Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 189
NL,
Nilifika shuleni pale mwaka 1991 kuchukua form za kujiunga na shule hiyo kwani mtoto wa dada yangu (Dr sasa wa mifugo) alikuwa anahamia hapo kutoka Forodhani sec. Nilichukua basi moja lenye kichwa cha roli kutoka Ilala hadi nikawa nimefika pale kwenye kituo cha mabasi (Pugu Sec.) na pana miti mirefuuu. Nikaangaza kulia na kushoto kama nilivyoelekezwa. Nikarudi nyuma kidogo na kuingia upande wa kushoto kama waenda Dar (Kulia kama waenda Kisarawe). Nikaingia hadi sehemu palipo majengo na kuanza kuangaza angaza mtu yeyote nimuulize ilipo shule ya Pugu. Nikamuona mama mmoja na kumuuliza, kama anafahamu shule ya secondary ya Pugu ilipo. Mama hakuamini na akaanza kucheka. Mie sikuelewa kisa cha kucheka ni nini hasa? Mama akaniangalia na kusema "baba, hapa ulipo ndiyo Pugu Sec." Sikuamini macho yangu kama kweli hii ndiyo Pugu Sec. Hata kambi za JKT nilizopitia zilikuwa na nafuu. Yale majengo yalikuwa yamechoka na nikawa naona kama vile yapo pale tangu JKN ni mwalimu na hawajafanyia upanuzi au matengenezo makubwa yoyote.
Nilionyeshwa Ofisi na kuchukua form zangu na kurudi zangu mjini. Sikuamini kama ile inaweza kuwa secondary, tena PUGU (Pugu jina kubwa). Anyway, mliosoma hapo msijione kuwa nawatukaneni. Nimekuja kukata tamaa zaidi baada ya kuona lile bweni lililomliza Naibu waziri wa Elimu, mama nani sijui....
Kuna ukame hivi wa POND boys hapa JF......Can't be!
Mzee unauliza makofi polisi??? Unategemea Pugu boys wasiwemo JF ili iweje tena mkuu! Tupo pamoja
Kweli mkuu umenikumbusha mbali sana,those time tulikuwa tunapandia chai maharage mwisho wa lami,believe me ukioga maji ya Pondi lazima utoke na Fungus!!!
HA HA HA HA HAAAAAA!!!! NEXT LEVEL.
At least we now have something in common!
Nilikuwa Pugu in 1975 High School.
It was a very challenging place.Chakula hamna, maji hamna na tarehe sitaishau ni 5/5/1975 wanafunzi wote tuliandamana kwa mguu toka Pugu hadi kwa Mkuu wa Wilaya Mama Kunambi kuprotest hali mbaya ya maisha pale shuleni.
Marehemu Mama Kunambi alituonea huruma sana na akakodi maba si ya UDA kuturudisha shuleni.
Kwa miezi kadhaa baada ya hapo chakula na na maji yalirudi kwa fujo!!
Mwalimu Mkuu aliyejulikana kama Mbise wakati huo alitushukuru kwa undertones kwa kuwezesha tatizo kujulikana na hatua kuchuliwa haraka.
Vile vile hivyo mwaka huo 1975, Mozambique ilipata uhuru wake na tulisherehekea sana na kwa fujo kubwa na kikundi cha ngoma ya sindimba ya kimakonde toka Gongo la Mboto!!!!
Hivi pale Baghdad siku hizi vipi, bado wauza mafuta na wapiga ndumu wapo?
nimefurahi sana kusikia baghdad!!!!! niliacha kiatu pale masela waliomba hela ya ndumu na mimi nikawa hata 100 ya kupanda gari za chanika sina, pia kwa wale waliokuwepo till 2000 wanakumbuka jamaa mmoja alikua anaitwa Mabagala? anakukimbiza hata ukiwa uchi.
Unawakumbuka walimu wafuatao?Mabagara,Wajimira,Nzoi,Msungu(marehemu),Secondmaster Swai(marehemu),Headmaster Mtera,Mama Mukuru,Mzee Mukuru,Makono(marehemu),Teti,Mkwiche,Grace Chuma,Mamiro,Mama Mtera,Mbulanya,Godfrey Wasiwasi,Kaunda(mwalimu wa michezo 1984-1988),Mzava,Chamuriro,Mugyabuso(marehemu),Bakari Mbonde(Ex-Rufiji Mp)n.k Orodha yao ni wengi sana,waliotangulia mbele ya haki Mungu awaweke mahari panapostaili, aaaammmmmmiiiiiiiiiinnnn.
Aksante kwa kutukumbusa mambo ya DOCEBIT VOS OMNIA,