prosperity

prosperity

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
18,272
Reaction score
20,720
hivi kwann pale mtu anapokuwa yuko prosperous huwa idadi ya watu walioko nyuma yake inakuwa kubwa sana. Yaani utakuta marafiki, ndugu, wafanyakazi wake wapo karibu nae sana sana. ila sasa mtu huyu huyu akipatwa na majanga halafu mafanikio yake yakaanza kudrop basi watu wote hundoka nyuma yake.utakuta kama ni ndugu wanaanza kumtenga, marafiki wanamkimbia watumish nao hivyo hivyo je hii husababishwa na nini??

tena kuna wakati yule mtu mwenye mafanikio hata kama ni mchoyo, mringi bado watu watajikomba kwake tuuuuuu.
 
Dada siku zote:
Mti ulio na matunda ndio unaopopolewa sana.
Nijuavyo mimi kwa mtu aliyebarikiwa kwa mafanikio, idadi kubwa au ndogo ya wale wamtegemeaye, pia ni sehemu ya baraka.
 
makuuuuuuta mama!
kitu ya uchawi wa kizungu!
kitu ya karatasi yenye raaangi
kitu ya kuyaza mufuko fasi ya ku wallette
kitu ya kusafisha ile wanasema roho
ndyo vile wananjuagha watapata muteremko ku maisha ya kupeleka mukono kinywani!
makuuuta maaama!
 
Dada siku zote:
Mti ulio na matunda ndio unaopopolewa sana.
Nijuavyo mimi kwa mtu aliyebarikiwa kwa mafanikio, idadi kubwa au ndogo ya wale wamtegemeaye, pia ni sehemu ya baraka.

sawa ni baraka lkn sasa kwann ghafla ile hali ikitoweka watu huondoka?? je kwann wasiwe nyuma yako kama kwanza
 
fuata nyuki ule asali

sasa hata nyuki huwa wanahamaga mzinga, hivyo kubidi kuutundika upya mzinga.
kwann kwa binadamu huwa ni tofauti kabisa?? wewe zinga wako hauna asali basi raia wote hukuona kama mwenye mkosi na kukukimbia??
 
makuuuuuuta mama!
kitu ya uchawi wa kizungu!
kitu ya karatasi yenye raaangi
kitu ya kuyaza mufuko fasi ya ku wallette
kitu ya kusafisha ile wanasema roho
ndyo vile wananjuagha watapata muteremko ku maisha ya kupeleka mukono kinywani!
makuuuta maaama!

mwali lkn mbona basi ukiterereka hao wote waliokuwa nyuma yako huondoka??
 
sawa ni baraka lkn sasa kwann ghafla ile hali ikitoweka watu huondoka?? je kwann wasiwe nyuma yako kama kwanza

jibu rahisi ni kwa kuwa Baraka imeondoka..."Mzinga wenye asali ndio ulinwao"
 
Ni wanafki. Wapo nawe kwa ajili ya pesa zako tu.
Hivi nicas unajua kuna hata baadhi ya familia mzazi ama wazazi wanabagua watoto kulingana na kipato??
wengine wakiwa na vipato basi wazazi huona ndo injini zanyumba. yaani wakisema jambo hawapingwi, na hata wakikose hakuna kuna wa kuwaonya. umewah ona hii??

huu ni ujinga ama woga wa pesa za mtoto??
 
Last edited by a moderator:
Hata makanisani wenye pesa ndio wanapewa vipaumbele.
Ni kwa Mungu peke yake kuna fairness.

Na ndio maana tunashauriwa kwamba tukifanya sherehe tualike wasio jiweza ili wasitulipe ili Mungu atulipe; but what do we do?????........

It begins and ends with you, l am afraid.
Umelala kweli leo?
 
Watu wanapenda kusaidiwa ... Ila ukifulia maa yake utaanza omba ama tegemea msaada toka kwao... Pia yawezekana hawakuwa marafiki wa kweli kwako
 
Hivi nicas unajua kuna hata baadhi ya familia mzazi ama wazazi wanabagua watoto kulingana na kipato??
wengine wakiwa na vipato basi wazazi huona ndo injini zanyumba. yaani wakisema jambo hawapingwi, na hata wakikose hakuna kuna wa kuwaonya. umewah ona hii??

huu ni ujinga ama woga wa pesa za mtoto??

Yeyote asiyejali utu wa mwenzie amepungukiwa hekima.. Pesa imejenga classes kubwa sana kati ya watu..
 
Last edited by a moderator:
Hata makanisani wenye pesa ndio wanapewa vipaumbele.
Ni kwa Mungu peke yake kuna fairness.

Na ndio maana tunashauriwa kwamba tukifanya sherehe tualike wasio jiweza ili wasitulipe ili Mungu atulipe; but what do we do?????........

It begins and ends with you, l am afraid.
Umelala kweli leo?

Kaunga wewe ni supa sana.. Do you know that?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom