Qaddar na harakati za kuitoa CCM ikulu

Qaddar na harakati za kuitoa CCM ikulu

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
Mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2010 ustadhi wangu madrasa aliniita nyumbani kwake na kuniambia maneno yafuatayo, naomba kumnukuu.

" Suleiman CHADEMA imefanya jitihada kadiri ilivyojaliwa katika kuhakikisha inashinda uchaguzi huu lakini matokeo yake wameshindwa na siku zote jitihada haiondoi qaddari"

Mimi huwa na tabia ya udadisi na kuhoji mambo hususani yale ninayo yatilia shaka katika ukweli au uhalali wake. Katika kuyatafakari maneno ya Ustadhi wangu na kwa jinsi nilivyo yaelewa maneno yale pamoja na ufafanuzi wake, kwa ustadhi wangu, mja hata awe na mbawa kama malaika Jibrili katu hataweza kuibadilisha qaddari yake." Qaddari" na kama ijulikanavyo kwa umaarufu kuwa ni "kudura" ni mambo yote aliyokadiriwa mja na M/mungu kuyafanya au kumfika katika kipindi chake chote cha maisha yake ya chini ya jua, yaani leo, na maisha yake yote ya kesho baada ya leo.

Kwa ustadhi wangu CCM itaendelea kuwa madarakani kama ndio qaddari yake kuwa madarakani au itatolewa na CHADEMA madarakani kama ndio qaddari yake kutolewa madarakani na CHADEMA, kinyume na hivi ni kupigana na ukuta ili hali twajua vema matokeo yake ni kuumiza mikono bila faida.

Ukichunguza na kuyatafakari maandiko ya M/mungu katika qur-an na biblia yanayo zungumzia qaddari unaweza ukaamini au kuelewa ndivyo sivyo, waweza amini kuwa katika ushindani kuna "mshindi" na "mshindwa" na wote hao "mshindi" na "mshindwa" walikuwa hawana hiyari katika kuelekea kwenye "ushindi" au "kushindwa" ingawa wenyewe walijiona wako huru katika kuchagua "kushinda" na "kushindwa" kwa kupitia maandalizi yao kabla ya kuingia kwenye ushindani. Hebu tuperuzi maandiko ya misahafu yetu kuhusiana na hiyo "qaddar".

"Musa na Haruni walifanya ajabu hizo zote mbele ya Farao; Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake"
Kutoka 11:10

Hapa mtu anaweza kujenga hoja kuwa Farao alikuwa anafanya mambo yote maovu dhidi ya wana waisraeli kwa kushinikizwa na mungu mwenyewe kwa vile tu, ni M/mungu ndiye aliyemfanya Farao kuwa na moyo mgumu badala ya moyo mwororo. Mbaya zaidi mtu anaweza kusema kuwa ushindi wa Mussa uliandikwa na kutabiriwa siku nyingi na kushindwa kwa Farao pia kuliandikwa na kutabiriwa siku nyingi pia, na yule aliyetabiri ndiye aliyeshiriki katika kufanikisha ushindi wa Mussa na ndiye aliyefanikisha kushindwa kwa Farao. Mtu mwenye imani hii, jitihada alizozitumia Mussa katika kuwakomboa wana waisraeli kwake ni mchezo wa shere uliochezwa na M/Mungu mwenyewe dhidi ya viumbe vyake. REJEA Mwanzo 15:13-14

"Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne. Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi."
Mwanzo 15:13-14

Maneno hayo M/mungu alimwambia Ibrahim miaka mingi tena wakati huo hata Ibrahimu hana dalili yoyote ya kupata mtoto, lakini aliambiwa uzao wake utaenda Misri na utakombolewa. Kwahiyo Mussa, Haruni, Farao, Wamisri na wana wa Israeli walikuwa wanafanya yale ili kutimiza unabii na si vinginevyo.

Pia mtu anaweza kujenga hoja kwa kutumia qur-an kuwa mungu huumpa ushindi amtakaye na kumnyima pia mtakaye. Qur-an 2:247 tunaoneshwa jinsi Sauli alivyofanywa na Mungu kuwa Mfalme wa kwanza wa taifa teule la Israeli.

"Na Nabii wao akawaambia: Mwenyezi Mungu amekuteulieni Taluti (Sauli) kuwa
ni mfalme. Wakasema: vipi atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tuna haki
zaidi kupata ufalme kuliko yeye, naye hakupewa wasaa wa mali? Akasema: Mwenyezi Mungu amemteua yeye juu yenu na amemzidishia ukunjufu wa ilimu na kiwiliwili. Na Mwenyezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mjuzi."
Qur-an 2:247

Fikra na imani ya kuwa jitihada haiondoi kudura ni mtaji wa shetani katika kujiongezea wafuasi na ushindi dhidi ya nuru ya MUNGU. Kwakuwa CCM ni moja wa mashetani wabaya katika nchi yetu, hivyo basi hii "imani" au "fikra"[jitihada haiondoi kudura] lazima iwe mtaji wake wa kuirudisha ikulu katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Imani hii ni moja ya sababu[zipo nyingi hizo sababu] iliyopelekea asilimia kuwa ya watu walio jiandikisha kupiga kura uchaguzi uliopita wasijitokeze kupiga kura, kwanini waende kupiga kura ili hali wanajua kuwa kura zao haziamui nani wa kushinda na nani wa kushindwa, bali mwenye kuamua ni mungu kwa kupitia qaddar.

Uchaguzi wa mwaka 2010 tulishindwa na CCM ilishinda, je, tubweteke na tuachane na jitahada kwa kudhani qaddar ndio kila kitu katika mchakato wa kupata rais wetu? Hivi na sisi kama chama tunaamini juu ya "jitihada haiondoi kudura?". Kwa jitihada zifanyazwo na viongozi wetu katika kukijenga na kukiimarisha chama ni kiashiria tosha kuwa imani hii kwao haijathibiti, hili ni jambo la faraja kwangu na kwa kila mtakia jema nchi hii. Huku tukiipuuza imani hii nafikiri ni vema kuelekea uchaguzi ujao CHADEMA kama chama ikazipitia na kuziboresha mbinu ilizozitumia hata ikawa mshindi wa pili katika uchaguzi uliopita. Kwa kunzia ni lazima wenye imanii watambue kuwa JITIHADA zao ndio kila kitu na si QADDARI.

Pamoja na kwamba katika ulimwengu wa imani za kimungu "qaddar" ina nguvu na ndio kila kitu katika maisha ya mja, lakini kiukweli hiyo "qaddar" haina nguvu kuizidi "dua" au "maombi". Pamoja na kwamba Yesu alijua kuwa kifo cha msalabani hakiwezi kumuepuka[kwa maana kulikuwa na utabiri juu ya hilo] lakini maandiko yanasema kuwa Yesu aliomba dua kwa Mungu ili kama kungekuwa na uwezekano kifo kile kimuepuke.

Pasina kuzingatia matokeo ya maombi yale ya Yesu, maombi yale ni kishiria tosha kuwa "qaddar" mbabe wake ni MAOMBI. Maombi ya kujinyenyekeza mbele za Mungu yana nguvu kuliko qaddar. CCM iwe imeandikiwa kutufanyia madudu na kuitawala nchi au la, vyovyote iwavyo, kama wapenda na wataka mabadiliko tufanye harakati pasina kusaahu kufanya maombi mazito kwa mungu na miungu kwa kuzingatia imani na dini zetu.

Nilishawahi kusema, leo naomba kurudia tu kile nilichokisema. Watanzania tulioahidiwa maisha bora na CCM na sasa tunalalama kwa maisha kuwa magumu, huduma mbovu za afya, maji, na elimu, na hivi majuzi tunalalamika kwa kukosa mikopo au watoto wetu kukosa mikopo ya elimu ya juu, kiukweli hatuna uhalali wa kisiasa wa kufanya hivyo ikiwa na kwa mfano ilani ya CHADEMA ilisema elimu itakuwa bure ya CCM ilisema ELIMU itaendelea kuwa si bure, lakini tukachagua ilani inayosema kupata elimu shuruti uwe na kitu. Je, tuko na uhalali wa kulalamika kwa kukosa mikopo?

Mfalme juha aghalabu hupatikana katika kaumu ya wajinga, ikiwa sisi kama umma ndio tuliomchagua Kikwete kuwa rais wetu bila kulazimishwa iweje sasa tumlaumu ikiwa kulikuwa na machaguo bora kuliko Kikwete? Iweje tulipanda upepo jana leo hii tughairi kuvuna tufani? Pamoja na hayo halijatufika bado, au huenda tungali tunaridhishwa na uongozi wa Kikwete au tu wajinga na waoga, kinyume chake kwa kimbunga kama kile kilicho muingiza Rais Kikwete madarakani 2005 ndicho ambacho kingemtoa 2010 au kabla hata ya 2015, hivi yale Tunisia hayakuwa na mazingatio kwetu?

Wizi wa kura, tume mbovu ya uchaguzi, sheria mbovu za uchaguzi, na matumizi ya idara za kiusalama katika uchaguzi ni visingizio tu vya wanasiasa walionyimwa ridhaa ya kuongoza serikali kwa niaba ya umma. CCM inaweza kuiba maelfu ya kura lakini si mamia elfu au mamilioni ya kura, hivyo kama umma ukijitokeza kwa wingi katika kupiga kura na kuichagua CHADEMA mwaka 2015 sito tarajia kusikia visingizio vya wizi wa kura, kinyume chake visingizio vitaendelea pamoja na kwamba katiba mpya itakuwa imetumika katika uchaguzi huo. Katika hili uchaguzi wa JIMBO la Ubungo ambao ulimpatia ushindi Mnyika ni kiashiria tosha CCM humudu kuiba kwenye ushindi mwembamba na si kwenye ushindi mnono.

Niliondoka kwa ustadhi wangu siku ile huku nikimuachia neno lifuatalo ambalo ningependa kuwachia pia watanzania wenzangu hususani wale wapenda na wataka mabadiliko.

"Jitihada haindoi kudura lakini kudura si kitu mbele ya maombi"

Njano5.

0784845394
 
Ni imani hiyo hiyo inayohimiza usali uombe ili Mwenyezi Mungu akupe kwa kiasi ya haki ya maombi yako. Pia kumbuka usiombe tu bila matendo. Haya matendo ndiyo mzani anaotumia Mwenyezi Mungu kukupa neema au kukunyima. Kama CHADEMA wanasema na wanatenda kwa haki mbele ya Mungu hakika Mwenyezi Mungu atawatunuku kwa ajili ya haki ya watu wake.

INAWEZEKANA TIMIZA WAJIBU WAKO.
 
Ni imani hiyo hiyo inayohimiza usali uombe ili Mwenyezi Mungu akupe kwa kiasi ya haki ya maombi yako. Pia kumbuka usiombe tu bila matendo. Haya matendo ndiyo mzani anaotumia Mwenyezi Mungu kukupa neema au kukunyima. Kama CHADEMA wanasema na wanatenda kwa haki mbele ya Mungu hakika Mwenyezi Mungu atawatunuku kwa ajili ya haki ya watu wake.

INAWEZEKANA TIMIZA WAJIBU WAKO.
Hivi chama kinaongozwa na wazinifu hivi unafikiri Mungu anaweza kukubali maombi yao kirahisi?
 
hapa kwani hakatwi mtu kama airtel ndio useme habari ya pumba mkuu??? au una mkono wa sweta???
Wewe utakuwa na jinsia mbili tu. na ndo maana unashabikia chadema huku unatumia Avatar ya rangi za ccm
 
Hivi chama kinaongozwa na wazinifu hivi unafikiri Mungu anaweza kukubali maombi yao kirahisi?

Kweli mwenzetu kichwa chako ni kifuu cha nazi. Musa alikuwa muuaji Mungu alimutumia. Winston Churchil alikuwa bongo lala kama wewe lakini ndiye alikuwa jemedari wakati wa vita. JK mzinifu namba moja mama yake Rizwan alikufa kwa ngoma. Babu Seya na wanae wanasota jela kwa sababu walipitia vitu vya JK; akashusha kisasi.

Wewe baba yako na mama yako wasingezini usingezaliwa.

Chama chenu kina akina Nchemba na akina Sofia Simba wenye mapepo ya ngono. Tafakari chukua hatua huu uzi huungumzii uzinifu unazungumazi KUDRA YA MWENYEZI MUNGU "QADDAR"
 
Wewe utakuwa na jinsia mbili tu. na ndo maana unashabikia chadema huku unatumia Avatar ya rangi za ccm

Hebu acha kupumuliwa nyuma wewe... eti rangi.... lusinde again!!!!
 
Imani za Kimungu na Miungu zikianza zaidi kushamiri katika kipindi cha kati (middle ages). Historia inasema ancient Philosophers walikua na uwezo mkuu sana wakufikiri na kugundua mambo mengi sana amabayo hadi leo hii yanatumika. Rejea Wanafalsafa mashuhuri Socrates &Plato kwa uchache. Leo hii somo lolote kwenye iwe uhandisi au ya kijamii lazima kwny foundation wasomwe mawazo yao.
Ilipofika kipindi cha kati watu wakaacha kufikiri, wakaacha kutafuta suluhu ya changamoto zao za maisha. Na ndipo imani za Mungu na Miungu zikajengeka kwa watu na dini zikajitokeza.
Fikra hizo ndo tumerithishwa kizazi hiki cha Leo, makala yako nzima inaongelea KUDRA! Sijui kisayansi kama kudra inaelezekaje.

Unataka tuache kwenda kutoa elimu kwa watu jinsi ccm inavyozidi kuwatia umasikini tusubiri KUDRA??
Tuache kulaani wizi wa kura,Tume mbovu ya uchaguzi n.k tusubiri KUDRA?

Pengine Naota! Nitarudi ..
 
Wewe utakuwa na jinsia mbili tu. na ndo maana unashabikia chadema huku unatumia Avatar ya rangi za ccm

Na wewe uko ccm afu unatumia jina la kata gani... kweli kuchamba kwingi....
 
We dogo angalia njaa zako zisijekutia motoni kwa kuzipinga aya za Mwenyezi Mungu kuhalalisha njaa zako. Rudi tena kwa ustadh wako akakupe maana y 'QADAR' NA 'QUDURA'. Hayo ni maneno mawili tofauti. Qadar hubadiliko kwa kumuomba Mungu ila Qudura haibadiliki hata kwa maombi. Mfano kifo ni Qudura hata umuombe Mungu haitobadilika. Utajiri ni Qadar ukimuomba huenda mwenyezi Mungu anawezakupa au akakunyima. Ndio maana wapo maskini na matajiri. Wacha kuchanganya akili kutafsiri maneno ya Mungu. Mwisho ni kuacha na maneno ya imamu Abubakar ibn Abi daudi Mungu amrehemu 'HAKIKA KUAMINI QADAR NA MATAKWA YA MUNGU ZIMEPOTEA KTK HILI AKILI ZA WATU NA ZIKATELEZA NYAYO KWA WALE WOTE WALIOACHA DALILI ZA QUR&HADITH, KWANI WALITEGEMEA KTK AKILI ZAO NA FIKRA ZAO'
 
Kweli mwenzetu kichwa chako ni kifuu cha nazi. Musa alikuwa muuaji Mungu alimutumia. Winston Churchil alikuwa bongo lala kama wewe lakini ndiye alikuwa jemedari wakati wa vita. JK mzinifu namba moja mama yake Rizwan alikufa kwa ngoma. Babu Seya na wanae wanasota jela kwa sababu walipitia vitu vya JK; akashusha kisasi.

Wewe baba yako na mama yako wasingezini usingezaliwa.

Chama chenu kina akina Nchemba na akina Sofia Simba wenye mapepo ya ngono. Tafakari chukua hatua huu uzi huungumzii uzinifu unazungumazi KUDRA YA MWENYEZI MUNGU "QADDAR"
Mkuu Mimibaba, umeandika kwa jazba kubwa na kutaja majina ya watu pasipo na sababu wala ushahidi wa uliyoandika. Najua umeandika hayo kutokana na chuki uliyonayo dhidi ya watu uliowaandika. Rejea kwenye hoja ili uone kama upo sahihi kwa uliyoandika au umepotoka. Pia nakushangaa kukumbatia maovu eti kwa kigezo kuwa watu fulani ambao walikuwa na mambo machafu walipata kuwa maarufu. Uchafu wa mtu hauwezi kuwa mbadala wa mazuri yake. Maovu yataendelea kuwa maovu hadi anaingia karibuni
 
Mkuu Mimibaba, umeandika kwa jazba kubwa na kutaja majina ya watu pasipo na sababu wala ushahidi wa uliyoandika. Najua umeandika hayo kutokana na chuki uliyonayo dhidi ya watu uliowaandika. Rejea kwenye hoja ili uone kama upo sahihi kwa uliyoandika au umepotoka. Pia nakushangaa kukumbatia maovu eti kwa kigezo kuwa watu fulani ambao walikuwa na mambo machafu walipata kuwa maarufu. Uchafu wa mtu hauwezi kuwa mbadala wa mazuri yake. Maovu yataendelea kuwa maovu hadi anaingia karibuni

mkuu bavicha ndiyo walivyo wao ni kutukana na kuzusha mambo yasiyo na ukweli.
 
Back
Top Bottom