mambo_safi
Senior Member
- Jul 22, 2019
- 180
- 446
Mafao mengi ya wanachama yakilipwa huwa hayalipwi yoote. Unakuta mtu anastahili kulipwa milioni 35. Badala ya kulipwa yoote unalipwa milioni 30. Anaambiwa aandike barua kukubali kulipwa milioni 30 alafu nyingine atalipwa baada ya michango yake kuwekwa sawa. Hicho kiasi kilichobaki ambacho wanakiita "Mapunjo" atafuatilia miaka nenda miaka rudi bila kulipwa. Kwanini hamtaki kulipa hela za watu? Tumeandika barua nyingi kukumbushia hazifanyiwi kazi nyingine zinatupwa haziwekewi rekodi ukirudi wanasema barua haionekani!!! Kwanini mnafanya hivyo? Hiyo si ni hela yake na haki yake na jasho lake kwanini mnafanya dhuruma? Huuu ni mpango wa wizi wa mchana wa mafao ya wanachama kwasababu ukijumlisha mapunjo yoote ya wanachama (kwasababu hakuna mwanachama alishawahi kulipwa mafao yoote) ni mabillioni ya hela. Ukifuatilia wanasema tunashughulikia kwanza ambao hawajalipwa kabisa wewe subiri. Kwahiyo asubiri mpaka mwaka gani? PSSSF epukeni laana zisizokuwa za lazima lipeni Mapunjo ya wanachama