Punguzo bei za barakoa

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Nimefatilia nchi nyingi ambazo wamechukua hatua kubwa za kukabiliana na Covid19 nimejikuta naanza kuwaza fursa hii ya Barakoa.

Nitajikita apa kwetu kuna mafundi wa cherehani ambao ukipita mitaani unakuta wakipiga mihayo lakini kuna uhitaji mkubwa wa Barakoa bei inapanda kila uchwao.

Nashauri serikali andaeni wataalamu wasambazwe mikoani wakatoe elimu kwa mafundi awa ili watengeneze Barakoa nyingi watakavyoweza ili kila Mtanzania aweze kupewa Barakoa nne kila mmoja ambazo zinatosha kwa siku na kusafishwa kwaajili ya siku nyingine.Hii itasaidia upatikanaji wa Barakoa bila ghalama za usafilishaji.

Serikali itoe fedha zinazotolewa waajili ya Covid19 zikanunulie Barakoa.
Atakayeonekana hana barakoa barabarani achukuliwe hatua.

Lakini pia kumbuka hatujui ugonjwa huu utadumu muda gani,nashauri Serkali ipileke hoja ya dharula Bungeni ili bajeti ipitishwe ya kupambana na Covid19

Jijini la Dar Es Salaam lifungwe ili kuzuia maambukizi kuenea nchi nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka ushirikiano gani wakati uzi wako upo hewani? Alafu ushauri wako wizara iliuchukua.

Sent using Jamii Forums mobile app

..umerudishwa baada ya kum-tag bwana mkubwa mwenye JF.

..lakini leo nini nyuzi mbili nyingine ambazo zimefutwa na sioni sababu yoyote ya kuzifuta.

NB.

..naomba unielekeze zilipo taarifa za serikali kuamua JKT na Magereza watengeneze barakoa.
 
..nilianzisha uzi nikipendekeza viwanda vya JKT na Magereza vitengeneze barakoa.
Mkuu tumeshauri sana hapa hadi kuambiwa hatuna Uzalendo. Leo kila ulilosema lipo wazi

Nilimwambia Pascal Mayalla incubation period ikiisha iva kinachofuatia ni community spread katika exponential rate. Ndicho kinatokea. Kesho utasikia wagonjwa zaidi wapya kuliko leo.

Pascal nilisema nitaomba radhi kama haitatokea kwa kupotosha. Uungwana unakuhitaji,nawe sema neno!

Tumepoteza fursa nyingi za kuzuia ugonjwa.Kenya , Uganda na Rwanda walichukua hatua kali mapema, Tanzania ikiwacheka kama anavyoonekana Gwajima n.k.

Tukaruhusu mzaha kama ule wa Makonda ''watoke kuchapa kazi'' . Leo kuna anayetoka?
Wajuvi walifunga maduka, wanajua nini kinaendelea duniani. Hawasubiri kusimuliwa au kushurutishwa.

Tulishauri marufuku ya mikusanyiko hakuna aliyesikiliza. Tukashauri kinga za airborne disease na si kuosha mikono tu na hapa ndipo wangefikiria Barakoa,tulionekana wendawazimu tu.

Hayo yakiendelea akina MsemajiUkweli walivaa njuga kusifia hata visivyosfikia.

Wakasema Corona inahitaji ''African solution''. Leo hawaonekani tena wamejificha Lumumba baada ya kuupotosha umma. Watakaa kimya vilio vikitanda nchini. Wamepata kula yao kwa gharama za Watanzania.

Hili halina msamaha, corona ilianza China, ikaenda Ulaya na Marekani kabla ya kuja Afrika.
Tulikuwa na kila sababu za kuzuia, viongozi wetu hawakuona hatari au hawakusiklizia walipoambiwa

Na huu ni mwanzo tu, ikifika May 2020 , waliokuwa hawatuelewi watatuelewa.
 
Kipindi hiki cha gonjwa hili la mlipuko kumeniongezea msamiati.

Sikuwahi kufahamu, Mask kwa Kiswahili tunaita BARAKOA
 
1587006366088.png
 
Back
Top Bottom