Propaganda za uongo: Elimu bure, CHADEMA ikishinda


Jamani hebu tuzungumze NAMBA. Hivi mlitarajia sh ngapi zitoke makao makuu kwenda Kilimanjaro ikiwa kama CHADEMA INGESJHINDA. Kweli mlijianda kwa Namba kamili au mlifanya mahesabu ya nchi nzima tu. Sasa mnachoficha ni nini? Hatutawazonga tunahitaji Tzsh za elimu Kilimanjaro.
 
Kuna umuhimu wa kuweka vigezo vya kupost thread hasa jukwaa la siasa.Mtoa mada hajui ata nini maana ya propaganda,kuna watu mfano kwenye cha ya nyinyiem anaitwa kiongozi wa PROPAGANDA NA UWENEZI SERA sijui kama unajua ilo.!
 

Usemayo ni kweli na sikweli. Kuwa huko Zaire mikataba ilivunjwa ni kweli lakini unachoshindwa kuelewa ni kuwa wakati unafanya hivyo uko mgongoni kwa nani. Kwa mfano Libya leo mikataba yote inaweza kuvunjwa kwa masaa tu. Kwa sababu nia ya vita vyenyewe ilikuwa ni kugeuza mikataba toka kundi 'A' kwenda kundi 'B'. Unajua kesi ya fisi........

Lakini kwa suala la Tanzania ni gumu kwa vile mwenye mikataba ndiye mwenye Mahakama ya kimataifa....... Uganda iliwalipa wahindi wote mali yao... Wakati watu kibao duniani wamedhurumiwa ardhi zao na mali zao hutasikia wanalipwa.

Hii dunia imekaa kivyake vyake ndugu yangu, wala haina haki. Hayo ninayokwambia ndio majibu JK aliyopewa na Uingereza, Canada na Marekani. Sasa wewe sisi mizi utafanya nini.
 
Topical hajui lolote zaidi ya uongo unaoenezwa na mihadhara ya wahuni pale manzese na magomeni kuwa "CHADEMA ni mfumo Kristo"
 
Nenda kaulize kwanini Kenya Elimu bure inawezekana wana nini zaidi yetu.
 
Wewe mbaguzi wa rangi uliekosa adabu, rudi kwenye tuhuma zako za kibaguzi kwamba "waafrika hawajui uchumi". Wala usinilazimishe kusoma thread na unachoita hoja zako, kwani huna hoja zaidi ya "naive arrogance" inayotokana na ushabiki wako wa kisiasa pia ufinyu wako wa kuchambua uchumi.
 

Haya mimi nina ufinyu wa kuchambua uchumi. Sasa wewe mpevu wa Uchumi niporomoshee mambo ili niyakubali. Nafahamu fika kuwa uchumi unaujua lakini hebu waonyesha wana JF hapa uwanjani.
 
Haya mimi nina ufinyu wa kuchambua uchumi. Sasa wewe mpevu wa Uchumi niporomoshee mambo ili niyakubali. Nafahamu fika kuwa uchumi unaujua lakini hebu waonyesha wana JF hapa uwanjani.
Futa kauli yako kwamba "waafrika hawajui uchumi".
 
Futa kauli yako kwamba "waafrika hawajui uchumi".

Wewe hakikisha hapa kuwa unaujua uchumi, kwani tabu iko wapi. Usije tu ukanionyesha B. COM YAKO sihitaji nahitaji maandishi hapa. Kama huwezi si ukubali tu. Au nimekupa misifa ya bure wakati uchumi huujui.
 
Wewe hakikisha hapa kuwa unaujua uchumi, kwani tabu iko wapi. Usije tu ukanionyesha B. COM YAKO sihitaji nahitaji maandishi hapa. Kama huwezi si ukubali tu. Au nimekupa misifa ya bure wakati uchumi huujui.
Your naive academic arrogance signifies your doom. Goodbye!
 
Katika hilo lakutoa elimu bure nakuunga mkono mtoa mada,cdm walilisema sana ktk kampeni huku wakijua ni uongo hawawezi,hata yule mbunge wa ilemela aliwadanganya watu kua elimu itakua bure na michango yashule itakua marufuku akichaguliwa kuwa mbunge,matokeo yake sasa michango imezidi na hakuna cha elimu bure,wapiga kura wa ilemela wakamfata nyumbanikwake kumuuliza mbunge wao kulikoni iwapi elimuyabure?mbona tunachangishwa michango kamakawaida?aliwatimua akafoka akawambia hapa hakuna ofisi yamalalamiko ondokeni,sasa anakesi yakupigwa ubungewake watu wa ilemela wanaomba ubungewake utenguliwe uchaguzi urudiwe wameapa hawampi kura,wanajuta kumchagua mtu aliewadanga na ambae ni fedhuli,akumbuke kilichomuangusha masha ubunge atapata jibu.
 
Your naive academic arrogance signifies your doom. Goodbye!

Lala salama, lakini ni lazima utaota maneno yangu maana ukweli hukaa kichwani muda mrefu na hujirudia usingizini ama ukipenda unawea kuuita NDOTO.
 


Watajuta kuwachagua wengi wanaowadanganya. Lakini yote 9 kumi ni hili la Mh Slaa, si kwamba tutajuta bali IKULU HAIONI KABISAAAAA.
 
Wewe kweli ni mbwiga, kwani mpaka leo hujui ni chama gani kinaunda serikali na kutekeleza sera zake? Sio lazima uchangie humu hata kama huna chakuchangia kwani hakuna atakaye kulaumu kwa kuto kuchangia.
Kwani unajua hukumu yakesi ya kupinga matokeo itakuwaje mpaka uanze kutabili uchaguzi utakuwaje? wewe na mtoa thread wote wachovu waakili.
 

kama mimi mbwiga basi wewe *****,umepitiwa naule usemi usemao ukipenda ukiona chongo utaita kengeza,huyo mbunge aliedanganya watu wa ilemela wakampa kura hata akimaliza huo mudawake wamiaka5 hawezi hata kurudi kugombea tena amelikoroga na atalinywa,na ushahidi upo wa mikanda yavideo alivyowatukana watu waliomfata kumuuliza kuhusu ahadi ya elimu bure,pia kuna ushahidi wa cd wakati wa uchaguzi alivyowadanganya watu mambo mengisana hata aliahidi kuwapelekea maji wale waliokua hawana leo hata kupita jimboni anaona aibu,akipata tena kura ilemela hata masha atakua tena mbunge wa nyamagana,nazani huwajui watu wa mwanza unawasikia tu.
 
Bwana mkubwa siyo kwamba napingana na sera ya elimu bure ila naomba tu niongezee facts zako kwamba sera ya CDM pia inasema watakuja na utawala wa kimajimbo which means jimbo la Kaskazini litajiendesha kwa mapato yake pekee. Hata mimi nina wasiwasi kuwa CDM watakuwa wanajutia hiyo ilani, is quite impossible.
 
Ilani ya CDM hai reflect bajeti zao walizotoa bungeni, pia hotuba zao kwa wananchi.
 
Usidhani watu wa Mwanza ni limbukeni kama wewe, na hii inaonyesha jinsi gani hujui hata kazi za mbunge nini, pili mbunge sio sultani kwamba kila kipindi lazima achaguliwe yeye tu, hizo ni fikra duni za wachovu kama wewe. Wananchi wana haki ya kubadirisha uongozi kadri wanavyotaka. Aliye kuambia mbunge aliyepo sasa lazima agombee tena ninani?
 

Jambo moja linalonihuzunisha kutoka kwa mtoa maada ni kutojua chanzo cha tatizo linalotupelekea kushindwa kulipia gharama za elimu. Mtatizo haya yote ya mikataba ya madini na ufisadi mwingine umeletwa na ccm. Na hata kama Jk amejaribu kuivunja akashindwa ni kwa sababu ya masilahi ya kundi lililo ndani ya ccm!

Kama vile bado hawajajifunza wamekwenda tena kuwekeana saini mikataba ya kuuza ardhi huko Marekani, ili vizazi vijavyo vishindwe kujitoa ktk ukoloni huu mpya unaoletwa na ccm.

Suala sio kugharamia elimu kutoka ktk vyanzo gani? Bali ni kuvunja kabisa mfumo mbovu uliopo wa kukusanya kidogo na kutumia sana na kuweka mfumo wenye mizania kati ya matumizi na mapato na kisha kuchagua vipaumbele vya matumizi.

Haiwezekani ukawawekea CDM ukusanyaji mapato mbovu uliopo ili wapange matumizi sawasawa na vipaumbele vyao! Hizo takwimu ulizotoa ni kutokana na usimamizi mbovu wa mapato uliopo ambao kwa vyovyote hauwezi kutoa elimu bure!
 
alieniambia atagombea tena ni yeye mwenyewe kwa kauliyake aliitoa ktk mkutano wa hadhara pale viwanja vya sahara,ila kwa sasa hata wazo la kugombea atakua hanatena maana watu wa ilemela wameshamwambia uso na macho au wazungu wanasema live kuwa hata uchaguzi ufanyike kesho bora wachague ng'ombe kuliko kumchagua mtu muongo anaewatukana wapigakurawake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…