Qatar, Fly540 zakubaliana kushirikiana


kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
5,144
Likes
268
Points
180
kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
5,144 268 180
Dar es Salaam. Kampuni ya Ndege ya Fly540 imesaini makubaliano na Shirika la Ndege la Qatar Airways, yenye lengo la kuwezesha abiria wa Qatar Airways kuendelea na safari za ndani na kanda kwa kutumia ndege za Fly540.
Chini ya makubaliano hayo, abiria wa Qatar Airways baada ya kufika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Kenya, wataendelea na safari zao mbalimbali kwa kutumia ndege za Fly540.
Shirika hilo la Ndege la Qatar huruka mara mbili kwa siku kwenye safari ya Nairobi-Doha, wasafiri wanaweza kuunga safari nyingine katika miji mikubwa barani Ulaya, Mashariki ya Kati na Asia Pacific.
Qatar Airways ilisema uamuzi wake wa kuchagua Fly540 kuwa kama mbia, unadhihirisha dhamira ya shirika hilo lenye makazi yake Doha kufanya uwekezaji eneo la Afrika Mashariki.
Msemaji wa Shirika la Fly540 la Kenya, alisema makubaliano hayo yanadhirisha jinsi shirika hilo linavyoaminika na kuhudumia mashirika makubwa kama la Qatar Airways.
“Tunayo furaha kufikia makubaliano haya na Shirika la Ndege la Qatar, ambayo ni makubaliano yetu ya kwanza ya pekee,” alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Fly540 Kenya, Don Smith. Safari hizo zinahusisha Zanzibar, Juba na vivutio vya utalii.

CHANZO: MWANANCHI
 
morphine

morphine

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Messages
3,089
Likes
357
Points
180
morphine

morphine

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2012
3,089 357 180
Wapi airtz mikono juuu juuu juuuu
 

Forum statistics

Threads 1,273,052
Members 490,245
Posts 30,469,012