Rais Magufuli, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapaswa kuwa na kozi za Afya

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,238
4,464
Mheshimiwa Rais, hongera na majukumu mazito ya kulijenga taifa. Umeonesha njia na nia kwa kipindi kifupi cha uongozi wako, pamoja na mapungufu madogo ya kibinadamu ambayo hayawezi kufukia mazuri uliyofanya.

Mheshimiwa Rais, mimi ni miongoni mwa watumishi wa afya nchini, ingawa sitibu, bado ninahudumia wananchi nikiwa upande wa pili katika sekta binafsi, nikisimamia afya ya mama na mtoto. Nimesoma Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili (MUHAS, nitaita Muhimbili), enzi zile ukiwa Waziri na mara kadhaa ulikuja kunywa chai pamoja nasi kantini ya Muhimbili chuo. Hivyo mimi ni mhitimu wa chuo Kikuu Muhimbili. Tunashukuru kwa offer ulizokuwa unatupa kipindi kile tukiwa na ukata wa pesa. Wacha waseme, ukarimu wako haukuanza jana.

Mheshimiwa Rais, nikiwa kama mdau wa elimu Tanzania, ambaye pia niliathirika kwa Chuo Kikuu cha Muhimbili kuamua kujiengua toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, huku sisi tuliopata udahili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam enzi hizo tukilazimishwa kupokea vyeti vya Muhimbili (MUHAS) pamoja na kwamba tulienda kuomba haki Mahakamani lakini hatukupata ni kwa muda mrefu sana nimekuwa natamani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kianzishe digrii za Afya (hapa nitajikita zaidi kwenye Medicine). Nina kiu hiyo, kwa sababu hakukuwapo na mantiki ya Muhimbili kujitoa ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa wakati huo hata ingekuwa sasa. Duniani tuna vyuo vikuu vingi ambavyo ni vikubwa, na bado havijameguka, mfano ni Massachusetts Institute of Technology (MIT), Indian Institutes of Technology (IIT). Nakumbuka mwaka 2013, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilikuwa ni Chuo cha Nne Bora Afrika, na hakika kingekuwa na kozi za Afya kingefanya vizuri na kuliletea sifa taifa letu.

Mheshimiwa Rais, kugawanyika kwa vyuo vikuu Tanzania hususani Muhimbili toka UDSM kulikoongozwa na Prof. Mutabaji (sasa mwenyekiti wa TCU) ulikuwa ni ubinafsi uliotukuka, uroho mkubwa wa madaraka na hatua za kutaka kufisadi pesa zinazotoka serikalini.

Mheshimiwa Rais, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo pekee cha Tanzania kinachotambulika kama comprehensive university, lakini pamoja na hilo wengi wamekuwa wakikishangaa kwanini hakitoa digrii za afya. Muhimbili haiwezi kuwa comprehensive university kwa sababu imejikita na kozi ya afya pekee, SUA nao wana kilimo na biashara tu, UDOM wana miaka mingi mbele mpaka watakavyoweza kuwa na sifa za kuwa comprehensive university. Kuna faida kubwa za chuo kikuu kuwa ni comprehensive university ambazo si hoja za leo, lakini mojawapo kuu ni kuwa na sifa ya kupata ushirika wa tafiti kubwa, kuvutia miradi mikubwa mikubwa na kupokea misaada na ushirika toka mataifa na taasisi kubwa duniani.

Mheshimwa Rais, Tiba ni kati ya taaluma ambazo mara kadhaa huwa nyuma na maendeleo ya Sayansi hasa pale tafiti zenye kuleta matokeo chanya zinapokuwa hazifanyiki. Kwa Tanzania ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pekee ambacho kina uwezo mkubwa wa kuunganisha mkazo wa sasa wa Afya na Sayansi na technolojia kwa sababu kuna idara zilizojijenga kama za mechanical engineering, electrical engineering, computer science, computer engineering, molecular biology, na nyingine nyingi ambazo zinaweza zikafanya kazi pamoja na taaluma za afya ili kuboresha afya ya Mtanzania na dunia kwa ujumla. Katika ulimwengu wa sasa huwezi tenganisha medicine na sayansi yeyote ile hasa engineering. Medicine na Engineering inabidi wakae sehemu moja katika kuhakikisha ulimwengu wa tiba unaendelea. Iwe katika ugunduzi wa vifaa tiba, utengenezaji na ukarabati wa vifaa tiba n.k. Mfano mkubwa wa hasara ya kutounganisha afya na engineering ni kuwepo kwa uharibifu wa vifaa tiba vingi ambavyo hununuliwa kwa pesa nyingi na serikali pamoja na wafadhili mbalimbali, na bado vikakosa mafundi wa maintenance and repair, ambao tungetegemea wawe walisomea Biomedical Engineering. Ni aibu kwamba mafundi wengi tunaowatumia sasa wanatoka Nairobi na Mombasa, na tena si mafundi wajuvi.

Mheshimiwa Rais, si siri kwamba pamoja na jitihada za UDSM kuanzisha kozi za afya, kumekuwa na vita kali ya chini kwa chini ingawa inaonekana kati ya Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili dhidi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taarifa zinasema, vita hii imekuwa ikitumika kufanya lobbying kadhaa kuonesha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hakina uwezo na hakistahili kuanzisha kozi za Afya. Bahati mbaya lobbying hizi zinafika hadi ofisi yako tukufu. Taarifa zinasema vita hii ilisababisha hata Muhimbili kuhitaji malipo makubwa pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipoomba curriculums za Afya toka Muhimbili ili wazi adopt (ambazo kiuhalisia zilikuwa ni curriculums za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama hawajatengana) na kuweza kuleta faida kwa watanzania!!! Hivyo Muhimbili imekuwa inafanya kila aina ya figisufigisu kuhakikisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hakianzishi course za afya hasa za udaktari, ikihofu jina la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa ufupi wanataka wa monopolize Afya kwa Tanzania. Hofu waliyonayo unaweza iona kupitia wanafunzi waliochaguliwa kuingia kozi ya Medicine UDSM mwaka huu wa masomo 2016/2017, kwa kuona kuwa wanafunzi waliokuwa na ufaulu mzuri waliomba kujiunga na UDSM badala ya Muhimbili. Ingawa serikali inaamini kwamba Mlonganzila inaweza ikawa kiwanda cha madaktari wenye sifa Tanzania, tusidanganyike, Mlonganzila haitokuwa Harvard wala Stanford. Ni taasisi ya kawaida kabisa, hivyo isitishwe majukumu makubwa. Lakini itachekesha sana ikiwa IMTU, Kairuki, KCMC, UDOM, Bugando wataruhusiwa kuwa na Chuo Kikuu cha Tiba, huku UDSM ikiambiwa ifunge kozi za afya.

Mheshimiwa Rais, Tanzania kumekuwa na uanzishwaji holela wa vyuo vikuu vya tiba, vyote vikizalisha madaktari wasio na ujuvi wa kutosha kwa sababu ya usahili wa wanafunzi wasio na sifa, ukosefu wa walimu wa kufundisha, ukosefu wa maabara, kujazana kwa wanafunzi kwenye hospitali za kufundishia n.k. Bahati mbaya sana, hili limesababisha tuzalishe madaktari wengi wasio na sifa ambao pia hawana ajira. Kwa sasa inakadiriwa kuwa madaktari takribani 1400 waliohitimu hivi karibuni hawana ajira rasmi.

Mheshimiwa Rais, pamoja na sifa zake kubwa ilizonazo Muhimbili, bado ina mapungufu yaliyotajwa hapo juu. Chuo hiki ni kati ya vyuo vyenye changamoto kubwa ya walimu, na vifaa vya kufundishia. Ingawa wamejenga hospitali ya Mlonganzila, bado Muhimbili ina uwiano mkubwa sana kati ya idadi ya walimu na wanafunzi wa udaktari. Huwa ninashangaa sana kuona Chuo Kikuu Muhimbili kinadahili wanafunzi zaidi ya 250 kwa mwaka wa digrii ya udaktari pamoja na mapungufu yake makubwa wakati huohuo rasilimali watu, vifaa na majengo yakiwa na yaleyale yaliyotumika kudahili wanafunzi 40 hadi 70 kwa mwaka!!! Nasikia Mlonganzila ikifunguliwa rasmi Muhimbili watadahili wanafunzi zaidi ya 500 kwa mwaka kwa digrii ya udaktari. Hii ni sawa na kutoa photocopy ya madaktari. Huwezi ukatoa photocopy ya madaktari. Tutauana bure.

Mheshimiwa Rais, ukipitia vyuo vikubwa vyenye sifa kubwa duniani kama Harvard University (MA) wao mwaka 2016 walidahili wanafunzi 167 wa Medicine wakati uwiano wa mwalimu na mwanafunzi ni mwalimu 1 kwa wanafunzi 7-12. Wakati chuo kikuu cha California, San Francisco mwaka 2016 wamedahili wanafunzi 149 na wao wana uwiano wa wanafunzi 4 kwa mwalimu 1. Ukienda Johns Hopkins University utakuta pia wana udahili mdogo sana wa wanafunzi kama 120 kwa mwaka huku uwiano wa walimu na wanafunzi wote ukiwa ni wanafunzi watano kwa mwalimu mmoja. Chuo kikuu cha Washington ndio kinaonekana kudahili wanafunzi wengi zaidi ambao hivi karibuni walidahili hadi wanafunzi 235.

Mheshimiwa Rais, kwa Afrika ya Kusini, vyuo vikubwa kama Chuo Kikuu cha Cape Town hakijawahi dahili wanafunzi wa Medicine zaidi ya 220, wakati wenzao Witwatersrand wao hudahili kama wanafunzi wasiozidi 230, Chuo Kikuu Cha KwaZulu-Natal kupitia shule yao ya Tiba ya Nelson Mandela wao husajili hadi wanafunzi 250, wakati chuo kikuu cha Pretoria hudahili wanafunzi hadi 238. Vyuo vingine kama Stellenbosch hudahili wanafunzi 235, huku Walter Sisulu wakidahili wanafunzi 126. Pamoja na kutofautiana kwa mazingira kati ya nchi na nchi, ninashangaa sana kuona serikali inataka ikiongezee Mhuhimbili wanafunzi waliopo UDSM ili kuua kozi za afya za UDSM. Hii haiwezekani kufanyika katika mazingira yoyote yale, labda kama tunataka kuzalisha madaktari wenye vyeti tu lakini sio madaktari bora. Dawa si kufuta kozi za Afya UDSM na kuzihamishia Mlonganzila au mahala pengine, dawa ni kufanya capping ya wanafunzi kwa kila chuo chenye sifa ili kuzalisha madaktari wenye sifa.

Mheshimiwa Rais, ukizingatia kwamba sekta binafsi bado ni changa, na serikali haitoweza kuajiri madaktari wote, ni wakati muafaka sasa kwa serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na vyuo vyenye sifa za kuzalisha madaktari wachache na bora. Hii itafanikishwa kwa kufuta vyuo vyote visivyokuwa na uwezo wa kimfumo katika kufundisha madaktari (hapa chuo Kikuu cha Dar es Salaam hakihusiki) na pia kufanya capping kwa idadi ya wanafunzi wanaopaswa kudahiliwa na kila chuo (kuzuia Muhimbili kudahili wanafunzi wengi zaidi ya 250), na pia kuwa na mitihani ya pamoja. Tukifanya hivi tutapunguza uzalishaji wa madaktari wengi wasio na sifa lakini pia wenye nafasi chache ya kuweza kuajiriwa.

Mheshimiwa Rais, pia msisitizo uwekwe kwa mamlaka zenye sifa kujenga vyuo au matawi kwenye mikoa ya pembezoni ili kuwazoesha wahitimu kuwa tayari kufanya kazi mazingira ya pembezoni mwa nchi kama Sumbawanga, Katavi, Kigoma, Lindi, Singida, Tabora n.k.

Wasalaamu,

Tutafika, MWANZA

Nilishawahi andika kuhusu kutoziruhusu hospitali za mikoa kuhamishiwa Wizara ya AFYA

Rais Magufuli, Usiruhusu Hospitali za Rufaa za mikoa kutolewa TAMISEMI
 
Yes..wote wew na Magufuli huwa nawaelewa sana
Ngoja tuone kama watafanyia lazi ushauri huu na kufanya uchakataji wa kina kabla hawajafikia uamuzi.
 
Huu uchambuzi ni mzuri sana. Na unatakiwa akili ya ziada kuuelewa.

Nakumbuka hoja ya UDSM kuanzisha Kozi za Medicine iliwahi tokea ubishani mkubwa humu miaka 2 iliyopita.

Watu walisema UDSM haina uwezo huo kwa vigezo vingi sana:

Moja ni kuwa UDSM haina wataalam wanaoweza kutoa elimu inayohitajika kwa Tasinia ya Medicine. Mwaka huo UDSM walipoonesha nia hiyo, inajulikana ndo walianza kuajili walimu wa kufundisha Medicine na waliingia Mkataba na Chuo kimoja China kufundisha watalaam hao. Hii ina maana sana kataalam. Huwezi tegemea watu wa namna hii waje wainue taaluma yoyote ile.

Pili, Walihoji kuongezeka kwa Kozi bila kuwa na vitendea kazi na Madarasa ya kutosha kutoa taaluma hiyo. Mfano, huwezi tegemea Dispensary ya Chuo kuwa eneo la kutolea elimu ya kidaktari. Ukiangalia vyuo vingine unaweza angalia kwa urahisi sana. KCMC, Bugando, Aga Khani, UDOM na MUHAS na IMTU pia wana hospital kubwa sana. UDSM haina hivyo vitu. Pengine wapewe muda waandae mazingira hayo.

Sababu ya Tatu ni kuwa kumekuwa na Kozi fulani kwa UDSM kuanzisha bila kujipima uwezo wake zaidi ya kuiga. Mfano walitoa kuwa Miaka ya 2005-2009 walianzisha Kozi iliitwa Food and Biochemical Engineering. Hii kozi ilikuja kupambanishwa na kozi ya Food Science and Technology ya SUA. Mwisho ilishindwa kusimama, ikafa miaka ya 2010. Haijulikani wale waliodahiliwa walitunukiwa digrii gani.

Katika hili kuna Kozi inaitwa Wild Life pale UDSM na SUA pia. Wanafunzi wake wanajua nini kinatokea katika soko. Wengi wanatoka weupe kwa sababu ya kukosa elements nyingi za kozi hiyo kwenye soko.

Pia, mwaka juzi wameanzisha chuo cha Kilimo na Uvuvi. Kilichoonekana mpaka sasa wameshindwa kusimamia kozi ya Food Science and Technology na Bee Keeping. Shida kubwa imekuwa walimu wa kufundisha masomo haya. Wamewapa walimu wa Biotechnology, Fisheries na Microbiology kufundisha masomo haya bila kujali wanatakiwa wajue masomo ya msingi ya Food Science. Mwaka uliopita wameshindwa kudahili wanafunzi katika Uzamili wa kozi hizi kwa sababu hakuna anayeweza simamia tasnifu za level hiyo. Maana wale wenye Food Science MSc. tu.

Sawa tunahitaji jina ila tuwe pia tunaangalia nini kitatokea kama tunajianzishia tu kozi kwa ushabiki.

Kama wanataka kuanzisha degree za namna hiyo wanaweza leta strategic plan yake na kuangalia plan yao, ila si kuangalia lazima nao wawe na chuo cha namna hiyo.
 
umeongea vizuri but ulipodicredit mloganzila(muhimbili mpya) nmeona tu una interest zako tu na UDSM kuwa na coz za afya, mkuu hujasoma peke yako MUHAS nasi tumesoma hapo pia na tunaelewa vizuri na nadhan unafaham kuwa mloganzila ikianza kuoperate itakua ni chuo kilichojitosheleza mpk kwa teaching hospital yake binafsi, kutopata cheti cha udsm kusikuumize mpk ukawa blind usione kipi kizuri..............umejaza na negatives kuhusu MUHAS mkuu cjui ulikumbwa na nn enz unasoma hapo but mi naamin udsm ina safari ndefu sana kuja kuifikia MUHAS upande wa afya kama kweli umesoma muhimbili hili lazima ulifahamu.....
 
Nijuavyo UDSM wameamua kuipeleka idara ya tiba hospitali ya rufaa Mbeya. Nadhani wana kila uwezo wa kuachiwa wanafunzi waendeleze kozi zao.
 
umeongea vizuri but ulipodicredit mloganzila(muhimbili mpya) nmeona tu una interest zako tu na UDSM kuwa na coz za afya, mkuu hujasoma peke yako MUHAS nasi tumesoma hapo pia na tunaelewa vizuri na nadhan unafaham kuwa mloganzila ikianza kuoperate itakua ni chuo kilichojitosheleza mpk kwa teaching hospital yake binafsi, kutopata cheti cha udsm kusikuumize mpk ukawa blind usione kipi kizuri..............umejaza na negatives kuhusu MUHAS mkuu cjui ulikumbwa na nn enz unasoma hapo but mi naamin udsm ina safari ndefu sana kuja kuifikia MUHAS upande wa afya kama kweli umesoma muhimbili hili lazima ulifahamu.....

Sidhani kama kasema kasoma mwenyewe MUHAS. Ila kasema Mlonganzila sio Harvard.
 
Rais Yupo sahihi......MD kwa UDSM bado kabisa hawajajipangaaaa.......huo ndio ukwelii walimu wanachukua MUHIMBILI wanafunzi wanapigishwa over shule kisaaa walimu ni wa mudaa sehemu ya mazoezi hawanaaa yaani bado na kuwa chuo bora sio lazima uwe na kozi zote
 
Sidhani kama umesoma. Ni nadra sana kukuta chuo kikuu kina wanafunzi wa medicine zaidi ya 250. Hata uende Harvard au Stanford. Haifanywi hivi kwa sababu ya wivu, ila nia ni kuzalisha madaktari bora wenye good clinical skills ambazo zinapatikana kwa kuwa na wanafunzi wachache mawodini na pia kuwa na uwiano mdogo kati ya teaching staff na wanafunzi.

Chuo cha Muhimbili Kinatosha...

Umaongelea swala la Walimu....Hao Walimu waliokuwa UDSM watahamia Muhimbili kuungana n wenzao wa Mloganzila..
 
Kwa leo niko UDSM. Si dhambi maana ni chuo chetu. Lakini pia ni Chuo Kikuu pekee kilichoiletea sifa kubwa Tanzania. Makerere na Nairobi hawashindani na Muhimbili wala UDOM. Chuo kikuu kinajengeka kwa miaka, lakini course unaweza ukaitengeneza kwa mwaka mmoja tu.

mtoa mada ana interest zake UDSM haki ya nani
 
Hata Muhimbili walikuwa wanatumia MNH na MOI kama teaching hospitals. Si hospitali zao ingawa ni za JMT. Kuna faida nyingi ya hospitali kutumika kama teaching hospital. UDOM wanatumia Mkapa na Iringa kama teaching hospital. Mlimani wanataka wahamishie kozi yote ya MD kwenye hospitali ya kanda Mbeya. Sasa kosa lao ni nini? Mbona Muhimbili ndio wamejenga teaching hospital yao sasa baada ya zaidi ya miaka 20? Ina maana waliohitimu huko nyuma hawakuwa na sifa?
 
Kwa sasa wanafunzi wao wako mwaka wa kwanza na wa pili. Hawahitaji hospitali. Mwezi wa kumi wanaenda Mbeya. Bado wamo Tanzania. Mbona UDOM wanasomea Iringa Hospital.

Rais Yupo sahihi......MD kwa UDSM bado kabisa hawajajipangaaaa.......huo ndio ukwelii walimu wanachukua MUHIMBILI wanafunzi wanapigishwa over shule kisaaa walimu ni wa mudaa sehemu ya mazoezi hawanaaa yaani bado na kuwa chuo bora sio lazima uwe na kozi zote
 
umeongea vizuri but ulipodicredit mloganzila(muhimbili mpya) nmeona tu una interest zako tu na UDSM kuwa na coz za afya, mkuu hujasoma peke yako MUHAS nasi tumesoma hapo pia na tunaelewa vizuri na nadhan unafaham kuwa mloganzila ikianza kuoperate itakua ni chuo kilichojitosheleza mpk kwa teaching hospital yake binafsi, kutopata cheti cha udsm kusikuumize mpk ukawa blind usione kipi kizuri..............umejaza na negatives kuhusu MUHAS mkuu cjui ulikumbwa na nn enz unasoma hapo but mi naamin udsm ina safari ndefu sana kuja kuifikia MUHAS upande wa afya kama kweli umesoma muhimbili hili lazima ulifahamu.....
Niendelee kumkumbusha tu kwamba hata baada ya kuanzishwa hizo kozi huko UDSM bado walimu waliohusika kufundisha wametoka MUHAS. Si vyema kugawa vyuo vingii kwa kutumia walimu wale wale. MUHAS haijitoshelezi kwa walimu na hata hao wanaochukuliwa na UDSM ni products za MUHAS. Serikali na Dr. Magufuli wameona mbali Sana. Tuiache MUHAS izalishe wataalam wa afya UDSM iendelee kujiweka sawa na taaluma nyingine wa naweza shirikiana katika kuandaa wataalam waelekezi kama hao wa Biomedical Sciences.
 
Back
Top Bottom