Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

sio dhihaka tu bali ni kuwatusi watu yaani mbwembwe nyiiiingi ila hamna kitu....sasa kila kitu basic wanapandisha kodi hadi simu,magari sasa kwa staili hii mtu mshahara wa 1M ukijafika kwako si imebaki laki 5 tu kutokana haya makato na mfumuko wa bei uko busy unapanda maana naona hadi mafuta yanaongezewa kodi
 
Punguzo la 1% (kutoka 15% hadi 14%) kwenye kodi ya mishahara (PAYE) ni dhihaka kwa wafanyakazi wa Tanzania kwani gharama za maisha ziko juu sana kufuatia mfumuko mkubwa wa bei. Ifike wakati sasa serikali iwaonee huruma wafanyakazi kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi badala ya kufawafanyia mzaha kama huu. Wafanyabiashara wakubwa na mafisadi kibao wanasamehewa kodi lakini mfanyakazi masikini anazidi kukandamizwa tu kila kukicha. Hii haikubaliki hata kidogo.

Kwa jinsi serikali ilipokuwa inatamba kwa mbwembwe kwamba itapunguza kodi ya mishahra, sikutegemea kwamba mwisho wa siku wangekuja kupunguza kiasi kidogo kama hiki cha kodi. Ni aibu kwa kweli. Wafanayakazi mnanapaswa kutambua kwamba seriklali ya CCM haina nia njema katika kuwapunguzia ukali wa maisha, hivyo basi fanyeni uamuzi sahihi hapo mwaka 2015 ili kurejesha nidhamu kwa serikali hii isiyokuwa na mwelekeo.

Kana kwamba hili halitoshi, bado wafanyakazi hao hao watakamuliwa Tsh 2500 kama kodi ya kumiliki simu kwa kila mwezi! Wananchi mmnatakiwa kuacha uzezeta—amkeni tukawafundishe adabu hawa mafisadi mwaka 2015. Saa ya ukombozi ni sasa. Bila kufanya hivyo, tutaendelea kukandamizwa hadi mwisho wa dahari. Tafakari, chukua hatua!

duu mbona hii 2500 sijaielewaelewa kidogo..
 
Sio kila kitu kinahitaji siasa siasa na kubeza.
ni halali kulipa kodi but kwa kiwango cha 14% Is too much kwa wafanyakazi maskini wa kitanzania.Zimebakia nchi 2 tuu duniani (UK na TZ) zinazoongoza kwa kukamua wafanyakazi wake.
 
Kuindoa CCM kwa sanduku la kura sahau!mwaka 2010,jwtz ndio waliobeba masanduku
 
Ni dhihaka hasa. Nafikiri hatuna haja ya kusubiri kubamizwa marungu kama mabwege wa Mtwara iliyokuwa inaitwa NGOME YA CCM ndio tuamke. Asiyepiga kura 2015 ni ndugu yake na shetani
Suala sio kupiga kura tu suala ni nani unayempigia kura maana unaweza ukawa unabadilisha watu wenye tabia zilezile au ukabadilisha chama chenye watu wa aina ileile.
 
Mkuu..serikali zote duniani zinatoza PAYE.. Hata kama misamaha ya kodi kwenye madini itafutwa bado Paye itaendelea kutozwa kwa viwango vya kulalamikiwa

Watu wengine hua mnaudhi kweli kwenye comments zenu, kwani nani aliyesema kwamba wafanyakazi hawataki kukatwa kodi? Uzi unasema ni dhihaka kupunguza only 1%, hivi ambacho wewe huajelewa ni nini hapo? Kweli walimu wanakazi ngumu, unajua kutumia computer lakini uzi rahisi kama huu bado huelewi! Watu wengine hua wapo kwa bahati mbaya tu, sorry to say that.
 
Kwenye uchaguzi 2015 lazima mgombea urais aseme wazi kwamba atapunguza paye kutoka 14% hadi 3% mbona migodi wanachajiwa 3% tena kwenye net profit iweje sie tunalambwa kwenye gross? Hilo neno paye lifute iwe tax tu.
 
Mkuu..serikali zote duniani zinatoza PAYE.. Hata kama misamaha ya kodi kwenye madini itafutwa bado Paye itaendelea kutozwa kwa viwango vya kulalamikiwa

... Ni wizi mtupu, kwa kuwakandamizi wafanyakazi.
Makato ya PAYE yanaishia matumboni mwa wajanja chache na familia zao.



.
 
kwa nini wanifanyie dhihaka?
1%? Kweli?
Watoze PAYE sawa sikatai, lakini mbona sioni dhati yoyote ya kupunguza mfumuko wa bei ili niyamudu maishi? Unadhani mfumuko wa bei ungedhibiwa ningelalamika kuwa PAYE ipunguzwe?

Hayo ni maswali ya msingi sana mkuu! Unapunguza PAYE kwa 1% halafu unapandishia kodi ya mafuta ambayo mwisho wa siku itapandisha kila kitu kwa mfano bei za vyakula, nauli n.k. na kusababisha mfumuko wa bei kwenda juu. Katika hali kama hiyo bado kuna watu wanaitwa wabunge ambao wanasimama na kusema bajeti hii inamjali mtu wa chini!!! Kweli? Ni mtu wa chini yupi huyu ambaye wanamzungumzia wao? Hii ni dhihaka ya hali ya juu sana na tatizo hapa ni watawala kujifanya kutojua kwamba watanzania walio wengi ni masikini wa kutupwa.
 
Jamani CCM haitegemei kura za wafanyakazi Jk.alishasema kura zenyewe ni laki tatu tu,kwa hiyo hata wakikatwa kodi kubwa magamba haiwahusu,ni saa ya wafanya kazi kufanya kampeni kwenye familia zao kuanzia babu mpaka mjukuu wanaikataa CCM maana na wao ni wahanga.
 
Kulikuwa na matarajio makubwa kuwa PAYE ingepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu ilikuwa ni ahadi ya Mh Rais mwenyewe aliyoitoa kule Mbeya. Kwa punguzo hili sidhani hata kama kulikuwa na sababu ya kuwatangazia wafanyakazi kuwa PAYE itapungua.
Angalia jedwali hapa chini (mapato ni kwa Mwaka).
Viwango vya Sasa
Viwango vya sasa Jumla ya Mapato
Kiwango cha Kodi
Mapato ya jumla yasiyozidi Shilingi 2,040,000/=
Asilimia sifuri (0%)
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 2,040,000 lakini hayazidi shilingi 4,320,000/=
14% ya kiasi kinachozidi Shilingi 2,040,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 4,320,000/= lakini hayazidi shilingi 6,480,000/=
Shilingi 319,200/= + 20% ya kiasi kinachozidi Shilingi 4,320,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 6,480,000/= lakini hayazidi shilingi 8,640,000/=
Shilingi 751,200/= + 25% ya kiasi kinachozidi Shilingi 6,480,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 8,640,000/=
Shilingi 1,291,200/= + 30% ya kiasi kinachozidi Shilingi 8,640,000/=
Viwango vinavyopendekezwa
Jumla ya Mapato Kiwango cha Kodi
Mapato ya jumla yasiyozidi Shilingi 2,040,000/=
Asilimia sifuri (0%)
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 2,040,000 lakini hayazidi shilingi 4,320,000/=
13% ya kiasi kinachozidi Shilingi 2,040,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 4,320,000/= lakini hayazidi shilingi 6,480,000/=
Shilingi 296,400/= + 20% ya kiasi kinachozidi Shilingi 4,320,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 6,480,000/= lakini hayazidi shilingi 8,640,000/=
Shilingi 728,400/= + 25% ya kiasi kinachozidi Shilingi 6,480,000/=
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 8,640,000/=
Shilingi 1,268,400/= + 30% ya kiasi kinachozidi Shilingi 8,640,000/=
 
Ni dhihaka hasa.

Nafikiri hatuna haja ya kusubiri kubamizwa marungu kama mabwege wa Mtwara iliyokuwa inaitwa NGOME YA CCM ndio tuamke. Asiyepiga kura 2015 ni ndugu yake na shetani

Wewe umegusa penyewe haswaaaa....Kupiga kura...Hata sisiem na wanmazi wake wanalijuwa jili kuwa kinachowaokoa ni kwamba wasioipenda ambao ndio wengi sana hawapigi kura...in short ni wavivu kupiga kura na sio vinginevyo.
 
Hiyo 1% ni kubwa sana upande wa serikali. Hapo serikali inapoteza mabilioni ambayo inabidi ikayatafute kwenye vyanzo vingine. Ni kweli kuwa hii PAYE sisiw afanyakazi hatuipendi lakini ukiangalia kwa picha kubwa bora wangeongeza hata Kidogo hii PAYE na kupandisha juu kiwango cha msamaha ili serikali ipate uwezo zaidi wa kutuhudumia vizuri .
 
Chapeni kazi acheni kulia lia, kuna vyama vingi sana vya upinzani viliingia madarakan katika bara la Afrika ukianzia, kenya, burundi, zambia, nigeria, algeria,ghana,n.k lakin maisha ni yale yale , hiko chama chenu kina kitu gan so special kias kwamba kikiingia kitatofautiana na vyama vingine vilivowah kushika dola. Punguzen kulalamika pigen mzigo mbona wengi tu tumeyatoa maisha ndan ya tawala hii hii, mzee ndesa, mbowe na kina mtei mbona wamefanikiwa chin ya sera hizi hizi za CCM!
Kwa sababu wewe unawalamba viatu watwana na wezi wa rasilimali zetu. mwisho wenu waja
 
Yani nilikuwa nasubiria kwa hamu hiyo ahadi ya rais ya kupunguza kodo kwenye mishahara nilichosikia sikuamini1% ni dhihaka!
Nyie mnaotetea mtu unabasic ya laki7na20 alafu mkononi unaondoka na laki4 kodi laki na 20 kazi tunayo wafanyakazi!
 
Mfanyakazi ni mnyonge, kila sehemu ana lipa kodi lol1
Nalipa kodi kuanzia kwenye mshahara hadi kwenye pedi lol!
 
Ivi katika hili nani mtetezi wetu? mwanzo nilifikiria wabunge watalipigia kelele baadae nimegundua kuwa hawatofanya hivo kwani wao huwa hawakatwi kodi.
Mbona wafanyakazi tunaonewa sana? ivi tuna dhambi gani kwa serikali?
mie nikilipwa mshahara tayari ninakuwa nimesha katwa kodi
nikienda kwa mangi/kwa mpemba kununua chochote kile nakatwa kodi
nikienda kariakoo nikanunua chochote nalipia kodi
nikinunua mafuta sheri nalipia kodi
nikipanda daladala nalipia na kodi katika nauli nayotoa
nikinunua vocha nalipia na kodi,
nikiongea kwenye simu nalipia kodi
nikimhamishia salio mtu kwa m-pesa/tigo/ezypesa/airtel money nalipishwa kodi
...............................kodi
................................kodi

inaniuma sana kwani kila kona minezunguukwa na kodi kiasi kwamba mshahara wote nalipa kodi. serikali sikivu hii ni haki kutufanyia sisi wafanyakazi?
 
Chapeni kazi acheni kulia lia, kuna vyama vingi sana vya upinzani viliingia madarakan katika bara la Afrika ukianzia, kenya, burundi, zambia, nigeria, algeria,ghana,n.k lakin maisha ni yale yale , hiko chama chenu kina kitu gan so special kias kwamba kikiingia kitatofautiana na vyama vingine vilivowah kushika dola. Punguzen kulalamika pigen mzigo mbona wengi tu tumeyatoa maisha ndan ya tawala hii hii, mzee ndesa, mbowe na kina mtei mbona wamefanikiwa chin ya sera hizi hizi za CCM!





......yaani wewe ndo'mbuchuuuuchu-mbuchuchu!ukoma wa akili ni m'baya sana!namna hii unawavunja moyo waliokupa elimu......darasani na nje.......coz effort zao wangeelekeza kwingine wangekua na maisha bora zaidi,nadhani wanasikitika sana kwa sasa coz uhai wako haujawasaidia kitu.go to sleep!
 
Back
Top Bottom