Quote of the Week

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,045
Just the other day, we learnt that a minister in the current government actually owns a gemstone mine. This gives us the impression that we probably have a cabinet full of ministers who are inspired by money and personal wealth.

~Professor Mwesiga Baregu
 
Niliyasema haya niliporudi kutoka Bongo, kuwa viongozi wetu sasa hivi wanagawana ardhi kubwa zenye kusadikika kuwa zina madini.

Sisi wananchi walalahoi tunaambia ardhi ni mali ya serikali na hata imefikia wachimbaji wadogowadogo kufukuzwa katika makazi yao lakini wao wanaweza kuchukua hizi ardhi na kudai kuwa zao tena basi kuleta makampuni ya kuchunguza madini (mine exploration) kama vile hizi ardhi ni mali yao na kila kilichomo..

Inasemekana kwa uchache sana kama kuna madini basi viongozi hawa hudai mabillioni ya fedha toka makampuni ya nje.
 
Niliyasema haya niliporudi kutoka Bongo, kuwa viongozi wetu sasa hivi wanagawana ardhi kubwa zenye kusadikika kuwa zina madini.
Sisi wananchi walalahoi tunaambia ardhi ni mali ya serikali na hata imefikia wachimbaji wadogowadogo kufukuzwa katika makazi yao lakini wao wanaweza kuchukua hizi ardhi na kudai kuwa zao tena basi kuleta makampuni ya kuchunguza madini (mine exploration) kama vile hizi ardhi ni mali yao na kila kilichomo.. Inasemekana kwa uchache sana kama kuna madini basi viongozi hawa hudai mabillioni ya fedha toka makampuni ya nje.

Mkandara, kwa kuongezea tu wanagawana ardhi ambayo ina rasilimali namely madini. Nasikia Mawaziri wenye migodi ya madini wako wengi tu si Kapuya pekee yake, na wengine wa awamu ya tatu ambao sasa hivi wanakula kuku kwa mrija, wakati asilimia kubwa ya Watanzania ikiishi katika umaskini wa kutisha.
 
Nimeshitushwa sana na taarifa kwamba Waziri Kapuya anamiliki mgodi wa madini, hii bila shaka ukiukaji wa maadili na miiko ya uongozi. Kitendo cha kiongozi kama waziri kumiliki mali kubwa kiasi hicho ni picha mbaya kwa wananchi kwani imani ya wananchi kwa serikali inapotea kabisa, hivi Nyerere aliongozaje nchi, inaonyesha kwamba hawa waliopo madarakani walifuarahi sana kufa kwake maana mambo mengi na ya ajabu yameibuka kwa ghafla baada ya kifo chake.

Hebu check hata aliowaamini Mwalimu wamekuwa mafisadi wakubwa, kwanini mnaichakaza nchi namna hii je mmesikia kesho mwisho wa dunia? Kumbukeni kwamba ipo siku hamtakuwa na uwezo wa kuinua hata vidole vya mikono yenu na miili yenu itatengana na uhai wenu na mali zenu, na ndugu zenu, na hapo mlipo ingawa siku hizi mnawateua watoto wenu kushika madaraka ili kulinda maslai yenu mkizeeka wataondoshwa kwa nguvu kwani "You can cheat a person all the time but you can not cheat all the people all the time" Mmekuwa waongo sana kwa wananchi kwamba mtawaletea maendeleo kumbe afadhali mngekuwa mnasema mtawaletea umaskini tukawa tayari kwa hilo kuliko hadaa zenu.

Mtu kazalia na amekulia Ikulu kazeekea Ikulu anataka kufia Ikulu na atataka azikwe Ikulu. Mnajifanya waadilifu kiuongozi wakati ni wabadhirifu wa mali za umma. Ipo siku mtavuna mnachokipanda.
 
Jamani kuuliza si ujinga. Hivi kiongozi anatakiwa awe mwasikini? Mfano jamani huku nakuwa popo (huko US mnasema kubeba mabox) Nikijipatika kamtaji kangu nikaenda nyumbani na kumiliki mgodi si wezi kuwa kiongozi? Nadhani kama ni pesa ya halali ni sawa tuu kuliko hao makaburu na wacanada ambao wanachukua kila kitu ila kama mtaji ulipatikana kiusisadi nadhani hapo ndio kiongozi hafai. Jamani hayo ni mawazo yangu tuu.
 
Just the other day, we learnt that a minister in the current government actually owns a gemstone mine. This gives us the impression that we probably have a cabinet full of ministers who are inspired by money and personal wealth.

~Professor Mwesiga Baregu

The current Govt in power is there b'se of their money, unategemea nini? They must find the means of recovering the money they spent to put the Govt in power. Na njia mojawapo ni hiyo ya kugawana resources zenu.

Hata mimi nilishindwa kuamini nilipomuona muungwana akifuta machozi pale Chimwaga baada ya kutangazwa kuwa kada # 1 wa #1. Alikuwa ametimiza malengo yake.

So the cabinet must be inspired by money and wealth japo muungwana alikuwa akijibu swali kabla ya kuulizwa Serikali yangu haina ubia na mtu yeyote akasahau kumalizia isipokuwa mtandao wangu pekee

Nani asiyejua 80% of the cabinet ni wanamtandao.
 
Jamani kuuliza si ujinga. Hivi kiongozi anatakiwa awe mwasikini? Mfano jamani huku nakuwa popo (huko US mnasema kubeba mabox) Nikijipatika kamtaji kangu nikaenda nyumbani na kumiliki mgodi si wezi kuwa kiongozi? Nadhani kama ni pesa ya halali ni sawa tuu kuliko hao makaburu na wacanada ambao wanachukua kila kitu ila kama mtaji ulipatikana kiusisadi nadhani hapo ndio kiongozi hafai. Jamani hayo ni mawazo yangu tuu.

Hatujakataa katu Kiongozi kuwa na pesa tunachokataa yeye akiwa angali ni waziri ofisini anamiliki mali nyingi kiasi hicho, kuna maadili na miiko ya viongozi havimruhusu kuwa hivyo alivyo. Mfano ni huu kuwa kiongozi wakati huo huo ni mfanya biashara lazima mambo mengi ya kiofisi utayamuvuzisha katika miradi yako. Isitoshe hata kuwajibika kwako kiofisi itakuwa ni kwa kiwango kidogo sana hii imefanyiwa utafiti hatutoi vichwani mwetu. Huwezi kupanda farasi wawili ukafanikiwa kuwaelekeza unakotaka.
 
Sasa kama alimiliki mali nyingi kabla ya kuwa kiongozi hapo inakuwa je? maadili na miiko ya uongozi inasema maxmam kiongozi anaruhusiwa kumiliki kiasi gani?

Mtu anaweza akawa anaown biashara na kuajiri watu wa kufanya kazi au akawa anaown biashara kwa njia ya kununu share kwenye makampuni. Unajua Mungai anaown share nyingi sana TCC? Mbona walimu na wafanyakazi wengine wa serikali na wa makampuni binafsi wanafanya biashara japo ya nyumba za kukodisha au hata kuuza maandazi?

Mimi naona tuangalie kama utajiri umepatikana kihalali waache wamiliki nchi imeshatoka kwenye ujamaa ni nchi ya kibepari hii mkuu.

yeah kwa upande mwingine nakubaliana na wewe mawaziri ni waajiriwa na wanatakiwa kutumia muda wao wa kazi kuwatumikia waajiri wao na si kutumia muda wa ofisi kwa kazi zao.
 
Hizi Ndo Zama Za Chukua Chako Mapema,unajua Nchi Ikishajaa Ufisadi Alafu Hakuna Wa Kuwatia Discipline Mtu Anaona Kheri Nae Awe Na Kajiplot Na Ata Kajimgodi Ukiuliza Mbona Fulani Anao Na Hajachukuliwa Hatua Zozote.
We Need To Change And Do Away With The Personalization Of Public Properties
 
We waache waendelee kujichukulia tu bila kukumbuka kuwa public inanotice na kurekodi kila wanachofanya..... wakati wa pay back ndio itakuwa matata....... wananchi yanaanza kuwafika shingoni na kuna siku wataivamia hiyo miradi yote na kudemand vya kwao

kuna mchangiaji hapa JF alisema kuwa kuna siku watanzania wataingia ikulu kwa miguu... bado natafakari uzito na maana halisi ya hii statement ingawa pia naamini kuwa hiyo siku si mbali!
 
Mimi naona tuangalie kama utajiri umepatikana kihalali waache wamiliki nchi imeshatoka kwenye ujamaa ni nchi ya kibepari hii mkuu.
.

Hawa viongozi wote tunawajua walikuwa na hali za kawaida kabisa. Hawakuwa matajiri, hivyo utajiri waliokuwa nao sasa hivi umepatikana kwa njia za haramu ndiyo maana hata Mkapa anashindwa kujibu tuhuma chungu nzima za mambo aliyoyafanya akiwa Ikulu. Hivi ni tamko lipi lililosema Tanzania ni nchi ya kibepari? Itakuwa vizuri ukiliweka hapa ili tujue lilitamkwa lini na nani.
 
Success in business
and in life is a “connect the dots.”
Process. All you need to do is find
out the habits, disciplines and
strategies that others have used to
obtain their results and connect
the dots by duplicating their
actions. Once you follow the steps
they have taken, in the order they
have taken them in, you are bound
to get the same results.
 
Niliyasema haya niliporudi kutoka Bongo, kuwa viongozi wetu sasa hivi wanagawana ardhi kubwa zenye kusadikika kuwa zina madini.
Sisi wananchi walalahoi tunaambia ardhi ni mali ya serikali na hata imefikia wachimbaji wadogowadogo kufukuzwa katika makazi yao lakini wao wanaweza kuchukua hizi ardhi na kudai kuwa zao tena basi kuleta makampuni ya kuchunguza madini (mine exploration) kama vile hizi ardhi ni mali yao na kila kilichomo.. Inasemekana kwa uchache sana kama kuna madini basi viongozi hawa hudai mabillioni ya fedha toka makampuni ya nje.
True Kabisa Mkuu....
 
Hawa viongozi wote tunawajua walikuwa na hali za kawaida kabisa. Hawakuwa matajiri, hivyo utajiri waliokuwa nao sasa hivi umepatikana kwa njia za haramu ndiyo maana hata Mkapa anashindwa kujibu tuhuma chungu nzima za mambo aliyoyafanya akiwa Ikulu. Hivi ni tamko lipi lililosema Tanzania ni nchi ya kibepari? Itakuwa vizuri ukiliweka hapa ili tujue lilitamkwa lini na nani.
Kahama Geita watu wanaumasikini wa KUTUPWAA.....
 
Back
Top Bottom