Putin has a big problem in Syria that no one is talking about

Putin has a big problem in Syria that no one is talking about

Nimekupata Nonda. Hapo ndipo napozidi kujifunza mengi sana ambayo katika hali ya kawaida, mtu hawezi kuelewa. Hebu tuangalie huu mchezo unakoelekea.

Link If these extraordinarily powerful images of a dead Syrian child washed up on a beach don't change Europe's attitude to refugees, what will? | Europe | News | The Independent

Link 2. Photo of drowned Syrian child prompts calls for action - Business Insider

You will like this one. Link 3.

Link 3. Farsnews
 
He will, lakini inabidi aende kwa uangalifu maana akiharibu, itamuathiri sana nyumbani. Kama asilimia ya wananchi wanaomuunga mkono sasa hivi ni wachache, hali itakuwaje watu wake wakianza kufa? Hata kama Bunge litaendelea kumuunga mkono, atakuwa na mtihani mgumu.
Uzuri wa Putin, maneno yake ni machache sana, kwa hiyo hatuwezi kujua war plan kutoka katika war room yake ina nini. Tutarajie maajabu mengi.
Kama evil wishes za Westerners kwa Putin zingekuwa mishare Putin angekuwa kama nyama machinjioni. Lakini they are just wishful thinking. Tuliambiwa vikwazo baada ya matukio ya Ukaraine vitammaliza na wananchi watamchukia. Ni wazi bado ana kiburi cha kuingia Syria. Westerners wanapenda sana kumu-underrate Putin na Warussi. They have to wake up. Russia ia still a power.
 
Putin yupo tayari kuchafua hadi kieleweke, maana anajua akipoteza hapa atapoteza kote hadi nyumbani.
Tayari kuna taarifa kapeleka kisiri huko Syria vifaa vya kila aina kana kwamba anaenda kupigana na nchi kubwa. Anajua ISIS wameifikisha dunia kwenye koo, hadi hata waarabu wenyewe wamewachoka, hivyo kwa kuwapa kichapo cha mbwa itamfanya awe kipenzi cha wengi duniani na kurejesha hadhi kwa Mrusi.

Hivyo majihadi wote waikimbie Syria na Iraq maana mvua ya jehanamu ipo itanhyesha hivi karibuni.
 
Nimekupata Nonda. Hapo ndipo napozidi kujifunza mengi sana ambayo katika hali ya kawaida, mtu hawezi kuelewa. Hebu tuangalie huu mchezo unakoelekea.

Ukifika hapo unakaribia kwenye ukweli mkuu ,ukweli ambao wengi itakuwa ngumu kuukubali sasa hivi hata ukiwaambia nini ila wataukubali kwa matokeo yake, ambayo hawatakuwa na uwezo wa kuyapinga kamwe na wote watakuwa wamechelewa tayari, hawatakuwa na la kufanya ila kushiriki madhara ya matokeo yake, ukweli kuwa DUNIA INAONGOZWA NA UJINGA!
 
Wapi watu wa vitabu hapa, watudadavulie kuhusu THE BOOK OF REVELATION, inasemekana kuwa imeelezwa humo na kwenye EZEKIEL kuwa mrusi ana operation muhimu in the middle east ili kuuleta mwisho, so we should reckon it the beginning of the end masna jamaa kaenda kukamilisha maandiko pale, hatoki tena mpaka yaibuke makubwa yalioandikwa !
 
Putin yupo tayari kuchafua hadi kieleweke, maana anajua akipoteza hapa atapoteza kote hadi nyumbani.
Tayari kuna taarifa kapeleka kisiri huko Syria vifaa vya kila aina kana kwamba anaenda kupigana na nchi kubwa. Anajua ISIS wameifikisha dunia kwenye koo, hadi hata waarabu wenyewe wamewachoka, hivyo kwa kuwapa kichapo cha mbwa itamfanya awe kipenzi cha wengi duniani na kurejesha hadhi kwa Mrusi.

Hivyo majihadi wote waikimbie Syria na Iraq maana mvua ya jehanamu ipo itanhyesha hivi karibuni.

Dah! Kwa hiyo sasa hivi tutegemee makubwa kutokana na kile atakachokifanya Mrusi Syria? Ila mauaji ya raia pia yanaweza kuwa makubwa sana.
 
Ukifika hapo unakaribia kwenye ukweli mkuu ,ukweli ambao wengi itakuwa ngumu kuukubali sasa hivi hata ukiwaambia nini ila wataukubali kwa matokeo yake, ambayo hawatakuwa na uwezo wa kuyapinga kamwe na wote watakuwa wamechelewa tayari, hawatakuwa na la kufanya ila kushiriki madhara ya matokeo yake, ukweli kuwa DUNIA INAONGOZWA NA UJINGA!

Wala hujakosea kabisa na wengi wanatumika kufanya ujinga bila wao kujua.
 
Nashangaa sana haya mambo. Hivi kuna mtu anaeweza kunieleza kwanini US ili-Veto kukataa ISIS kuwekewa vikwazo juzi hapa? Sijaelewa kabisa hiyo kitu.
Ni sir kubwa lakini kwa sasa imeanza kujulikana. Russia inachofanya pale Syria ni kuwatwanga ISIS na kuwatwanga waasi wengine wote wa Asad. Kwasababu wote hao walitengenezwa kwa mpango maalum.
 
NENDA PUTIN achana na US
....putin hana dini na atafuta upuuzi wowote unajiita dola ya kiislam huku ikiuwa wanadamu

NAIPENDA sana USA ila sipendi namna ISIS wanavyowika mbele ya US na sasa wamepata mshenzi mwenzao anayeabudu mashetani kama wao so...it gonna be fine......watakufa ISIS with their GOD

Hao waliojipachika jina la Uislam ili waupake matope Uislam ni US na Wayahudi - kumbuka hilo.

Hapo Putin anatandika US, Wayahudi na vibaraka wao.
 
Huko syria itafika wakati kukosekana kabisa watu wa kuishi huko! Na je hawa magaidi/ISIS hawawezi kufanya mauwaji huko urus ya kujitolea mhanga?
 
Huko syria itafika wakati kukosekana kabisa watu wa kuishi huko! Na je hawa magaidi/ISIS hawawezi kufanya mauwaji huko urus ya kujitolea mhanga?

Ukifatilia hotuba ya juzi ya Put in kule UN kasema Russia inajua yote hayo na ipo tayari kwa yote. Ndio maana bunge lao liliamua kuwafata ISIS huko walipo na si kuwangoja mpaka waje nyumbani.
 
Ukifatilia hotuba ya juzi ya Put in kule UN kasema Russia inajua yote hayo na ipo tayari kwa yote. Ndio maana bunge lao liliamua kuwafata ISIS huko walipo na si kuwangoja mpaka waje nyumbani.

Well said, Putin pamoja na washauri wake walifanya homework ya kutosha kabla ya kuanzisha operation hii maluum huko Syria - URUSI inataka kudhilishia Dunia kwamba sio TAIFA la kuchezea likihumua kufanya kweli halifanyi hajizi hata kidogo. Uzuri wa OPERATION hii tokomeza ni kwamba Warusi wana taarifa kamili kuhusu sehemu walipo jichimbia, makambi yao ya mafunzo, viwanda vya kutengeneza IEDs, bunkers zinazo hifadhi ammunitions na silaha nyingine nk, barabara/njia zinazo tumika kusafirisha silaha kutoka nchi jirani, si hilo tu Syria vile vile hiko kwenye darubini ya majeshi ya URUSI wanatumia Drones na Satellites 24X7,Radio scanners kusikiliza mawasiliano yote yawe ya ISIS au NATO - they know how to decipher scrambled Signals na kuzifanyia kazi fasta.

Narudia ku-insist kwamba Urusi itahakikisha inawapa fundisho la mwaka kwa kufutilia mbali vikundi hivyo hatarishi vinavyo fadhiliwa na Merikani na Wayahudi, lengo kuu la Merikani ni kuvuruga amani Mashariki ya kati kwa maslahi yao binafsi, halafu MSM za magharibi bila aibu vinasingizia Waislaam, Rais wa Syria na IRAN!!

We fikiria Merikani pamoja na Washirika wenzake wametumia karibu mwaka mzima wakijifanya wanashambulia vikundi vya ISIS, narudia mwaka mzima!! Cha ajabu kikundi cha ISIS kiliedelea kuimarika na kushamiri licha ya Merikani kudai kwamba ndege zao zinashambulia kundi la ISIS, hatukuwahi kuona picha wala video yoyote kutoka Merikani au Ulaya ikionyesha wapiganaji/makambi ya ISIS yakipigwa mabomu na ndege za Merikani/NATO - walikuwa wanafanya usanii tu, wanabeba dummy bombs kwenye ndege zao na kuyadodosha jangwani ambapo hakuna wapiganaji wa ISIS au makambi yao, kesho yake Merikani inatumia Helicopter kuwadododeshea silaha kundi la ISIS ili waendeleze harakati zao ya kushambulia majeshi ya Syria na raia ambao hawana hatia. Cha kujiuliza hapa ni: inakuwaje jeshi la anga la URUSI linatumia siku tatu kufanya kazi ambayo Merikani/NATO walishindwa kufanikisha kwa takribani mwaka mzima wakashidwa kuwadhibiti ISIS!! NATO kazi yao ni blah blah na majigambo tu ni wahusika wakuu katika uvurugaji wa amani Africa kaskazini, Mashariki ya kati na Ulaya ya Mashariki. Sijui kwa nini makundi ya Wakimbizi kutoka Africa kaskazini, Mashariki ya kati na Afghanistani awapandi meli kwa wingi kwenda Merikani Taifa ambalo linahusika kwa uvurugaji amani ndani ya Mataifa yao?
 
Namtafuta NN, superpower anapewa masaa mawili aondoke anga ya Syria wala habishi anaondoka kimya kimya. Juzi kati nilikutana na kundi la contractors pale Krossestrasse uso wao ulionyesha kuchanganyikiwa. Nikahisi ni kazi ya Mrusi!
 
Huko syria itafika wakati kukosekana kabisa watu wa kuishi huko! Na je hawa magaidi/ISIS hawawezi kufanya mauwaji huko urus ya kujitolea mhanga?

Mrusi anapiga vita vya anga tu kwa hiyo kujitoa muhanga kwa Isis itakuwa shughuli pevu kwani hata kuzifikia base za Mrusi within Syria haitakuwa rahisi. Isis anaweza kuanza kujitoa muhanga pale Mrusi atakapoanza kusambaza majeshi ya ardhini au pale Muiran na/au Hezbollah watakapoingiza majeshi ya ardhini. Hapo ndipo vita itakapokolea ikiwa imechanganya kila aina ya vurugu ikiwa ni pamoja na wapiganaji wa kujitoa muhanga.
Kwa upande wa Isis kuishambulia Urusi nyumbani, hilo linaweza kuwa katika agenda ya Isis kwa sasa maana ni rahisi kwao kushirikiana na makundi fulani Chechnya au Ingushetia ambayo yanaweza kutoa msaada ila napo sidhani kama itakuwa kazi rahisi maana Mrusi ana uzoefu na mashambulizi nyumbani kwake na kama amesema amejiandaa kwa yote, mashambulizi ya nyumbani yatakuwa yamepewa kipaumbele kikubwa katika kuzuiwa.
 
Namtafuta NN, superpower anapewa masaa mawili aondoke anga ya Syria wala habishi anaondoka kimya kimya. Juzi kati nilikutana na kundi la contractors pale Krossestrasse uso wao ulionyesha kuchanganyikiwa. Nikahisi ni kazi ya Mrusi!

Hebu fafanua Mkuu, uliokutana nao ni Military contractors au nini? Mrusi ameamua kuwaondolea uchovu hao jamaa na pia kama wanavyobashiri wengine, ili awin credit na friendships za huko Middle east.
 
Ukifatilia hotuba ya juzi ya Put in kule UN kasema Russia inajua yote hayo na ipo tayari kwa yote. Ndio maana bunge lao liliamua kuwafata ISIS huko walipo na si kuwangoja mpaka waje nyumbani.

Kabla ya hii vita aliyoianzisha, Mrusi alituma majasusi wengi tu Syria na baadhi waliwahi kukamatwa na kuuwawa na Isis, kwa hiyo kuna uwezekano anao wengi tu hata sasa ambao wanamupdate juu ya taarifa muhimu.
 
Hebu fafanua Mkuu, uliokutana nao ni Military contractors au nini? Mrusi ameamua kuwaondolea uchovu hao jamaa na pia kama wanavyobashiri wengine, ili awin credit na friendships za huko Middle east.

Ndiyo Mkuu hao hao!
 
Back
Top Bottom