Majengo Mapya ya mahakama ni sawa na jeneza lenye maiti ndani, masheikh wamekaa miaka karibu kumi bila kesi zao kuisha

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,983
20,634
Jeneza nje hurembwa kwelikweli kwa nakshi na maua, ndivyo yalivyo majengo ya mahakama. Katikati ya majengo hayo mazuri, Kuna watu wamekaa rumande miaka karibu kumi, kesi zao haziishi, na mahakama ipo.

Naifananisha na jeneza kwa sababu ukilifungua lazima ukutane na harufu, maiti. Kwa mahakama, majengo hayo yameficha uzembe,uozo, uonevu, watu kuacha majukumu yao (abdication), kutumika kutakatisha uonevu (laundering impunity) kwa kuwa muoneaji atasema kesi iko mahakamani, yeye hahusiki na uonevu.

Haya yanatokea mahakama ikiwa inasimamiwa na profesa. Yuko bize kujenga majengo, ameachana na jukumu la msingi la utoaji haki. Wakati wa Nyerere, kesi za uhaini zilifanyika katika mahakama za kawaida kabisa lakini ziliisha ndani ya mwaka, Leo katika Dunia ya teknolojia, zinachukua miaka kumi.

Mahakama Ina case management system, Jaji Mkuu anapata daily report ya Kila mahakama nchini, mbona hazifanyii kazi?

Prof Juma alipata Hela za kununulia suti makarani wake na mahakimu nchi nzima, lakini amekosa Hela za kuwatoa mahabusu masheikh na kuwapangia majaji, wasikilize kesi zao hata kwa mwezi mzima

#ProfJumaMustgo
 
Kila akisikika anaongea maboresho ya mahakama huwa ni majengo tu
 
Back
Top Bottom