PSSSF inavyowatesa wazee wastaafu

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Hakika inasitikisha sana kwa wanayopitia wazee wastaafu waliojitolea kuitumikia nchi kwa nguvu zao na kuchangia michango yao kwenye mifuko ya jamii lakini leo wanashinda wanazurura kudai haki yao.

Kuna mzee alistaafu Julai 2018 lakini mpaka leo amekuwa akizungushwa na watendaji wa PSSSF kwa kuambiwa njoo kesho njoo mwezi ujao.

Kwa mujibu wa maelezo ya mstaafu huyu anadai mafao yake ya serikali kuu kwani amefanya kazi serikali kuu na serikali za mitaa.Tunaiomba serikali ikawaangalia wazee wastaafu kwa jicho la huruma na kuwalipa mafao yao.
 
Makosa yapo sehemu tatu kuu,mwajiri na mwajiriwa.PSSSPF wanatumia makosa hayo katika kuhakikisha wanakaa na fedha za waastaafu kwa kipindi kirefu.
Kuna waajiri ambao baadhi ya michango hawakuiwakilisha na kuna wakati nyaraka zinatofautiana.Kwa PSSSPF jina likiwa na tofauti hata ya herufi moja tayari wameshapata sababu,RICHARD na RICHAD,HASSAN na HASANI.
Kwa wastaafu wengi wanashindwa kuandaa nyaraka zao mapema na kuzihakiki,hii inasababisha usumbufu mkubwa na hili linatakiwa idara ya uajiri iwasaidie mapema.
Kwa PSSSPF hawana customer care,namba wanazotoa hazipokelewi.
Ni wakati muafaka wa kuwa na consultancy companies za kuwasaidia wastaafu.
 
Hakika inasitikisha sana kwa wanayopitia wazee wastaafu waliojitolea kuitumikia nchi kwa nguvu zao na kuchangia michango yao kwenye mifuko ya jamii lakini leo wanashinda wanazurura kudai haki yao.

Kuna mzee alistaafu Julai 2018 lakini mpaka leo amekuwa akizungushwa na watendaji wa PSSSF kwa kuambiwa njoo kesho njoo mwezi ujao.

Kwa mujibu wa maelezo ya mstaafu huyu anadai mafao yake ya serikali kuu kwani amefanya kazi serikali kuu na serikali za mitaa.Tunaiomba serikali ikawaangalia wazee wastaafu kwa jicho la huruma na kuwalipa mafao yao.
Jamani Raha sio rahaaaaa?
Au nadanganya ndugu zangu?
Mliona ujiko mliposikia miradi inajengwa kwa fedha za ndani, Sasa kufeni tu sisi hatujali, lazima kila water body nchi hii ipate daraja la kifahari.
MITANO Tena
 
Psssf wana kitu inaitwa FAO LA UZAZI,,, Huwezi kuelewa maana yao katika hili kwani kuna watu walijifungua January 2020 lakini hadi sasa hawajaambulia chochote...
Sasa jiulize nini lengo la FAO LA uzazi ? Binafsi naamini hili FAO limekusudia kumsaidia aliyejifungua kukidhi mahitaji kadhaa baada ya kumaliza kujifungua! Sasa huyu m/mke kakaa hadi mwaka umepita mtoto kawa mkuubwa mfano anatembea na pengine ni mjamzito tena lakini cha ajabu bado anasubiri mafao ya kijana wake aliyemzaa miezi zaidi ya 12 iliyopita..
Kwanini hawa watu PSSSF wanasumbua watumishi na wastaafu hivi? Kama kitu ni kigumu kiutekelezaji ni heri wakaachana nacho tu! Sipendi kuona watu wanazungushwa kwenye kudai haki zao bila sababu ilihali wamekidhi vigezo vyote na kupewa visingizio vya kijinga
 
Tatizo Hela hakuna huko tunajenga kwetu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo huwa hamlioni haraka. Mifuko hii hutegemea zaidi waajiriwa waliopo kazini ili kupata hela ya kulipa wastaafu. Waajiriwa anapokatwa mshahara plus makusanyo toka vitegauchumi, unapata hela ya kulipa wastaafu na gharama za kuendesha shirika. Sasa hivi watu wanastaafu, maana yake mawasilisho kutoka mishahara yanapungua, kwa sababu hakuna ajira Mpya! Hela ya kuendesha mashirika, ikiwa Ni kulipa mishahara ya watumishi Wa psssf na pia kulipa wastaafu, zitoke wapi? Ajira Mpya hakuna. Au nadanganya!
 
Psssf wana kitu inaitwa FAO LA UZAZI,,, Huwezi kuelewa maana yao katika hili kwani kuna watu walijifungua January 2020 lakini hadi sasa hawajaambulia chochote...
Sasa jiulize nini lengo la FAO LA uzazi ? Binafsi naamini hili FAO limekusudia kumsaidia aliyejifungua kukidhi mahitaji kadhaa baada ya kumaliza kujifungua! Sasa huyu m/mke kakaa hadi mwaka umepita mtoto kawa mkuubwa mfano anatembea na pengine ni mjamzito tena lakini cha ajabu bado anasubiri mafao ya kijana wake aliyemzaa miezi zaidi ya 12 iliyopita..
Kwanini hawa watu PSSSF wanasumbua watumishi na wastaafu hivi? Kama kitu ni kigumu kiutekelezaji ni heri wakaachana nacho tu! Sipendi kuona watu wanazungushwa kwenye kudai haki zao bila sababu ilihali wamekidhi vigezo vyote na kupewa visingizio vya kijinga

Hao ni kawaida yao mkuu,hawana pesa.
 
Back
Top Bottom