Queen of Africa

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
MALIKIA NJINGA MBANDE, ALIKUWA MALIKIA SHUPAVU,MAHIRI, MWENYE DIPLOMASIA LAKINI MWENYE MBINU ZA HALI YA JUU ZA KIJESHI KUWAHI KUTOKEA AFRIKA.

Na.Comred Mbwana Allyamtu
Thursday - 17/10/2018

Malikia Njinga Mbande alikuwa malikia wa Dola ya Ndongo eneo la N'gola ambayo ndio Angola ya leo, malikia huyu utajwa kama ndie malikia pekee Afrika mwenye umahiri wa hali ya juu katika mapambano dhidi ya adui zake vitani. Pia hutajwa kama kiongozi wa Afrika aliyekuwa na diplomasia na mbinu za hali ya juu za kijeshi katika dola zote Afrika zilizowahi kutawaliwa na viongozi wa kike.

Malikia huyu amebakia na histoaria kubwa sana barani Afrika hususani ndani ya taifa la Angola ambalo ndio historia yake imebakia, taifa la Angola humtazama malikia huyo kama bibi wa taifa (the founding grand mother of nation) wa taifa hilo. Kwani jina lake limepewa baadhi ya mitaa nchini humo ikiwa ni pamoja na mtaa mkubwa uliopo jijini Luanda wa Kinaxixi ambapo sanamu lake lilijengwa kwa heshima yake.

Njee ya mitaa na vyuo kadhaa kupewa jina la malikia huyo pia tarehe ya kifo chake ni siku ya kitaifa nchini humo ili kuenzi juhudi zake za mapambano za kulijenga taifa hilo la Angola, kwani kupitia yeye amefanya Angola kuhifadhi historia nyingi za zamani na zenye mvuto mkubwa kupitia malikia huyo Njinga Mbande. Hakika malikia huyu ndie Angola na Angola ilikuwa Njinga Mbande.

Hata hivyo jina Angola linatokana na neno la lugha ya Kibantu "N’gola", ambalo lilikuwa jina la kiongozi wa ufalme wa Kwimbundo karne ya 16, ambapo Wareno walianza ukoloni katika eneo hili. Katika historia wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne ya kwanza BK kutoka kaskazini walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Kuanzia karne ya 14, falme mbalimbali zilienea sehemu za Angola, mfano wa Dola hizo ni ile ya Kongo, Dola la Lunda na Dola la Kasanje.

Kabila kubwa linalotajwa kutamalaki Angola ni Wambundu, kabila hili la Wambundu ni kabila la Angola. Wanaishi katika maeneo ya Luanda, mji mkuu wa Angola, Malanje, na Bengo. Wako pia maeneo ya Cuanza Kaskazini na Cuanza Kusini. Lugha yao ni Kimbundu, ambayo ni lugha ya Kibantu. Zamani Wambundu walikuwa wakaazi wa Ufalme wa Ndongo, uliokuwako kusini mwa Ufalme wa Kongo. Wafalme wa Ndongo waliitwa "ngolas", jina ambalo baadae lilikuja kuitwa kwa taifa la kisasa la Angola ya leo.

Baadhi ya ngolas viongozi wanaojulikana zaidi huko Angola ni Ngola KIluanji kia Ndambi, aliyetawala tangu mwaka 1562 hadi 1575, mwingine ni Njinga Ngola Kilombo kia Kaseda, aliyetawala tangu 1575 hadi 1592, mwingine ni Ngola Nzinga Mbandi aliyetawala mwaka 1592 mpaka 1617, kisha huyu tunayemtazama leo Ana de Sousa Nzinga Mbandi aliye tawala mwaka 1624.

Leo tutamuangazia malikia Nzinga Mbande ambae ni moja ya viongozi wa kike maarufu sana Afrika kutokana na umahiri wake wa kuingoza taifa la Ndongo (Angola ya sasa), malikia huyu hutajwa kama kiongozi shupavu na mwenye mbinu za mapambano katika vita.

Malkia Anna Nzinga alizaliwa 1583 tarehe aifahamiki vizuri na alifariki December 17, 1663, pia alijulikana kwa jina la Njinga Mbande au Ana De Sousa Nzinga Mbande alikuwa malkia wa karne ya 17 wa Ufalme wa Ndongo na Matamba Angola. Alipata madaraka, kama mwakilishi wa kitaifa baada ya kuonyesha umahiri wake katika kuonyesha mapungufu ya mbinu za utawala wa wa ukolononi na aliweza kushinda Wareno katika mamlaka ya Ambaca.

Alitawazwa kuwa malkia baada ya kaka yake kujiua. Nzinga alichukua madaraka badala ya kifo cha baba yake na kushikilia nafasi ya malikia kwa niaba ya mtoto wake. Leo anakumbukwa katika Angola kwa umahiri wake katika siasa na shughuli za kidiplomasia. Pamoja na mbinu zake za hali ya juu za kijeshi malikia Njinga hubakia kuwa malikia pekee afrika anayetajwa kuwa na nguvu. Leo katika jiji la Luanda Mtaa mkubwa wa Luanda umepewa jina lake kama kumbukumbu yake, pamoja na sanamu yake kubwa kuwekwa mtaa wa Kinaxixi kwenye eneo la pembe nne, hii ilitokana na shinikizo la rais Eduado dos Santos kuamuru lijengwe sanamu la kumbukizi ya malikia Njinga katika sherehe za kusherehekea miaka 27 ya uhuru ya nchi hiyo.

Sanamu lake iliyoko Kinaxixi ni kumbukumbu ya Maisha toka kuzaliwa kwa malikia huyo. Mtwa huyo Nzinga alizaliwa na ngola Kia Samba na Guenguela Cakombe inakadiriwa mwaka 1583. Alikuwa na uhusiano na Nzinga Mhemba ambae alikuwa mfalme wa Congo ambae alibatizwa jina na kujulikana kama Alfonso mnamo mwaka 1491 na Wareno. Nzinga alikuwa na dada wawili, Mukumbu, au Lady Barbara na Kifunji au Lady Grace. Baba yake Nzinga alikuwa dikteta, na mfalme wa Ndongo na Matamba ambayo ilitawala watu wa dola ya mbundu.

Kia Samba alitolewa madarakani mwaka 1610, na mtoto wake wa nje, Mbandi, alichukua madaraka na Nzinga alilazimishwa kuondoka katia nchi kwani alikuwa mpinzani wake katika ufalme. Kutokana na mila, alipewa jina kutokana na Njinga kwasababu alipozaliwa kondo la uzazi lilizunguka shingo yake (kwa lugha ya Kimbundu kujinga ni kuzunguka) kwahiyo Nzinga ni iliyozunguka. Inamaanisha mtu mwenye tukio hilo atakuwa mtu mashuhuri, mwenye maringo na asiyeogopa kuongea. Mwanamke mmoja mwenye busara alimwambia mama yake kuwa, Nzinga atakuja kuwa malkia. Kutokana na kumbukumbu
Nzinga alikuwa mtoto aliyependwa sana na baba yake, kiasi ambacho baba yake hakumwacha akiwa katika shughuli zake za kifalme na alishuhudia baba yake alivyofanya maamuzi, na pia alikwenda vitani na baba yake. Alikuwa na kaka mmoja Mbandi pamoja na madada wawili Kufunji na Mukambu. Aliishi kipindi cha biashara ya watumwa njia ya Atlantic na mipango ya Wareno kuchukua madaraka ya eneo lao ilikuwa inakwenda kwa kasi kubwa.

Ikumbukwe kuwa ureno walikuwa watu wa kwanza kifika Angola, hivyo walifanya juhudi kubwa kutanua biashara zao ndani ya Angola. Hivyo kwao wareno waliona eneo la Ndogo kuwa sehemu muhimu katika biashara zao za utumwa

Mnamo karne ya 16, nafasi ya Wareno katika biashara ya utumwa ilihatarishwa na Waingereza na Wafaransa. Matokeo yake Wareno walihamishia biashara yao ya watumwa Congo na Kusini Magharibi mwa Afrika. Kwa kuchanganya jina la kiongozi na eneo, Wareno waliita watu wa Mbundu "Waangola" neno ambalo mpaka leo hii linajulikana hivyo.

Nzinga kwanza alijulikana katika historia kama msindikizaji wa kaka yake, ngiolssa Ngola Mbandi, katika mkutano ma masuluhisho pamoja na Gavana wa Ureno Joao Correia de Sousa uliofanyika Luanda mwaka 1922. Ukorofi wa Wareno. Wareno waliweka soko la watumwa mjini Luanda mwaka 1557, na wakati huu familia ya kifalme ya Ndongo "ilipigana kufa na kupona kulinda himaya yake".

Baadae Wareno walilweka makazi katika ardhi ya Mbundu na kujenga ngome na kujiimarisha Luanda mnamo mwaka 1618, Wareno, kwa msaada wa rafiki zao wa Imbangala, walivamia mji mkuu wa Ndongo na kuwaua mashujaa wa ukoo. Wareno walitegemea kuchukua eneo la ufalme wa Kiafrika na kuchukua watumwa. Utaratibu wa kuchukua watumwa uliwekwa na ofisa wa Kireno aliyeitwa Bento Cardoso mnamo mwaka 1608, ambae "alidai watumwa kutoka Ndongo waende kwenye himaya ya Wareno".

Ubalozi wa Nzinga Mbandi alimuita Nzinga arudi kwenye ufalme mnamo mwaka 1617 ili akutane na Wareno akiwa na lengo la kulinda uhuru wa Ndongo. Nzinga alituma ujumbe na maombi ya kufikia muafaka wa amani, ulimfikia gavana wa Kireno mjini Luanda. Mkutano ulifanyika mwaka 1622, na Nzinga kwa kushangaza wageni "walishangazwa na kujiamini kwake". Gavana Joao Correia de Sousa, hakuwahi kubahatika kupata nafasi katika mkutano ule aliishia kukubali makubaliano ambayo yaliendea makubaliano ya amani na usawa kwa pande zote mbili Nukuu moja ya muhimu ambalo hakuna mwenye jibu nalo ni kama Ndongo ilisalimu amri kwa Wareno na kukubali kuwa chini ya Wareno.

Hadithi moja maarufu inasema kuwa katika mkutano ule gavana wa Ureno hakutoa kitii cha kukaa, Joao Correia de Sousa alitoa kwa Nzinga kukalia mkeka na kwa mila za Mbundu hii ni kwa mtu aliye chini yako. Nzinga alipoona vile hakukubali kujishusha, alimuamuru mfanyakazi wake mmoja akae chini na yeye akamkalia mgongoni wakati wa makubaliano hayo. Kitendo hiki kiliandikwa kwa ubunifu na paroko wa Kiitaliano aliyeandika kitabu mwaka 1687.

Nzinga alibadili dini na kuwa Mkatoliki mwaka 1622, alipobatizwa mjini Luanda. Inawezekana Nzinga alibatizwa ili aimarishe mkataba wa amani na Wareno, na alipewa jina la Dona Anna de Sousa kwa heshima ya mke wa gavana ambae ndiye aliyekuwa mama yake wa ubatizo. Kuna wakati alitumia jina lake katika mawasiliano ya barua (au Anna tu). Mwenyewe

alikubali kuwa "nilifanya hivyo kwa sababu ya msingi ni kuweka uhusiano mzuri na Wareno". Wareno hawakuwahi kuuheshimu mkataba wa amani. Pamoja na uhusiano aliokuwa nao naWareno, waliendelea kuingilia ufalme wake, kuchukua "watumwa na vito vya thamani".Aidha kuondoka Ambaca au kurudisha mateka waliowashikilia kama watumwa hawakuweza kushikilia kwanguvu Imbangala. Kaka yake Nzinga alijiua kufuatia diplomasia iliyoishia vibaya, alielewa hataweza kurudisha alivyopoteza katika vita. Kuna maneno kuwa Nzinga ndiye aliyemuekea kaka yake sumu, na maneno haya yalirudiwa tena na Wareno kuwa ni moja ya sababu zilifanya wasimheshimu kwakua hakuheshimu haki ya kaka yake.

Nzinga alianza kuongoza kwa niaba ya mtoto wake, Kaza ambae alikuwa anaishi na Imbangala. Nzinga alimtuma mtoto wake wa kiume kwa amri yake. Mtoto alirudi na inasemekana alimuua kwa hila zake. Baadae alichukua madaraka ya kutawala Ndongo. Katika mawasiliano yake mwaka 1624 kwa ustadi alijiita mwenyewe "Malkia wa Andongo" (rainha de Andongo), cheo alichokishikilia kutoka hapo. Nzinga alikuwa na adui, Hari a Ndongo, ambae alipinga utawala wa mwanamke. Hari ambae baadae alibatizwa kama Filipe I, aliapa kuwatumikia Wareno. Kwa msaada wa ufalme wa Kasanje na mashujaa wa Ndongo waliompinga Nzinga, alitolewa Luanda na alikimbilia Milemba a Cangola.

Nzinga alishindwa mashambulizi mwaka 1625 na majeshi yake kutolewa kwa upande wa mashariki. Wareno walimuweka dada yake Nzinga, Kifunji, kuwa kibaraka wao na alifanya kazi kama mpelelezi wa Nzinga dhidi ya Wareno kwa miaka mingi. Nzinga aliweza kukusanya nguvu na aliweka nguvu katika utawala wa Matamba mwaka 1629. Katika kipindi hicho Nzinga alichukua wakimbizi waliokimbia kuchukuliwa utumwani.

Mnamo mwaka 1630, Nzinga aliweza kuchukua madaraka ya Matamba wakati chifu wao mwanamke alipofariki au muhongo Matamba. Katika Ushrikiano na Wajerumani Mnamo 1641, Wadutch, wakishirikiana na ufalme wa Kongo, waliteka Luanda. Nzinga kwa haraka aliwatumia ujumbe na aliweza kufanikisha makubaliano ya ushirikiano nao dhidi ya Wareno ambao waliendelea kushikilia eneo la ndani ya nchi wakiweka makao yao makuu katika mji wa Masangano.

Alidhamiria kukomboa eneo lote lililotekwa kwa msaada wa Wadutch, alihamisha makao yake makuu kuelekea Kavanga, kaskazini mwa Ndongo ambako ilikuwa mji mkuu kabla. Baadae mnamo 1644 alishindwa na jeshi la Wareno katika mji wa Ngoleme lakini alishindwa kufuatilia. Baada ya hapo mwaka 1646 alishindwa na majeshi ya Wareno katika mji wa Kavanga na katika harakati hizo dada yake mwingine alitekwa pamoja na nyaraka nyingine za muhimu ambazo zilizihirisha uhusiano na Kongo.

Nyaraka hizo pia ziliweka wazi kuwa dada yake aliyekamatwa alikuwa na mawasiliano ya siri na Nzinga na kuwa pia ilionyesha jinsi alivyomueleza mipango ya Wareno kwake.Matokeo yake, dada aliyekamatwa alizamishwa katika mto Kwanza. Kuna maneno mengine yanasema kuwa dada yake alifanikiwa kutoroka na kukimbilia sehemu ambayo ni Namibia ya sasa. Luanda chini ya Wajerumani sasa ilimtuma Nzinga kwa shinikizo, na kwa msaada wao, Nzinga aling'oa jeshi la Wareno mwaka 1647 katika vita ya Kombi. Nzinga baadae aliwazuia Wareno kutawala Ambaca, Muxima na mji mkuu wao Musangano. Kukosekana kwa vifaa na mbinu za kijeshi kulipelekea kushindwa kuwaondoa Wareno. Wareno waliteka Luanda katika shambulizi liliongozwa na Brazil likiratibiwa na Salvador Correia de Sa. August 15th 1648, Nzinga aliomba mashambulizi kusitishwa na aliamriwa kukimbilia Matamba ambako aliendeleza mashambulizi na Wareno mpaka katika umri wa miaka 60, yeye mwenyewe akiongoza majeshi katika mapambano.

Siku za mwisho za maisha yake; Mwaka 1657, Nzinga akiwa ameezeheka pamoja na vita vya muda mrefu dhidi ya Wareno, Nzinga aliomba makubaliano mengine ya amani. Kanisa lilimkubali Nzinga 1656. Alibadili tena dini kuwa Mkatoliki mwaka 1657. Pamoja na Capuchins, alihimiza makanisa katika ufalme wake. Baada ya vita na Wareno kuisha, alijaribu kujenga tena eneo lake ambalo lilikuwa limeharibika sana kutokana na vita pia kilimo. Alihakikisha Njinga Mona's Imbangala hatamrithi kama mtawala wa falme mbili zilizoungana za Ngongo na Matamba, na alileta lugha ambayo ilikuwa na maneno ya Kireno ili kuhakikisha familia yake inabaki kuwa watawala.

Kukosa mtoto wa kiume wa kumrithi kulipelekea kuwapa haki ya utawala familia ya Ngola Kanini na mipango ilifanywa ili dada yake aolewe na Joao Guterres Ngola Kanini na amrithi yeye. Ndoa hii, hatahivyo haikuruhusiwa na paroko alisema Joao alikuwa na mke mjini Ambaca. Alirudia imani yake ya Kikristu kujiweka mbali na Imbangala, na alichukua paroko wa Kongo Calisto Zelotes dos Reis Magros kama mtu aliyeungama. Aliruhusu wamisionari wa Caupuchin, kwanza Antonio da Gaeta na Giovanni Antonio Cavazzi da Montecuccolo kuwasalia watu wake. Wote wawili waliandika maelezo marefu kuhusu maisha yake, ufalme na nguvu vitu alivyodhamiria.

Alipigana kwa nguvu zake zote kukomboa watumwa na aliruhusu wanawake wazae watoto pamoja na mbinu nyingi zilizotumika kumtoa madarakani, hasa Kasanje, ambae mzunguko wa Imbangala ulilowea kusini kwake, Nzinga alikufa akiwa na miaka themanini tarehe 17 December 1663 mjini Matamba. Matamba ilienda kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe bila yeye, lakini Francisco Guterres Nogla Kanini hatimae aliendeleza ukoo wa kifalme. Kifo chake kiliwezesha Wareno kuchukua madaraka ya Kusini Magharibi, kufuatia biashara kubwa ya watumwa iliyofanywa na Wareno.

Wareno wasingekuwa na nguvu ya kutawala nchi mpaka karne ya 20. Mnamo 1671, Ndongo ilikuja kuwa sehemu ya Angola ya Wareno. Leo tumemuangazia malikia huyu ili kuonesha juhudi za viongozi wa Afrika wa zama hizo namna walivyo kuwa katika ujenzi na ustawi wa mataifa yao katika dola tofauti katika historia ya Afrika.

Katika historia ya Afrika kumekuwepo watawala wa kike toka zama hizo ambao wote hutajwa kama viongozi shupavu, ukiacha Malikia Njinga mbande wa Angola kuna malika Cleopatra wa Misiri aliye sadikika kuwa mwanamke mzuri kuliko wote, nje ya hao pia historia humtaja malikia Nefetiti wa dola ya Misiri ya kale anaye tajwa kuwa mmoja ya watawala waliyo ijenga Misiri (Kemet) kuwa dola kuu.


Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
IMG_20190507_101353_751.jpeg
 
Back
Top Bottom