Putin ni Mwanadamu au Shetani Katika Umbile la Mwanadamu?

Putin ni Mwanadamu au Shetani Katika Umbile la Mwanadamu?

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,948
A maternity ward and a children's ward have been destroyed in a Russian air strike on a hospital in the southern city of Mariupol, officials there say.
"The destruction is colossal," the city council says. There are reports of many dead and injured, with children buried under rubble. BBC.

Mwanadamu wa kawaida, hata asiye mcha Mungu, kati ya vitu ambavyo ni vigumu kwake kufanya ni kuua. Ngumu zaidi ni kumwua mtu asiye na hatia. Lakini ngumu zaidi na zaidi, ni kuwaua watoto, tena watoto wadogo.

Kwa sababu za namna yoyote ile ambayo Putin anaweza kuitoa, hakuna hata moja inayoweza kumpa uhalali wa kuwaua watoto wadogo, na wananchi wa Ukraine. Tangu mwanzo wa vita, raia wa kawaida, watoto na wagonjwa waliopo mahospitalini, wamekuwa wakiuawa na makombora ya Putin. Hii si mara ya kwanza kwa makombora ya Putin kupiga hospitali na kuwaua wagonjwa.

Tunakuomba Mungu wetu uwajalie pumziko jema la milele watoto waliouawa leo na siku zilizopita na makombora ya Russia huko Ukraine. Na pia hata watu wazima wasio na hatia yoyote ile. Lakini kwa mkono wako wenye uweza wote, tunakuomba, ukawahukumu na kuwaadhibu Russia sawa na matendo yao kwa mauaji wayafanyayo dhidi ya wanadamu wenzao.
 
sio ngumu kwa putin. R.I,P kwa kina mama na watoto
 
A maternity ward and a children's ward have been destroyed in a Russian air strike on a hospital in the southern city of Mariupol, officials there say.
"The destruction is colossal," the city council says. There are reports of many dead and injured, with children buried under rubble. BBC...
Haya mambo tuwaachie wenyewe mkuu wangu Bams.

Kwani yameanza leo?
Tulalamike na haya yetu hapa kwetu, ambapo pia yanatokea kila siku na husikii wakisema jambo juu yake. Wakisema wanasema kinafiki.
 
Mpenzi wangu aliniuliza usiku wakati tumelala kitandani. Hivi Rais Putin ni shetani kiasi gani kwa kuivamia Ukraine???

Sikutaka kuzozana kwasababu nilikua nimechoka. Nikaamka na kwenda jikoni, nikachukua Kisu kikubwa sana halafu ni kikali kweli kweli na kwenda nacho chumbani. Nikamkuta amejilaza kitandani. Nilipofika nikakiweka katikati yetu kisha nikalala zangu. Akaniuliza hicho kisu kibwa halafu kikali si kitanichoma nikiwa usingizini??? Sitaweza kulala, bora ukitoe kwasababu nakiogopa na ni hatari kuwa jirani yetu!!!

Nikamwambia jambo kama hili unalolikataa na kuliogopa, ndio Rais Putin analolikataa na kuliogopa pia. Ila yeye unamuona ni shetani. Anakataa kuwekewa hatari karibu yake kwasababu hatolala, na hatari hio isije kumdhuru wakati akiwa usingizini kama wewe.

USA na NATO wanataka kumwekea Vinu Vya Nuclear Na Silaha Za Nuclear katika nchi ya Ukraine ambae ni Jirani Yake!!! Alilipinga kwa maneno jambo hilo ila hawakusikia!!! Na sasa ndio anachokipinga kwa vitendo!!!
 
Putin hata mimi simuelewi ila sometimes nahisi labda kuna jambo alifanyiwa ambalo mimi nawe hatulijui, ila hao BBC nao sio wakuwaamini sana na taarifa zao kwenye issue kama hii, wako upande wa NATO zaidi.
 
A maternity ward and a children's ward have been destroyed in a Russian air strike on a hospital in the southern city of Mariupol, officials there say.
"The destruction is colossal," the city council says. There are reports of many dead and injured, with children buried under rubble. BBC....
Hata huko Syria (Allepo) alifanya hayo hayo...dunia ilikemea tu ila haikuweka vikwazo vikubwa kwa Urusi sababu Vita vilikuwa mbali na bara la Ulaya.
 
A maternity ward and a children's ward have been destroyed in a Russian air strike on a hospital in the southern city of Mariupol, officials there say.
"The destruction is colossal," the city council says. There are reports of many dead and injured, with children buried under rubble. BBC...
Nime umia sana! Mungu atoe adhabu inayo tosheleza madhambi ya Rais na vigogo wenzake huko Russia
 
Mpenzi wangu aliniuliza usiku wakati tumelala kitandani. Hivi Rais Putin si shetani kwa kuivamia Ukraine???

Sikutaka kuzozana kwasababu nilikua nimechoka, nikaamka na kwenda jikoni, nikachukua Kisu kikubwa sana halafu ni kikali kweli kweli na kwenda nacho chumbani. Nikamkuta amejilaza kitandani...
None Sense! Kwa anacho kifanya Sasa Putin
 
A maternity ward and a children's ward have been destroyed in a Russian air strike on a hospital in the southern city of Mariupol, officials there say.
"The destruction is colossal," the city council says. There are reports of many dead and injured, with children buried under rubble. BBC...
Source yako kutoka wapi ?!!!

Ikiwa CNN ,FOX NEWS ,MSNBC ,BBC unategemea nini ?!!!
 
Back
Top Bottom