Putin Maji Shingoni, Alia na Mataifa ya Magharibi

Putin Maji Shingoni, Alia na Mataifa ya Magharibi

Hivi ndivyo unavyoweza kusema, zile tambo zake za kutunisha misuli alizokuwa nazo wakati anaanza kuivamia Ukraine zinazidi kufifia. Putin kwa sasa amekuwa ni mtu wa kulaumu na kulia kwenye hotuba zake tofauti na ilivyozoeleka hapo hawali, hizi ni dalili za kwamba haoni ushindi wa karibuni kwa vita aliyoianzisha.

Ni wazi kwamba kwa sasa inawezekana maji yameanza kufika shingoni mwa Bwana Putin.
___________________________________________


Putin alaumu mataifa ya magharibi kwa uvamizi wa Ukraine

Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatatu ameyalaumu mataifa ya magharibi kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.

Putin amesema kwamba Russia ilikuwa ikijibu vitisho kutoka kwa mataifa hayo karibu na mpaka wao. Akihutubia wanajeshi wakati wa maadhimisho ya kushindwa na wanazi wa Ujerumani kwenye vita vya pili vya dunia, Putin alizungumzia mada ya Russia kwa dhamana ya ulinzi, ambapo Russia ilitoa miezi kadhaa kabla ya uvamizi wake kwa Ukraine hapo Februari 24, akirejea kusema kwamba kamwe hakuwa na mipango ya kumvamia jirani yake.

Kabla ya uvamizi huo, maafisa wa Marekani pamoja na NATO walikutana mara kadhaa na wale wa Russia, lakini baadhi ya madai ya Russia yalikataliwa kama vile kuahidi kuwa Ukraine kamwe haitojiunga na NATO. Putin ameongeza kusema kwamba mataifa wanachama wa NATO hawakutaka kutusikiliza na kwamba walikuwa na mipango taofauti kabisa.

Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak kwa upande wake amesema kwamba Russia haikuwa na sababu yoyote ya msingi yakulivamia taifa lake, akiongeza kwamba mataifa wanachama wa NATO hayakuwa na mpango wa kuishambulia Russia kamwe.

View attachment 2221651
Endeleeni kujidanganya!!...wenye akili ndo wanaelewa ukweli halisi
 
Vita isikie kwa jirani tu, nashangaa humu watu wavoshadadia
Pale gongolamboto Kuna mwaka yalilipuka mabomu ya JWTZ ...baadhi ya watanzania kwa hofu kubwa walikimbia Hadi Chalinze...sauti ya mlipuko wa mabomu hayo ni wa kawaida Sana, kuliko hayo ya hypersonic ya Russia...
Pale gongolamboto watu wengi walikimbia na kuacha watoto wao ambao baadaye walikusanywa pale uwanja wa taifa shamba la bibi na wazazi wakaja kuwatambua...
 
Sasa unataka kusema sio mbabe?
Kama sio mbabe kwanini PANYA ROAD na KUBWA LAO wamekua nao wapenzi watizamaji na watoa press release kila siku kinacho endelea Ukrain?
Kiufupi naona wamejitekenya wenyewe, zaidi wanaendelea kuongeza nguvu, 30 hawatoshi.
Aliyesema si mbabe nan, kila mbabe ana mbabe wake hiki ndicho kinachomkuta mbabe Putin
 
C ana mshkaji wake yule naniliu anae penda mazali kama hayo, au hataki kumshilikisha
 
Huyu mwamba ana matatizo nimeingia Vlad kijijini ndani nikaomba Kwenda msalani nimekuta wale Pro Putin wametengeneza floor ya choo chao Kwa rangi ya bendera ya Ulaya hahaha

Kifupi wamechanganyikiwa, nikamuuliza Kwanini umefanya Hivi akasema is about secrecy don’t ask


View attachment 2221694

Britanicca
Unaondoka saa ngapi Jamiiforums?
 
Teh teh teh Pro Russia mshapoteana
Kwisha habari yao sasa hivi wamebakiza matusi. Sasa waswahili wanasema dawa ya moto ni moto, anapojibu tusi, nikumuongezea hili wakasimulie Kremlin kwa Bwana wao Putin
 
Yaani kwasiku mtu mmoja anaanzisha thead zaidi ya tano kuhusu Putin
 
Back
Top Bottom