PSSSF Yatumia Bilioni 880 Kulipa Mafao

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019
Wanachama elfu kumi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamelipwa takribani Bilioni 880 ikiwa ni malimbikizo ya Pensheni kwa wastaafu tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo mapema mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Meneja Kiongozi, Uhusiano wa mfuko huo Bi. Eunice Chiume amesema kuwa dhamira ya Mfuko huo ni kuhakikisha kuwa wanachama wake wanaendelea kulipwa mafao yao kwa wakati kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwafanya wastaafu wote kuishi maisha bora.

“Katika kipindi cha miezi 6 Mfuko umeendelea kutoa huduma bora hali iliyowezesha wastaafu wetu zaidi124,000 kuendelea kupata huduma zetu katika ofisi zetu za mikoani pamoja na Zanzibar” alisisitiza Chiume.

Akifafanua amesema kuwa mfuko huo una wanachama takribani 763,000 kote nchini na unaendelea kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma bora kwa wanachama wake.

Mfuko huo umeendelea kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kusimamia uwekezaji katika sekta hiyo ikiwemo kiwanda cha viatu Karanga kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kinachomilikiwa kwa ubia na Jeshi la Magereza.

Eneo jingine ni uwekezaji katika amana za Serikali, kiwanda cha Tangawizi kilichopo Same Mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande wa zoezi la uhakiki wa wanachama wa mfuko huo amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kati ya Desemba 2018 hadi Machi 2019 na ni endelevu.

Pia alitoa wito kwa wanachama wa mfuko huo ambao wamestaafu kuhakiki taarifa zao kupitia ofisi za mfuko huo zilizopo mikoani ili kuepuka usumbufu ikiwemo kusitishiwa pensheni.

Aliongeza kuwa dhamira ya kufanya uhakiki huo ni kuwezesha mfuko kuhakikisha kuwa anayelipwa pensheni ni yule anayestahili kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.

Kwa upande wa watumishi wa mfuko huo wameaswa kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wa mfuko huo ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza utoaji wa huduma bora.

Mfuko wa PSSSF ni matokeo ya kuunganishwa kwa mifuko ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi hasa kuchochea ukuaji wa sekta ya hifadhi ya Jamii hapa nchini.
 
Huyu mama natetea ugali tu, Kama yule aliyekuwa msimamizi ( Regulator) wa mifuko hii kwa kutetea kikokotoo
 
Mbona wapo wengi wanalalamika mitandaoni hawajalipwa? Mna uhakika sio data za kupikwa hizi!?
 
Ni rahisi kuongea lakini no action taken, nimestaafu disemba mpk sasa napambana na hali yangu, huyu anadai tumelipwa, aeleze ni wasaafu wa toka lini amelipa. Anyway he or she will also retire one day
 
Nikisoma heading tu naona ni trilion 880!!!
Hapo tunalipa deni la taifa alafu tanawatukana USA wakikataa tunawatangazia vikwazo wakileta ubishi tunaingia vitani na baada ya hapo tunabakiwa na hela ndogo tunakuwa baba wa Dunia
 
... walipeni wastaafu fedha zao kwa wakati na kwa kiasi stahiki; acheni longolongo au kutafuta sifa. Ni jasho lao hilo.
 
Mafao ya uzazi mbona wanazingua wenginw tulikuwa GEPF na tulikuwa tunaenjoy iyomambo
 
Ni rahisi kuongea lakini no action taken, nimestaafu disemba mpk sasa napambana na hali yangu, huyu anadai tumelipwa, aeleze ni wasaafu wa to p;lka lini amelipa. Anyway he or she will also retire one day
Comrade pole,tumelipwa sisi wengine juzi, tulisha staafu muda mrefu sasa waliposema tuhakiki upya mwezi January 2019
hatukupata taarifa , basi ikawa dana dana sana , sasa hatimaye tumelipwa mapunjo ote. Tumelipwa mafao ya kila mwezi,
Hata hivyo yule meneja alisema wanaolipwa kila mwezi ni kama 400 sasa sikujua kama ni Dar peke yake au vipi
 
1114275

Wanachama elfu kumi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamelipwa takribani Bilioni 880 ikiwa ni malimbikizo ya pensheni kwa wastaafu tangu kuanzishwa kwa mfuko huo mapema mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Meneja Kiongozi, Uhusiano wa mfuko huo Bi. Eunice Chiume amesema kuwa dhamira ya Mfuko huo ni kuhakikisha kuwa wanachama wake wanaendelea kulipwa mafao yao kwa wakati kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwafanya wastaafu wote kuishi maisha bora.

“Katika kipindi cha miezi 6 Mfuko umeendelea kutoa huduma bora hali iliyowezesha wastaafu wetu zaidi124,000 kuendelea kupata huduma zetu katika ofisi zetu za mikoani pamoja na Zanzibar” alisisitiza Chiume.

Akifafanua amesema kuwa mfuko huo una wanachama takribani 763,000 kote nchini na unaendelea kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma bora kwa wanachama wake.

Mfuko huo umeendelea kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kusimamia uwekezaji katika sekta hiyo ikiwemo kiwanda cha viatu Karanga kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kinachomilikiwa kwa ubia na Jeshi la Magereza.
Eneo jingine ni uwekezaji katika amana za Serikali, kiwanda cha Tangawizi kilichopo Same Mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wa zoezi la uhakiki wa wanachama wa mfuko huo amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kati ya Desemba 2018 hadi Machi 2019 na ni endelevu.

Mfuko wa PSSSF ni matokeo ya kuunganishwa kwa mifuko ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi hasa kuchochea ukuaji wa sekta ya hifadhi ya Jamii hapa nchini.
 
Ni wajibu wao kisheria.... so ts not a breaking news!!
View attachment 1114275

Waliolipwa hela zao kikamilifu zile za mkupuo ni kuanzia July mwaka 2018 kurudi nyuma. Kuanzia August 2018 kuja mbele bado wanadai nikiwemo mimi
 
Back
Top Bottom