Pwani: Watu 9 mbaroni kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Diwani Mteule Fatuma Ngozi(CCM)

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
WATU tisa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya Fatuma Ngozi, aliyekuwa diwani mteule wa Kata ya Kikongo, Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani…(endelea).

Mbali na mauaji ya Fatuma yaliyotokana na kuchomewa nyumba yake akiwa ndani, watu wengine watatu walifariki dunia kwenye tukio hilo lililotokea tarehe 9 Novemba 2020.

Kwa mujibu wa Wankyo Nyigesa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, tukio hilo lilitokea saa saba usiku katika Kijiji cha Chekeleni, Kata ya Kikongo , Tarafa ya Mlandizi kwenye Halmashauri ya Kibaha Vijijini.

Kwamba, mbali na watu wawili waliokuwa kwenye nyumba hiyo wakati wa tukio kufarika, we ngine watatu walifariki wakati wakipatiwa matibabu na kufanya jumla ya watu waliofariki kuwa sita huku mmoja aliendelea na matibabu.

Kamanda Nyigesa amesema, baada ya uchunguzi wa jeshi lake, limekamata watu tisa ambapo wanane ni wanaume na mmoja ni wanawake, akifafanua zaidi amesema ‘watu hao wamekamatwa kutokana na ushahidi uliokuswanywa.”

Amesema, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limewahoji watuhumiwa wote, na sasa taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.

“Uchunguzi wa tukio bado unaendelea, jeshi la polisi litaendelea kuhifadhi majin a, kazi na wadhifa wa watuhumiwa hawa. Kadhi tutakavyokuwa tunaendelea kupeleleza, tutakamata wengine kwa mujibu wa upelelezi wetu,” amesema.

1605607183384.png

 
hayatuhusu haya mambo
Yanatuhusu sana. Kwa Tanzania kuna uwezekano mkubwa hao waliokamatwa wala hawahusiki kwa namna yoyote. Ni juu yetu sote kufuatilia na kujua ukweli na kama tukiona kuna uonevu tupaze sauti kwa umoja wetu. Tukijifanya kusema hayatuhusu hatujui kesho litaangukia kwa nani.
 
Back
Top Bottom