NDUKI
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 3,423
- 2,414
Habari wandugu.
Natumai mu-wazima kabisa, naandika andiko hili kwa masikitiko makubwa sana kwa kweli.
Jana mnamo majira ya asubuhi nilipata taarifa ya kifo cha ndugu yetu mmoja amezoeleka kwa jina la Ka' Abdallah. Huyu jamaa bwana alikuwa ni dereva wa Prof. Mtulia aliyekuwa Mbunge wa Rufiji, amefanya kazi kwake tangu mwaka 1974 kamuendesha mzee na watoto mpaka watoto wamekuwa wakazaa akawaendesha mpaka na wajukuu.
Sasa bwana jana alikuwa anaenda Masaki kwa boss wake Dr. Ali Mtulia kuchukua gari ili awapeleke watoto shule, akatokea jamaa akampigia kelele za mwizi, basi wakanipiga hapo mpaka akafa.
Na wakati wanampiga walifika raia wakamueleza huyo jamaa aliyemuitia mwizi kuwa huyu jamaa ni dereva wa Dr. Mtulia sio mwizi tunamfahamu lakini bado jamaa wakawa wanazidi kumpiga mpaka akafa.
Katika hali kama hiyo inasikitisha sana kumuua mtu ambaye hana hatia kwa kujichukulia sheria mkononi. Ila mpaka dakika ya mwisho raia walimshikilia yule jamaa ambaye alimuitia kelele za wizi mpaka polisi walipofika wakamchukua yule jamaa na mwili wa marehemu wakaondoka nao.
Jamani tusiwe wepesi kuchukua sheria mkononi pasina kuwa na uhakika wa tukio alilofanya, kuwa na uhakika thabiti kuwa kweli unayemshuku amehusika na tukio na baada ya hapo mpeleke polisi sheria ikachukue mkondo wake kuliko kujichukulia sheria mkononi mtawadhulumu watu nafsi zao bure kabisa.
MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA KA' ABDALLAH. POLENI WAFIWA, NDUGU NA JAMAA.
NAWASILISHA.