Niliyasema haya niliporudi kutoka Bongo, kuwa viongozi wetu sasa hivi wanagawana ardhi kubwa zenye kusadikika kuwa zina madini.
Sisi wananchi walalahoi tunaambia ardhi ni mali ya serikali na hata imefikia wachimbaji wadogowadogo kufukuzwa katika makazi yao lakini wao wanaweza kuchukua hizi ardhi na kudai kuwa zao tena basi kuleta makampuni ya kuchunguza madini (mine exploration) kama vile hizi ardhi ni mali yao na kila kilichomo.. Inasemekana kwa uchache sana kama kuna madini basi viongozi hawa hudai mabillioni ya fedha toka makampuni ya nje.
Just the other day, we learnt that a minister in the current government actually owns a gemstone mine. This gives us the impression that we probably have a cabinet full of ministers who are inspired by money and personal wealth.
~Professor Mwesiga Baregu
Jamani kuuliza si ujinga. Hivi kiongozi anatakiwa awe mwasikini? Mfano jamani huku nakuwa popo (huko US mnasema kubeba mabox) Nikijipatika kamtaji kangu nikaenda nyumbani na kumiliki mgodi si wezi kuwa kiongozi? Nadhani kama ni pesa ya halali ni sawa tuu kuliko hao makaburu na wacanada ambao wanachukua kila kitu ila kama mtaji ulipatikana kiusisadi nadhani hapo ndio kiongozi hafai. Jamani hayo ni mawazo yangu tuu.
Hatujakataa katu Kiongozi kuwa na pesa tunachokataa yeye akiwa angali ni waziri ofisini anamiliki mali nyingi kiasi hicho, kuna maadili na miiko ya viongozi havimruhusu kuwa hivyo alivyo. Mfano ni huu kuwa kiongozi wakati huo huo ni mfanya biashara lazima mambo mengi ya kiofisi utayamuvuzisha katika miradi yako. Isitoshe hata kuwajibika kwako kiofisi itakuwa ni kwa kiwango kidogo sana hii imefanyiwa utafiti hatutoi vichwani mwetu. Huwezi kupanda farasi wawili ukafanikiwa kuwaelekeza unakotaka.
Mimi naona tuangalie kama utajiri umepatikana kihalali waache wamiliki nchi imeshatoka kwenye ujamaa ni nchi ya kibepari hii mkuu.
.
True Kabisa Mkuu....Niliyasema haya niliporudi kutoka Bongo, kuwa viongozi wetu sasa hivi wanagawana ardhi kubwa zenye kusadikika kuwa zina madini.
Sisi wananchi walalahoi tunaambia ardhi ni mali ya serikali na hata imefikia wachimbaji wadogowadogo kufukuzwa katika makazi yao lakini wao wanaweza kuchukua hizi ardhi na kudai kuwa zao tena basi kuleta makampuni ya kuchunguza madini (mine exploration) kama vile hizi ardhi ni mali yao na kila kilichomo.. Inasemekana kwa uchache sana kama kuna madini basi viongozi hawa hudai mabillioni ya fedha toka makampuni ya nje.
Kahama Geita watu wanaumasikini wa KUTUPWAA.....Hawa viongozi wote tunawajua walikuwa na hali za kawaida kabisa. Hawakuwa matajiri, hivyo utajiri waliokuwa nao sasa hivi umepatikana kwa njia za haramu ndiyo maana hata Mkapa anashindwa kujibu tuhuma chungu nzima za mambo aliyoyafanya akiwa Ikulu. Hivi ni tamko lipi lililosema Tanzania ni nchi ya kibepari? Itakuwa vizuri ukiliweka hapa ili tujue lilitamkwa lini na nani.