Protokali: Ni makosa Mkuu wa Wilaya kukaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa!

Hapa mtoa hoja tungekuwa pamoja kama ungetupa na vifungu vya kanuni. Hivi ilivyokaa imekaa kimtazamo wako, inawezekana pia kuwa wewe ndio umekosea
 
Awamu hii wajuvi mpo wengi sana.Tuoneshe taratibu au kifungu kipi kimekiukwa
Tangu enzi za Makamba,kuna wakati Athumani Mdoe alikuwa anakaimu,kuna haja gani kumtoa mkuu wa mkoa fulani aje kukaimu,kule alikotoka nani atakaimu.Tumia akili dada,sio kila kitu unapinga kuhalalisha hiyo laptop ya bure uliopewa
Mkuu mi ni male,
and I am an insider, I know what I have written unakumbua rc mecky sadick alivyokuwa kaimu mkuu wa mkoa wa dsm wakati akiwa mkuu wa mkoa wa lindi?
Hivyo ndivyo inatakiwa kuwa. Nawashauri waandishi wa Habari mnaopita Huku muulizeni eng musa iyombe aeleze Kwa nini ameruhusu suala hili msikie atakavyojiumauma
 
Kwa Mara nyingine nashangaa ukiukwaji mkubwa za taratibu za kiutawala na kiongozi ambazo tumejiwekea.

Kiutaratibu ambao Upo na unaeleweka na ofisini ya rais tamisemi, nafasi ya mkuu wa Mkoa inapokuwa wazi inatakiwa ikaimiwe na mkuu wa mkoa, wa jirani na Sio mkuu wa wilaya.

TAMISEMI mmeamua kweli kuruhusu huu ukiukwaji wa taratibu uliofanyika kwenye sekretarieti ya Mkoa wa Dar es salaam Kwa nafasi ya mkuu wa Mkoa kukaimiwa na mkuu wa wilaya.

TAMISEMI Taratibu zinajulikana, kwa suala lolote lile mkuu wa mkoa anaomba ruhusa kwenu, na nyie ndio mnawaruhusu au kuwakatalia, na ofisini yenu ndio inatakiwa kuteua mkuu wa mkoa wa kukaimu nafasi hiyo. Kwani mnafahamu kwamba ipo wazi.

Na inajulikana wazi instruments za mkuu wa mkoa ni tofauti na instruments mkuu wa wilaya.

Taratibu hazikubali kwa DC kukaimu u RC au DAS kukaimu UDC, mapungufu Haya yapo nayashuhudia kwenye vyombo vya habari DC ni Naomi RC, na DAS kaimu DC
TAMISEMI wajibikeni. Simamieni miongozo

Ila I am sad to you,that you have been put under the him self
Kwanza nafasi ya mkuu wa mkoa c ya kiutendaji ni kama mwenyekiti as long wamekubaliana sawa! its minor issue! mkuu!
 
Mkuu mi ni male,
and I am an insider, I know what I have written unakumbua rc mecky sadick alivyokuwa kaimu mkuu wa mkoa wa dsm wakati akiwa mkuu wa mkoa wa lindi?
Hivyo ndivyo inatakiwa kuwa. Nawashauri waandishi wa Habari mnaopita Huku muulizeni eng musa iyombe aeleze Kwa nini ameruhusu suala hili msikie atakavyojiumauma
Ule sasa ndio ulikuwa ni uharibifu wa Rasilimali watu.Na kule Lindi nani alikaimu nafasi ya Sadiki?Nioneshe ni sheria au kanuni ipi rasmi imevunjwa kwa Hapi kukaimu Dar kama wewe kweli ni insider
 
Hapa mtoa hoja tungekuwa pamoja kama ungetupa na vifungu vya kanuni. Hivi ilivyokaa imekaa kimtazamo wako, inawezekana pia kuwa wewe ndio umekosea
Mkuu waraka huo upo Kiutaratibu siwezi kuuweka hapa.
Yaani hata nafasi ya waziri kama hayupo itakaimiwa na waziri mwingine, manaibu waziri Sio wajumbe wa cabinet
 
tunaish kwa mazoea hyo ndio tanzania ........kama utaratibu uko hvyo bila shaka wanaufaham vyema kabsa
 
Ni kweli kabisa nakumbuka Mwantumu Mahiza alipokua RC Pwani aliwahi kukaimu sijui alikua RC nani yule
 
Awamu hii wajuvi mpo wengi sana.Tuoneshe taratibu au kifungu kipi kimekiukwa
Tangu enzi za Makamba,kuna wakati Athumani Mdoe alikuwa anakaimu,kuna haja gani kumtoa mkuu wa mkoa fulani aje kukaimu,kule alikotoka nani atakaimu.Tumia akili dada,sio kila kitu unapinga kuhalalisha hiyo laptop ya bure uliopewa

Mkuu:
Ni sawa unachokisema, lakini Instruments ni tofauti. Hata hivyo kuna wakati Mh. Said Meck Sadiki alikuwa RC Lindi na alikuwa anakaimu u-RC Dar.
 
Kuna madhara yoyote akikaimu mkuu wa wilaya??
Pia huwezi jua labda taratibu zimebadilishwa.
Kwa uzoefu wangu wa muda mrefu wa kufanya kazi kwenye sekretarieti za mikoa na tamisemi hizi nafasi za wakuu wa mikoa na ma dc hazina hazina faida kubwa kwanye jamii hivyo hata zikifutwa kabisa hakutatokea madhara yeyote. Ofisini zivunjwe watumishi waamishiwe halmashauri au wizarani, watumishi wa hospital I za mikoa warudishwe wizara ya afya.
 
  • Thanks
Reactions: RR
Mkuu asante kwa kukazia, wiki iliyopita nilikuja na uzi wa kwanini Hapi anakaimu nafasi ya Makonda. Nashukuru wengi walitoa mitazamo yao lakini pia wengi walinidhihaki. Kunawatu humu wanajifanya ni CCM 'die hards.' Hawatusaidii hata kidogo.
 
Nakumbuka said meck sadick alikaimu akiwa lindi, mwamtumu mahidha alikaimu akiwa pwani. Sasa ally happy imekuwaje tena.
 
Mkuu waraka huo upo Kiutaratibu siwezi kuuweka hapa.
Yaani hata nafasi ya waziri kama hayupo itakaimiwa na waziri mwingine, manaibu waziri Sio wajumbe wa cabinet
Hata kwa kutuambia tu, waraka namba gani wa mwaka gani tutautafuta tufanye reference.

Kwasababu kama ni kosa basi limefanywa kitambo kiasi kwamba imeonekana kama ndio utaratibu. Inawezekana waraka umesahaulika na hili swala la kushindikana kuwa public ndio hata huko kwenye maofisi hawauoni kufanya rejea
 
Mkuu:
Ni sawa unachokisema, lakini Instruments ni tofauti. Hata hivyo kuna wakati Mh. Said Meck Sadiki alikuwa RC Lindi na alikuwa anakaimu u-RC Dar.
Huko Lindi nani alikuwa anakaimu wakati yupo Dar?Hayo mambo ya kutumia vibaya rasilimali watu ndio yametufikisha hapa.
Ilibidi sadiki aje Dar kwa shangingi la RC Lindi,limsubiri siku zote na dereva alipwe posho pamoja na sadiki mwenyewe.Za nini hizo?
 
Back
Top Bottom