Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limekibaini kiwanda cha kutengeneza silaha na vifaa vya kutengeneza silaha za kienyeji Chalinze mkoani Pwani kinachodaiwa kumilikiwa na Shabani Athumani (61).
Akizungumza leo Jumanne Februari 2, 2021 kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema wamekibaini kiwanda hicho jana saa 7 usiku baada ya kupata taarifa kwa wasiri wao na askari walifanya doria ya kushtukiza na kufanikiwa kumkamata mhusika ambaye ni mkazi wa Chalinze.
Amesema Athumani anatuhumiwa kumiliki kiwanda cha kutengeza silaha na vifaa vya kutengenezea silaha jambo ambalo ni kosa.
Amesema vifaa vilivyokamatwa ni mtambo wa kufulia vyuma, mitambo mitatu ya silaha aina ya gobore ambavyo ipo tayari bado kuwekwa mtutu na kitako, pakiti moja ya unga wa kiberiti na chupa tano ndogo zenye baruti.
Vingine ni fataki 48, risasi 42 za gobore, mitambo ya kutobolea miti inavyofungwa kwenye gobore na kopo moja lenye unga wa tindikali unaotumika kuunganisha vyuma vinavyofungwa kwenye gobore.
Amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote na kuwaomba wananchi kutoa taarifa wakati wowote na kusisitiza kuwa taarifa zao zitakua siri kati yao na polisi.