Jengo si la Manji tena, sehemu kubwa ni la PSPF- Shirika la serikali, na waliomo mle ndani ya jengo ni wafanyabiashara mbalimbali wazalendo wazuri tu watazania. Inasikitisha kushabikia kuungua moto kwa jengo. Ni muhimu kutofautisha umiliki kwa maana ya kuwa na haki na mali fulani na Mali yenyewe.
Mimi niko radhi tuibiwe kama tunavyoibiwa kila kukicha kwenye migodi na makampuni kama ya bia, mabenki nk, ilmradi fedha hio isitoke nje ya mipaka ya tanzania. Wewe iba lakini pesa ibaki Tz kwa maana ya kujenga majengo kama hayo ya Quality Plaza na mengine. Maana hata Manji akifa au akikimbia nchi bado tunakuwa nayo. Ndio maana nafikiri si sahihi hata kidogo kwa mlioshabikia mali kuungua! Ni mali yetu haiondesheki ile ni yetu. Atakapochukuwa nchi jemadari, atasawazisha mapato yote yatokanayo na mali (assets) kama hizi. Lakini kama watakuwa wamekimbiza huko Jersey sio rahisi!
Hivi mnajua ni Bongo tu unaweza ukaingia kwenye Bureau de Change, ukatoa Dola hata 50,000 ukauza na wala usiulizwe tena wewe ni Mtz, na ukienda na vijisenti vyko ni Bongo tu unaweza kununua any amount of dola bila kuulizwa chochote, na bila kupewakaratasi lolote! Ndio hivyo! Ndiyo maana nchi inaliwa. Tujipe pole kwa kuunguliwa mali yetu pale Nyerere Road. Tutumaini jeshi letu la uokozi wa moto limenusuru mali na maisha!