Public hearing wazanzibar watupwa nje ya ulingo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Public hearing wazanzibar watupwa nje ya ulingo

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by MkamaP, Apr 7, 2011.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Maoni ya watanganyika ndio yataamua hatima ya wazanzibari, hii inatokana na kweli ya kwamba vituo vimeweka Dodoma na Dar ktk ardhi ya Tanganyika.

  Swali ni je wazanzibari watajifunza nini ? na je madai ya wazanzibari kutawaliwaliwa na mabeberu kutoka Tanganyika ni sahihi? na je ni hatua gani moja na ya uhakika wazanzibari wataichukua?
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Zanzibar pia ni kituo kwa hiyo watachangia
   
 3. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Wao wataanza lini kuchangia?
   
 4. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Why the Zanzibarians can decide on their own and move on while the mainlanders can't do it without the Islanders?
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Hata huko Dodoma na Dar wanaweza kuchangia pia, japo uwakilishi wao utakuwa mdogo..
   
 6. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mkuu unajua unachokisema? Au unafuata mkumbo tu.
   
 7. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwani Mbeya, Kagera, Mtwara, Kigoma n.k watachangia lini?. Hii ni katiba ya Jamhuri ya Muungano na Zanzibar ni sehemu mojawapo tu ya Jamhuri kama mikoa mingine ya bara
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wenzenu hata huku Tanganyika nako tuliishia kujitolea tu maoni sisi kwa sisi pembeni tu mwa barabara kule Dodoma mara baada ya CCM kufunga geti la bunge kuelekea ukumbini.

  Kama na nyinyi huko hamkupata fursa basi maana yake ni kwamba kumbe shuguli hii ilikuwa ni ya MAFISADI tu wa CCM kubadilishana maoni peke yao juu ya mambo ya taifa yanayotuhusu sote.

  Hadi hapo basi nyie ni vema mkatambue ya kwamba adui wetu sote ka Jamhuri ya Muungano wa Tanzani ni CCM; kwisha kazi!!!!!!!!!!!!

   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Mimi na wewe tunatofautiana katika hili.
  Zanzibar ni mbia wa Muungano, si sawa na Mbeya, Kagera ,Mtwara au Kigoma.
  Ni sehemu mojawapo ,yes,lakini sio sehemu mojawapo tu, pia ni mbia wa Muungano.

  Hili ni kosa kama lile la kumtoa Rais wa Zanzibar kuwa makamo Rais. tunafikiri ni smart move lakini ina-undermine Muungano wenyewe.
  At the end, Wazanzibari wanapata mwanya wa kuthibitisha kuwa wanaburuzwa.

  May be ,we have a diferent concept of what is the partial union of two countries.
  Nimesema partial kwa sababu hivyo ndivyo ilivyo.muungano wa baadhi ya mambo na kutokuunganisha baadhi ya mambo.

  Tunatengeneza "Kero" zaidi badala ya kujaribu kutatua tulizonazo.
  kila siku nakumbushia...mifano miwili..Ethiopia na Eritria....Indonesia na East Timor. It will be costly!
   
 10. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndio Mheshimiwa Nonda, nakubaliana nawe sikutaka kuandika mengi bali nilitaka kuleta hamasa kwa Wanzanzibar kuleta hoja zao hapa JF. Tatizo ni kwamba utaratibu mzima ni mbovu kupita kiasi, kuliwa na haja ya sehemu kubwa ya Jamhuri ya Muungano kushiriki lakini ccm kama kawaida yao hawataki ushiriki wa watanzania wengi. Kinachonishangaza zaidi ni kwamba Wazanzibar wako kimya mno kwa hili wala sijaona wakilalamika zaidi ya hii thread. Inaleta maswali mengi ya kujiuliza kwamba hivi baada ya CUF na CCM Zanzibar kufanya coaliation, Wazanzibar madai yao katika muungano ndio yamekufa? wanalidhishwa na hii hali ya muungano ndio maana CCM wanakiburi hata kuamua kuwa mambo ya muungano hayana mjadala katika mchakato wa katiba mpya unaoendelea?.
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa. Mkuu.
  Unajua CCM hawatafanya haki hata siku moja.
  Na kwa muelekeo ambao wanauchukua wataipeleka nchi pabaya.
  CCM haifanyi vitu kwa maslahi ya taifa kwanza. Wao lazima wafanye calculation za CCM kwanza.
  This was a unique chance kwa CCM kutubia na kuingiza nchi katika njia ya amani na utulivu wa kweli.

  Sasa hata katiba haijafikia hatua ya kuandikwa wanaanza madudu, sijui ikifikia hatua hiyo itakuwaje?
  Nchi itadumu lakini hakuna uhakika kuwa chama cha siasa chochote kinaweza kudumu. Tunisia si wamekifuta chama cha Ben Ali.

  Walio huko CCM, watokee wengine wawaeleweshe viongozi wao. wakati hauko upande wao.Mageuzi yanayotokea katika nchi nyengine wasifikirie hakuna uwezekano wa kutokea hapa TZ.

  Mkuu. Nimesikiliza baadhi ya semina zao mtandaoni za kuhamasisha wananchi kushiriki kutoa maoni...wako moto sana. Lakini inaonekana hiyo GNU yao imepingwa na baridi.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu msianze kulalamika hovyo pasipo kuelewa maudhui ya Muswada wa Jk ambaye kasema wazi swala la Muungano lisiguswe..
  Sasa la Wazanzibar wa nini ikiwa maswala yote ya muungano hayataguswa?
  Labda tushangae sote huu muswada.. hii katiba itakuwa katiba gani ukiondoa vitu muhimu vinavyoijenga kuwa katiba ya jamhuri ya Muungano..

  Kero yenu ni kero ya Watanzania wote na ndio maana sote tunaupinga muswada huu kwani hata bara tunataka nafasi yetu ktk Muungano ijadiliwe na hakika hakuna solution ila kwa kuunda serikali tatu na CCM hawawezi kukubali kugusa muungano ambao umewapa fursa ya kuunda serikali ya mseto kinyume cha katiba na taratibu za vyama vingi.
   
 13. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye bold ......Anaogopa asije akawa Gorbachev wa pili, hataki muungano umfie mikononi mwake ndio maana anachukua approach ya funika kombe mwanaharamu apite. Lakini ukiangalia kwa undani unaweza kuona katika mchakato huu aina ya muungano tunaotaka kama bado watu wengi wanaona una umuhimu ulikuwa ni lazima ujadiliwe.

  Kero moja ya muungano ni kuwa mipaka ya kimadaraka ya Tanzania na Tanganyika haijulikani inaanzia wapi na inaishia wapi na ndio umekuwa wimbo mkubwa wa wazanzibari sasa kama ni moja ya vitu ambavyo havitakiwi kujadiliwa tutatua vipi kero hii?
   
 14. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  angalizo:
  Kwa taarifa tu ni kuwa kamati ya bunge ya sheria na utawala ipo zanzibar asubuhi hii katika ukumbi wa bwawani na wadau mbali mbali wameshiriki katika mjadala huo. Punde tu nimetoka baada ya mkutano kuaikhirishwa hadi saa nane mchana baada ya salat el jumaa.
   
 15. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbona kinyemela hivyo, si walisema Wazanzibar watashiriki kituo cha Dar?. Naona sasa mjadala unaendeshwa kwa kuvizia kazi iko Tanzania
   
Loading...