani Ibrahim (Abu Bakr al-Baghdad) hakuwa tena kiongozi wa IS.

Mnamo Agosti 2019 Ibrahim alishakabidhi uongozi wa IS kwa Abdullah Qardash al-Afar. Lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Ibrahim anafahamu mengi sana kuhusu ISIL, ISIS, IS na Daesh kuliko mtu mwingine yeyote.

Mrithi wake Abdullah Qardash al-Afar nae alikuwa mfungwa wa kivita katika jela ya Marekani ya Camp Bucca. Jela hii iko katika mji wa bandari wa Umm Qasr jimbo la Basra lililoko kusini mwa Iraq. Hii iliundwa mwaka 2003 baada yakufungwa kwa jela ya Abu Ghraib iliyokumbwa na kashfa ya mateso na udhalilishaji. Wafungwa 20,000 walihamishwa kutoka Abu Ghraib na kuhamishiwa Camp Bucca.

Jela ya Camp Bucca (Ronald Bucca) imekuwa ni jela ambayo Marekani wameitumia kuwabadili tabia wafungwa wa kivita na kuwapa mafunzo ya kimaadili lakini leo hii ndio imetoa kiongozi mpya wa IS, Abdullah Qardash al-Afar.

Je, Qardash al-Afar atakuwa sawa na mtangulizi wake Ibrahim au nae ni ukurasa mpya wa kitabu cha Marekani kutoka Camp Bucca? Tusubiri tuone.

@jofumaster
 
Dini zimefanya dunia kuwa sio sehemu salama ya kuishi,Mimi naona maada yako ina lengo la kuficha ukweli kuwa makundi yote ya msimamo mkali yanampigania Allah.alikaida,alnusra,Boko haramu,alshababu n.k.hao nao je?msipindishe ukweli,wengine tulionao kwa jamii wameficha makucha tu na kwa sababu ya sheria za nchi husika la sivyo sijui ingekuwaje.
Nukta.
 
Alqaeda,Alshabab,Isis
Ngoja tusubiri tena US atatengeneza kundi gani tena lingine
stay tuned
 
Alqaeda,Alshabab,Isis
Ngoja tusubiri tena US atatengeneza kundi gani tena lingine
stay tuned
USA mjanja sana anawatumia warabu kama condom Sitashangaa baadae Meca na Madina inakuwa chini ya Marekani halafu anajenga hotel za kitalii. Warabu hawana akili ni bora hata na wachina wanatengeneza simu ila wao wanawaza kuchinjana tu na USA anawapa silaha wachinjane vizuri. Miaka 3000, Middle East yote itakuwa chini ya USA.
 
haitokuja tokea mwarabu akapata akili"makafiri hawa"
USA mjanja sana anawatumia warabu kama condom Sitashangaa baadae Meca na Madina inakuwa chini ya Marekani halafu anajenga hotel za kitalii. Warabu hawana akili ni bora hata na wachina wanatengeneza simu ila wao wanawaza kuchinjana tu na USA anawapa silaha wachinjane vizuri. Miaka 3000, Middle East yote itakuwa chini ya USA.
 
Ukiacha kuwaza kwa kutumia WOWOWO unitag
Dini zimefanya dunia kuwa sio sehemu salama ya kuishi,Mimi naona maada yako ina lengo la kuficha ukweli kuwa makundi yote ya msimamo mkali yanampigania Allah.alikaida,alnusra,Boko haramu,alshababu n.k.hao nao je?msipindishe ukweli,wengine tulionao kwa jamii wameficha makucha tu na kwa sababu ya sheria za nchi husika la sivyo sijui ingekuwaje.
Nukta.
 
Mtia mada umeongea exactly what it is

Ila nnachofurahi mwisho wa siku hii dunia yoye itafinyangwafinyangwa na kurudi mikononi mwa Mungu...

Wapuuzi wote watakua vumbi kisha watafufuliwa na kuwekwa kwenye uwanja wa hukumu

Nao watakua wanyonge sana na watayajutia makosa yao

Kama tungalikua tunaishi milele ningeliwaunga mkono kwenye hizo figisu wanazozifanya kwa their fellow humans

Ula kwa kua umri wetu ni masaa machache tu yawezayo kuhesabika kwa kalkuleta ya digital ........wait
 
Huyu jamaa nadhani wamemuua sababu mission ya kumtoa Al Bashar ameshindwa kuikamilisha.

Ila Osama huenda yupo mahali anakula zake bata maana alikamilisha missions nyingi za USA kwa ufanisi wa hali ya juu.

Unforgetable
hivi bin laden alikuwa ana uhusiano gani na marekani ukitoa ile vita ya urusi na afghanistan??
 
nishakusoma
Mengi ya matishio ya dunia kwa sasa ni haya kumpigania mungu,nakumbuka enzi za isis watu furani waliunga mikono lakini ilipoanza kupoteza wamegeuka eti ni mpango wa marekani.hii ni mipango ya dini tena dhehebu Fulani..NUKTA.
 
Kama ni kweli marekani anafanya kazi za kihuni kiasi iki
Karma is bitch so kuna siku atavuna anachopanda.
 
Back
Top Bottom