Puma Petrol station ya Mbezi beach Africana acheni wizi wa mafuta

Hawa jamaa wa Puma hapa external wako vizuri sana, me nikijaza wese la elfu kumi kwenye kibaby walker changu naenda Chanika na kurudi bila wasiwasi.! Alafu unajazaje mafuta uko kwenye gari umerelax lazima upigwe me huwa nashuka kabisa nakuwa naangalia hivi kuhakikisha kama kweli yanaingia
kwenye que ya kujaza mafuta uwe makini sana kama aliyekutangulia kajaza mafuta less than 10litres
 
Guys.. Naombe ambao hamjui uwizinwa hawa Puma mmnyamaze acheni kutokwa povu kama huna gari na hayaja kukuta tuache sisi tueleze ukweli .

Puma Sinza kijiweni ni wezi sana, yaan unaweka mafuta unashangaa taa haiwaki.. Nikajipa moyo labda baada ya muda itastuka ila ajabu gari yangu mafuta ya elfu 20 tu taa ina waka na ninaenda km 100 , sasa cha kushangaza nilienda only Km, 8 kufika Lugalo gari ikazima njiani .. Kwa kua najua mafuta nimweka nikapanic kuhis ni jambo lingne kubwa .. Nikachukua bodaboda hadi Mwenge kutafuta fundi.. Fundi kajia kachokora kila koba ingine gari iko poa akiniambia mafuta namkatalia namuonyesha na risit na muda nilio weka ni dakika 12tu zilozopita mafuta ya 20,000/= ata yeye hakuwa tena na shaka ya mafuta tume hanangaika hapo masaa 3 baadaye akasema labda pampu imeziba akaanza kufungu tanki kwandani ajabu hakukua na hata tone la mafuta. Pampu ilikuwa nzima .. Sasa nikashangaa Puma pale kijiweni wamefanyaje wakati nimeona kabisa wameweka number na risiti ikatoka . Dah.

Jaman puma ni wezi nasema mm kwa uhakika kabisa maana siyo mara yakwanza kuna pale posta kwenye coner ya Viva tower Niliweka tena mafuta nikiwa na wahi Airpot ghafla nikashangaa gari ina nizimikia mnazi mmoja .. Wakati nikiweka mafuta ya 30,000/= kwa kuwa nilikuwa na haraka nikawahi na kidumu pale Collusum hotel kuna shel ya total .. Guy mm naonge kutoka moyoni hawa jamaa wa puma nimewachukia sina raha kabisa gari yangu haiingi tena shel zao
Sina kijiweni ukienda pump namba 2 na 4 ujue basi umeliwa. Pump za kwenda pale ni namba 1 na 3. Nimechunguza wenye vidumu huwa hawahudumiwi kwenye pump namba 2 na 4 pale ni 1 na 3 tu na bodaboda pia ndio pump zao nahisi wanalijua hilo.
 
Hawa jamaa wa Puma hapa external wako vizuri sana, me nikijaza wese la elfu kumi kwenye kibaby walker changu naenda Chanika na kurudi bila wasiwasi.! Alafu unajazaje mafuta uko kwenye gari umerelax lazima upigwe me huwa nashuka kabisa nakuwa naangalia hivi kuhakikisha kama kweli yanaingia
Ukishuka unaonaje mkuu kama yanaingia?? Kwani ule mkonga huwa ni transparent?
 
Sasa kama hawakuweka ya 40,000/= au kama haikuanzia zero si ndio wizi wenyewe huo?
Lengo la maswali yangu ni kumsaidia ajue jinsi ya ya kuzuia huo wizi. Amekiri hata risiti hajachukua sasa hapo hamna ushahidi kama kaibiwa au kaweka mafuta hapo.
 
Hiki kituo ukiweka mafuta usiku imekuwa kwako, wajirekebishe wawaulize Oilcom Mbezi chini wanalia baada ya GBP kufunguliwa, Oilcom walizoe kuwaibia Wateja sasa hivi wanabembeleza watu warudi ila ndio hivyo watu wakishaamua imekuwa kwao
Lete ushahidi umeibiwa Mimi kama Menejanitakulipa Nakuomba radhi
Nashukuru Sana kwa taarifa nitalifanyia kazi
Hila Kama unakusudio lakuchafua Puma
Utakuwa unafanya jambo baya Sana
Wateja wetu wapuma ninaomba radhi kwa usumbufu huu atujawai kupata malalamiko toka kwa wateja Wetu ndio mara yakwanza
Naomba mtuunge Mkono kwakutokosoa na kutuelimisha sehemu tunapokosoa
 
Sina kijiweni ukienda pump namba 2 na 4 ujue basi umeliwa. Pump za kwenda pale ni namba 1 na 3. Nimechunguza wenye vidumu huwa hawahudumiwi kwenye pump namba 2 na 4 pale ni 1 na 3 tu na bodaboda pia ndio pump zao nahisi wanalijua hilo.
Kwa system ya sasa hivi kuibiwa ni kwa njia hii tu yaani pump inasetiwa kutoa pungufu ya lita moja labda 0.9L badala ya 1L lakini hizi ni tuhuma nzito sana ndugu unaweza kushtakiwa uthibitishe.
 
Lete ushahidi umeibiwa Mimi kama Menejanitakulipa Nakuomba radhi
Nashukuru Sana kwa taarifa nitalifanyia kazi
Hila Kama unakusudio lakuchafua Puma
Utakuwa unafanya jambo baya Sana
Wateja wetu wapuma ninaomba radhi kwa usumbufu huu atujawai kupata malalamiko toka kwa wateja Wetu ndio mara yakwanza
Naomba mtuunge Mkono kwakutokosoa na kutuelimisha sehemu tunapokosoa
Nashukuru sana mkuu kwa kuja na kutusikiliza najua tatizo ni wafanyakazi sio Sera ya Puma kuibia Wateja, binafsi nimepata tatizo Africana Mbezi lakini kuna wengi wamelalamikia sehemu zingine, sipo kwa ajili ya kuwaharibia biashara sababu sifanyi aina ya biashara yenu Bali kuwasaidia mfahamu kuna hili tatizo ndio maana watu wamekuja na malalamiko ya vituo vingine
 
Lengo la maswali yangu ni kumsaidia ajue jinsi ya ya kuzuia huo wizi. Amekiri hata risiti hajachukua sasa hapo hamna ushahidi kama kaibiwa au kaweka mafuta hapo.
Binafsi nilipendelea sana kuweka mafuta Puma, na nimeshangaa sana kwa kilichotokea maana niliamini puma ni waaminifu, nakubali pesa nimeshapoteza lakini nimeona ni bora kuwasaidia wajue hili tatizo lipo na wengi wamekuja na malalamiko kama haya. Ni vyema kuwasaidia kwa kuwaambia kuliko kukaa kimya na kuwakimbia sitakuwa nimewasaidia. Pesa nimeshapoteza lakini ni kama nimeumwa na nyoka nitakuja mwangalifu sana
 
Hiki kituo ukiweka mafuta usiku imekuwa kwako, wajirekebishe wawaulize Oilcom Mbezi chini wanalia baada ya GBP kufunguliwa, Oilcom walizoe kuwaibia Wateja sasa hivi wanabembeleza watu warudi ila ndio hivyo watu wakishaamua imekuwa kwao
PUMA sijawahi ona. Ngoja watu tufanye uchunguzi.
 
Nafikiri dawa ni Puma kufanyia kazi haya malalamiko otherwise ipo siku utawekwa mtego iwe aibu kwa kampuni ambayo imejijengea jina kubwa. Mimi ndipo ninapojaza mafuta mara nyingi kama nikipitiliza GBP ambayo ndio my first choice ...
 
Unaibiwaje mafuta na kuna risiti za efd pembeni..weka mafuta dai risiti ya efd..
 
Kwanza yule Dada niliposimamisha Gari akawa ananionyesha nisogeze mbele kama vile ile Bomba ya mafuta ni fupi, then nikasogeza Gari akaja MTU wa pikipiki akawekewa haraka baadae akatoa kwa pikipiki akaanza kuniwekea Mimi sikuweza kuona vizuri kwa sababu alinisogeza mbele UKAWA shida kwangu kuona ile meter inavyosoma. Nilipoondoka taa ya Gari haikuzima ilani nikafikiria labda itazima mbele, dah mpaka mohe hakuna kitu nikajua nimeliwa

Yaani umetoka kujaza mafuta taa ya mafuta bado inawaka na wewe ukaendelea kuendesha gari? Mavilinga stori haya......
 
Badilisheni mfumo. Mafuta jazeni wenyewe. Bongo raha sana watumishi nyumbani, ofisini, shambani, hotelini mpaka kujaza mafuta, haaah!
 
Kwa system ya sasa hivi kuibiwa ni kwa njia hii tu yaani pump inasetiwa kutoa pungufu ya lita moja labda 0.9L badala ya 1L lakini hizi ni tuhuma nzito sana ndugu unaweza kushtakiwa uthibitishe.
Nilishawahi kuibiwa pale ndugu na niliamua kurudi na kumuona meneja ambaye aliamuru niwekewe tena mafuta ya pesa ile ile niliyotoa na akaniomba msamaha.
 
Kwa system ya sasa hivi kuibiwa ni kwa njia hii tu yaani pump inasetiwa kutoa pungufu ya lita moja labda 0.9L badala ya 1L lakini hizi ni tuhuma nzito sana ndugu unaweza kushtakiwa uthibitishe.
Hapo itakuwa pungufu ya lita moja au 0.1L???
 
Back
Top Bottom