PSSSF na NSSF walipe watu

kamtesh

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
1,395
Reaction score
514
Inakuaje kulipa watu inachukua muda kiasi hiki? Visingizio, tunabadilisha mifumo. Ninacho jua, mifumo hubadilishwa mapema.
Hivi waliofukuzwa kazi nao wanamajuku kama yenu. Walio staafu hivo hivyo. January ndo hiyo yaja msimu wa ada za shule. Azitapashwa kulipwa.
Walipeni jameni, kama mtu anakahela anastahili kulipwa, mlipeni atatue matatizo yake. walipeni wateja wenu. December hii use mwezi wakuwapa watu unafuu wamaisha ili nao wauanze vema mwaka ujao. Its a shame kwa mashirika haya mawili, kua kero kwa wateja linapokuja swala lakuwalipa. Kupokea michango na kutafuta wanachama wapya munabidii kweli, Ila kuwalipa stahiki zao ni bugudha kweli. Mutawapataje wapya wakati wanaona adha wanayo pata walio ndani. Huduma kwa wateja ni zero kabisa.
 
Aisee Au nchi iuzwe wananchi wagaiwe hela watembee mbele...
 
Haya mashirika yamekua gumzo, watu hawalipwi kwa wakati, visingizio, wanabadilisha mfumo. Mfumo usio isha kubadilishika, tunaanza kua na wasiwasi kuhusu utaalamu wa watumishi wa IT wamashirika haya.
 
Wanasahau kwamba na wao ni wastaafu watarajiwa..
 
Hawaoni adha wanayoipata watu, hela yao kuipata shida, mtu anaomba leo, kuipata hela baada ya mieizi mitatu hadi sita wengine mpaka mwaka au miaka. Sio uungwana. Lipeni watu ndani ya wiki au wiki mbili. Imekua kero sana kwa walio staafu na kufuzwa kazi. Hawa wote wanamajukumu ya kifamilia muwaheshimu. Leo ni wao kesho ni nie, mutastaafu mutaona nadhara ya huu upuzi wakuchelewa kulipa watu wakati huna kitega uchumi chochote.
 
Watumushi wengi hawana vitega uchumi hela hawana unless awe aliiba kwa nafasi take.
 
dah kuna ka hela Mrs anadai ngoja tuanze kudai tena
 
Hawa watu lazima tuandamane kudai haki ya mafao. Wajua watanzania tunapokaa kimia, tunaonekana wajinga, hatujitambui. Ndo maana kila kiongozi anaamua anavyotaka. Ndo maana wameamua 25% mkupuo, watanzania wadau ba vyama vya wafanyakazi, kimia. Kesho watafika 10% mafao ya mkupuo. Sii hatusemi wala kulalamika. Ndo maana kulipwa mafao inakua shiiiidaaa! Ubaya nikwamba, yule ambaye hajastaafu, anaona mimi bado uainihusu. Kumbe naye itakuja kumuhusu miaka kumi ijao, naye atakuja kulalamika hapa hapa kuhusu mafao.
Kuna genge la watu fulani wanania ovu na mafao ya watu. Walipeni watu mafao yao.
 
Wameshindwa kulipa mafao kama walivyojinasibu kwamba ifikapo January, watakua wamelipa mafao yote. Kumbe ulikua ulaghai wa mkurugenzi mtendaji mkuu, kutafuta kiki kwa waziri na rais.
Leo ni tarehe moja mwezi wa pili, wastaafu wengi hawaja lipwa. Viongozi never walk the talk, :ts a shame.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…