Property tax | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Property tax

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Magpie, May 18, 2010.

 1. Magpie

  Magpie Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wanajamii naombeni msaada, kuhusu Tax Law hasa kwenye ishu ya property, je ni kweli kwamba mstaafu
  kwa hapa tanzania yupo exempted kulipa kodi kwa mapato yatokanayo na rent ya nyumba yake aliyopangisha ?
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kwanza naona kama vile unachanganya vitu viwili hapo, income tax (kodi ya mapato) na property tax (kodi ya majengo) ni kodi mbili tofauti na zinaongozwa na sheria mbili tofauti. Property tax inakusanywa na local govts (kwa sasa wamewapa hiyo kazi TRA kwa DSM) na Income tax inakusanywa na TRA kwa ajili ya central govt. Either way, wastaafu hawapo exempted (chukulia kwa mfano mstaafu ana nyumba arobaini za kupangisha....kweli asamehewe kodi kwa sababu tu ni mstaafu!?).
   
 3. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sheria ya inayosimamia property tax kwa Tanzania inaitwa Urban Authorities (Rating) Act 1983. Sheria hii haijatoa tax relief yoyote kwa mstaafu.
   
 4. consigliori

  consigliori JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu SMU, hizi rent tunazozilipa kwa wenye nyumba wetu uswahilini zinatakiwa zitozwe kodi kwa utaratibu gani? Manake naona kama serikali haikusanyi kodi huku uswahilini kwetu.
   
 5. Magpie

  Magpie Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashukuru wadau..kwa muongozo wenu...Viva jamiiforums...!!!!
   
 6. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,937
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Mbali na kodi ya majengo (property tax), pia kuna kodi nyingine inaitwa kodi ya pango la ardhi (land rent). Kodi hii hutozwa kwa viwanja ambavyo vimepimwa na kuandaliwa hati ya kiwanja. Inaitwa kodi ya pango la ardhi kwa sababu Sheria yetu (Na. 4) ya Ardhi ya mwaka 1999 sehemu ya 4 (Land Act No. 4 of 1999, section 4) inasema ardhi yote ni mali ya umma na amepewa rais kama mdhamini. kwa hiyo mtu mmoja mmoja anapopata ardhi ni kwamba anapangishwa kwa kipindi cha miaka 33, 66 au 99. na kwa kipindi chote hicho mtu aliyepewa ardhi atatakiwa kulipa kodi ya pango la ardhi pamoja na kutimiza masharti mengine ya umiliki.

  Kodi hii hukusanywa na halmashauri kama wakala wa wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi (serikali kuu) kwani hupewa asilimia fulani ya makusanyo ambayo yamepatikana.

  Wasalaam.
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kama anaelipa kodi hiyo akiwa kampuni, wakati wa kulipa anatakiwa akate asilimia 10% na kuipeleka TRA. Otherwise, sheria ya kodi inamtaka kila mtanzania (resident) kulipa kodi ya mapato kwa mapato yote anayoyapata iwe kwenye biashara, uwekezaji au ajira. Hili la pili kwa hapa kwetu bado ni ndoto na watu wengi hawalipi(kwa kujua au kutojua) kodi ya mapato inavyostahili. Kama system ingekuwa inafanya kazi vizuri hjao wa wenye nyumba uswahilini unaosema wanatakiwa kulipa kodi wenyewe TRA (self assessment system). Kwa sababu hakuna utaratabu mzuri (ingawa sheria iliyopo ni nzuri tu), watu wachache wanaolipa kodi ndio hao hao TRA inawang'ang'ania.
   
Loading...