PSPF huu ni sawa na utapeli

PSPF huu ni sawa na utapeli

moj6

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Posts
3,354
Reaction score
5,006
Habari wakuu ,

Jana nilikuwa kwenye daladala nikielekea posta, kwa pembeni yangu kulikuwepo na mzee mmoja ambaye alikuwa anaelekea ubongo terminal ,katika kupiga story za hapa na pale yule mzee akanielezea historia yake kua ni mstaafu wa wizara ya kilimo na mifugo , carrier yake ni agricultural officer wa kata mkoan Kagera ,alikuwa akilalamika sana kuwa shirika hili la mafao kwa wastafu linamzungusha sana kumpatia hela zake,

Mzee amestaafu rasmi mwezi wa nne na wakamuahidi watamlipa mwezi wa kumi ,baadae wa kumi na moja ,na sasa hiv ameambiwa watamlipa December lisha ya kuja dar kwenye ofisi zao ,imeniuma sana kwan mzee anaumwa ,then amechoma nauli kutoka kagera mpaka dar ,kwann pspf iendelee kumzungusha huyu mzee wakati ni hela zake yy mwenyewe ?

Hili linatufundisha nin tunaotegemea kujiajiri au kuajiriwa kuhusu PSPF? nawakirisha
Asante
 
Hayo majibu anapewa na Wasemaji wanaohusika na swala hilo? Na je wanamwambia tatizo ni nini hadi kupelekea kupigwa calendar muda wote huo?
Ninachofahamu kama amekamilisha utaratibu zote kabla ya kustaafu basi hata batch yake ya Malipo ipo kwenye Database na inafahimika kuwa ni lini check zao zinatolewa. Aidha Changamoto kubwa ni kuwa tunapokuwa na shida kwenye Taasisi hizo kuna kuwa na ugumu wa kuwaona wahusika mwishoe tunapewa majibu na wasiohusika!
 
Huu mfuko matangazo yao na huduma ni usiku na mchana!
 
Tatizo wanawekeza sana kwenye real estates business which involves major financing na no immediate return
 
Uhakiki wa umri haujaisha acha tuendelee kusoma sasa tutaanzA na za kirumi
 
Asubiri tumalize kujenga eapoti,veewonder,deni LA bom bar dia ndipo atalipwa.
 
Mifuko mingi inatatizo la Liquidity
Thus wana delay kulipa pensioners
Sababu kubwa ni kuwa serikali huwa na tabia ya kuchukua fedha huko ku finance shughuli zake bila kuzirudisha..
Mfano pesa za ujenzi wa UDOM sina hakika km serikali ilizirudisha..
So hapo mzee awe mpole tu...
Zitakuja kwa wakati wa bwana..
 
usilolijua kuhusu PSPF
utashangaa kulijua ndugu yangu.
Kama unanamba ya Mr Kijazi mbip akujuze
 
Aidha Changamoto kubwa ni kuwa tunapokuwa na shida kwenye Taasisi hizo kuna kuwa na ugumu wa kuwaona wahusika mwishoe tunapewa majibu na wasiohusika!


Na hili ndilo tatizo kubwa kwenye taasisi nyingi za umma, wameweka mfumo wa kupata majibu yote mapokezi ambako waliopo hapo hawajui chochote, hii ipo sana, sijui kwanini management inakwepa wajibu wake wa kuhakikisha wateja wanapata taarifa sahihi kutoka kwenye mifumo ya upatikanaji wa taarifa hizo.
 
Ni kweli kabisa mleta mada,hata mimi nina mtu wa karibu toka june mosi mpaka leo anasubiri malipo yake,kila akiuliza zone office eana wanamuahidi mwisho wwa mwezi.
Wazee wakimaliza utumishi hawathaminiki tena.
 
Mzee Wangu anestafu toka mwezi April mpaka Leo anaambiwa njoo kesho, mpaka amachoka
 
Back
Top Bottom