Propaganda za CCM kumpa chati Dr. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Propaganda za CCM kumpa chati Dr. Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mozze, Sep 7, 2010.

 1. m

  mozze Senior Member

  #1
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja za maisha binafsi ambazo ni dhahiri zimepikwa na CCM, Makamba ndio alianzisha, akafuatwa na makada wengine, zitaijenga Chadema na mgombea wake wa urais. Kwa nini hizi hoja zitajenga badala ya kubomoa.
  Zimekuja mapema sana na muda upo wa kutosha watu kujadili na kasha kuzipuuzia. Kwani zaidi ya kusema mtu kachukua mke wa mtu kuna lipi jipya watakalosema tena kuonyesha mabaya ya Dr. Slaa?
  Sababu huyo aliyekuwa Mume ndio kajitokeza baada ya CCM kuanzisha hizi hoja, na kwa sababu kuna ushahidi kuwa Mkewe alishaondoka nyumbani hata kabla ya kukutana na Dr. Dlaa, jamii ya watu wenye uelewa watawapuuza CCM na kuwapunguzia umashuhuri wao kwa kuwa wataonekana wanawanyanyasa wananchi wao kwa kuangalia maisha binafsi. Wasomi na watu wenye uelewa zaidi ni dhahiri wataona CCM ni chama cha wahuni na kisichofaa kuongoza nchi kwa kuweka mbele UDAKU kuliko ukweli.
  Jamii ilitegemea CCM ijibu shutuma mbalimbali zikiwemo za ufujaji madaraka, RUSHWA, udini, ukabila na upendeleo kwa watoto wa viongozi; lakini hawajaweza kujibu, hata kwa kukanusha au kukubali, na badala yake wameanzisha mjadala wa maisha ya Dr. Slaa. Wapiga kura wataamini shutuma dhidi ya CCM ni za kweli mana Dr. Slaa alishajieleza kuhusu maisha yake binafsi na bila shaka wananchi wameshajua ukweli.
  Ni wazi CCM itakosa kura za watu wasiopenda mambo ya kuingilia maisha binafsi kwa kuwa hawatafurahia hilo. Ukitaka kujua kuwa watu wengi hawapendi maisha kuingilia maisha binafsi fuatilia kwa week Magazeti ya Udaku wanauza kopi ngapi? Halafu ulinganishe na magazeti makini kama Mwananchi. Hivyo hii issue itakuwa na faida kwa Dr. Slaa.
  Kwa kuchapisha, tena kwenye ukurasa wa mbele, masuala ya Dr. Slaa, CCM inamuongezea umashuhuri kwa kuwa watu watapenda kujua huyu ni nani na ni kwanini anashambuliwa sana. Siku zote inatokea mnyonge kupendwa na watu wengi, na CCM hapa wamekosea step.
  Kumpeleka mahakani mume wa zamani kudai fidia ya 1bn ni kuongeza elimu kwa wapiga kura kuwa CCM na wana propaganda wake wanazusha mambo. Hii itadhihirika pale mlalamikaji atakaposhindwa case na jamii ya kitanzania itajenga uaminifu zaidi kwa Dr. Slaa na kuidharau CCM.
  CCM inapoteza nguvu na mali nyingi kutumia magazeti na njia nyingine kumchafua mtu kwa issue binafsi, wangeweka hizo nguvu kuwavutia watu kwa sera ingefaa zaidi kuliko kuwaelimisha watu na kuwafanya wamjue vizuri Dr. Slaa. Siku zote binadamu humfuata mtu wanayemjua kiundani, yote mapungufu na mazuri yake.
  Kumebaki zaidi ya mwezi na nusu kufufikia uchaguzi, hii STORY ya CCM juu ya maisha ya Dr. Slaa itaisha tu ndani ya week chache zijazo, CCM watakauwa na lipi? Itakuwa ni zamu yao sasa kutakiwa kujibu shutuma za Ufisadi na ubadhirifu katika uongozi na mambo ya ahadi zisizotimilika.
  Mwisho Namwonea huruma huyo Mume wake wa Zamani mana kaingia mkenge. CCM watamtumia tu wakati wa kampeni na zitakapoisha atajijua mwenyewe. Kama atakuwa na kesi mahakamani itabidi ajilipie gharama, na aibu nyingine zitakuwa juu yake. Watu wanajiuliza Tangu Dr. Slaa aweke hadharani mahusiano yake na huyu bibi alikuwa wapi? Tulitegemea siku ile ile angelalamika. Sasa kakubali kutumika kisiasa atayaona matokeo yake baada ya 31 Oct. Na kuna siku ukweli utawekwa hadharani hapo ndio itakuwa mwisho.
   
 2. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  True...
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ndefu lakini safi kweli kweli.well done mozze
   
 4. A

  Awo JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 793
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Hata mimi nimeacha kusoma magazeti ya Daily News na kuangalia taarifa za habari za Channel Ten na TBC 1. Hakuna chochote cha maana isipokuwa ahadi za Kikwete na ndoa ya Dr Slaa! What a shame! Waandishi wa habari na watangazaji wametuangusha jumla.
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Cheap journalist can easily be bought!
  Kuangalia news TV za Tz kWA sasa ni kheri nispend time CNN,SKYNEWS then narudi JF siku imeisha
   
 6. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mozze, safi sana! uko smart mkuu. Cha msingi hapa CCM wanajaribu kukwepa tuhuma au kuhamisha tension za watu kutoka kwao kwenda kwa Dr Slaa za kuhusu ufisadi, ubadhirifu wa mali, matumizi mabaya ya madaraka. Hakika HATUDANGANYIKI!

  CCM kama watuhumiwa wa wizi, inabidi watumie muda wao vizuri kutuhabarisha wananchi ni nini walichkuwa wakifanya kujibu hizo tuhuma. Kama watatueleza vizuri nasisi tukakubaliana nao, tutawapa kura. Lakini siyo kwa mizengwe wanayofanya. Itawajutisha bure. Mimi naamini katika ushindi wowote, lazima kuwepo na mambo magumu kama haya, mojawapo ni kama hili la tuhuma ya Dr Slaa kuiba mke. Dr Slaa akiipangua tu, basi ndo rais wetu october. Nachoomba, Dr ajipange vilivyo aje amalize kabisa kazi. wabaki kusubiri keko tu.
   
 7. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Inabidi CHADEMA wapate mtu ambaye hagombei wa ku-counter hizi tuhuma na kuzipenyeza kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari.

  UFISADI ni mojawapo ya mambo ambayo yanaitesa serikali ya CCM na akipatikana mtu kama Marando, Baregu (ingawa sina uhakika kama huyu anaweza bifu za akina Makamba). Marando nadhani anafaa zaidi kupewa kazi ya propaganda wakati huu wa kampeni ili apambane na propaganda za akina Makamba, RA, Kinana n.k. Bila kuwepo alternative news za CCM attention yote itahamia kwa Slaa na Chadema.
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160

  Asante Mdau kufafanua kwa undani, mimi nitaongelea zaidi juu ya huyu Mwanaume naomba ajibu yafuatayo
  1. Mke wake aliondoka nyumbani kwake lini?
  2. Je baada ya kupotea mke wake masaa zaidi ya 24 alichukua hatua gani?
  3. Vikao vingapi vya usuruhishi vya kifamilia vilikaa na maamuzi yalikuwa yapi?
  4. Jee ni nini chanzo cha mkewe kuondoka nyumbani?

  Mwanaume huyo ni mjinga yeye kadanganywa na kina Makamba na wanakurupukia mahamani, mambo ya ndoa ni ya kifamilia zaidi, mahakama lazima ipitie vikao vyote na maamuzi yaliyochukuliwa katika ngazi ya familia.
  Masuala ya ndoa yanahusishwa familia mbili wakuu sasa yeye anafikiri CCM itamlinda baada ya kufungua kesi hiyo matokeo yake atakuwa kajijengea maadui wengi zaidi ndani ya familia na jamii kwa ujumla, labda ahamie nyumbani kwa Makamba.

  Namlaumu huyu jamaa kwa kudanganywa na CCM (MAKAMBA), kwa kufikiri Makamba atamsaidia, amejitafutia matatizo makubwa mno, akiwa na aklli afute kesi hiyo mapema warudi kwenye vikao vya kifamilia, wayamalize.

  Na hao wanasheria Uchara na njaa zao hawajui kwamba maamuzi ya vikao vya kifamilia pia yanatambulika kisheria, kama mtu hatii au kutekeleza wajibu wake kwenye doa lazima abaki na vyeti tu, kufunga ndoa ya kikristo siyo msalaba hadi milele mtu ana uhuru wa kuamua maisha yake pia kama hiyo ndoa imeshindikana. Midume mingi huwa haitoi taraka kukomoa wanawake kwa kisingizio kuwa " Mimi huwa naoa tu kuacha sijui"

  Dr Slaa nakuomba uendelee na kampeni zako, haya yote we mwachie Ma Msapu na wanafamilia watamalizana na huyu mwanaume na hao wanasheria wa makamba.

  Pia waandishi wa habari acheki udaku, magazeti yote yanaandika story hii ki udaku udaku zaidi, mtanzania ndiyo kabisaa wanafurahia wakati hawajui hii si habari ya tija kwa wananchi -

  Wananchi wanataka kujua ufumbuzi wa matatizo yao siyo DR Slaa leo kala nini, kavaa nini, ameoga / hajaoga, ameongea na nani - all those are craps - tuangalie vitu vya msingi na nyie waandishi ndiyo watu wa kutupatia dira.

  Mbona hamuongelei ahadi hewa za Jakaya? ngapi alizotoa 2010 kazitimiza? na sasa anaongeza zingine?
   
 9. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CCM Unajua wanaishi karne iliyopita
  CCM wanafikiri magazeti ni muhimu sana kama zamani
  CCM wanafikiri hii mitandao ya simu iko mjini tu
  Kwa taarifa yao.....MWAKA HUU HADUDANGANYIKI
  Na tutapiga simu mpaka vijijini kuongea na ndugu zetu
  Kwamba huu ni uzushi TU.....
   
 10. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Gadafi kasema waafrika hatuna akili.inamaanisha watanzania pia.
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Salute mkuu, nimipenda hii!
   
 12. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "wataonekana wanawanyanyasa wananchi wao kwa kuangalia maisha binafsi".

  This theory is intact: The way people discusses other people's issues to you , is the same way happening to discuss with others your issues when you are not arround. CCM wameshayaongelea haya kwenye vikao vyao kwamba huyu tummalize ki-hivi.
  NOSENSE.
  CCM inawaangalia namna ya kuwanyanyasa watu wake na kuwadhulumu, kama ulivyoeleza hapo juu ufisadi umewashinda.
   
 13. The Good

  The Good Senior Member

  #13
  Sep 7, 2010
  Joined: May 26, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wakuu hii ndiyo siasa. Siasa ni mfumo maalum ambao una taratibu zake. kwa jina jingine siasa ni mchezo ambao mechi yake kubwa ni uchaguzi. kwa hiyo kama mchezo mwingine ili ushinde mechi inabidi mbali ya maandalizi pia utafute mbinu za kumvuruga mpinzani wako kisaikolojia. Hiki ndicho wanachofanya CCM kwa sasa.

  Kama mtakumbuka 2008 wakati wa kampeni za Urais Amerika, Republican walijaribu kumuhusisha Obama na mambo mengi ili kumvuruga kisaikolojia lakini pia kutafuta kura za wale wanaoweza kushawishika na mambo kama hayo ambao kwa kweli wapo.

  Obama alipigwa vijembe kuhusiana na asili yake kama mkenya, mwislam wa Somalia, Obama/Osama, mchungaji wake nk. Kwa upande wake Obama alijikita kwenye sera na hatimaye alishinda.

  Inawezekana Obama hakutingishika kwa kuwa nyingi ya hizi tuhuma zilikuwa za kupikwa. Kwa Dr Slaa kwa upande wake ni vizuri akaendelea na kumwaga sera.

  Tatizo ninalo liona ni jinsi gani Dr Slaa atajitenga moja kwa moja na kashfa hii mbali ya ukweli kuwa huyu bwana (Anayesemekena mume halali) anaonekana naye kutumika zaidi na wapinzani wa Chadema. Ugumu unakuja kama huyu bwana na Josephine wana ndoa halali ambayo haijavunjwa (Ingawa ndoa za kanisani tunaambiwa hazivunjiki) basi Dr Slaa kumnadi mbele ya watu kama ni mwenza wake kuna walakin. Hakukuwa na haja ya yeye kujinadi mbele ya watu. Na hapo naona Dr Sla amenasa katika mtego wa CCM. Walichofanya CCM ni kumvuta na kumbana kwa hoja dhaifu. Naye akaingia mtegoni mpaka akamnadani huyo bibie mbele za watu. Nadhani CCM wanafurahia hili kwa sasa.

  Ni muhimu sasa washauri wake wakamtahadharisha na mitego kama hii ambayo bado itakuja mingine maana hii ndiyo siasa. Ajikite kwenye sera kama Obama kinyume chake atawapa nafasi wapinzani kumvuruga kisaikolojia. maana hii ndiyo mbinu mojawapo ya siasa kama ilivyo katika mpira (Mourinho style).
   
 14. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hakika, na watu kama Michuzi wanajipunguzia umaarufu wao kwa kuweka habari hizo za udaku kwenye blog zao:

  MICHUZI

  Mume aeleza alivyoporwa mke na Dk. Slaa
  [​IMG] Bw. Amaniel Mahimbo

  “NAKUACHIA kibanda chako, nakwenda kwenye nyumba yangu.”

  Hayo yalikuwa maneno ya mwisho ambayo Aminiel Mahimbo aliambiwa na mkewe, Josephine Mushumbusi siku alipoachwa na mkewe huyo aliyeamua kwenda kwa mgombea wa urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa.

  Mahimbo ambaye ni mume halali wa Josephine, (kwa ndoa ya kanisani) alisema anakumbuka kuwa ilikuwa Machi mwaka huu na hakujua mke wake alipokuwa akienda na wala hakuhisi dalili yoyote ya kuwepo kwa mwanamume mwingine katika ndoa yao mpaka siku mwanawe wa kwanza Upendo (7) alipomwambia “baba tunaishi na daddy”.

  Akisimulia kisa hicho kilichoanza takribani miezi saba iliyopita, katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, Mahimbo ambaye ndoa yake ilifungwa Agosti 16, 2002 na Mchungaji Lewis Hiza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, alisema hakujua kama huyo ‘daddy’, ni Dk. Slaa mpaka siku moja alipoambiwa na mama mkwe wake.


  Chanzo na Habari Kamili Nenda Habari Leo
  BOFYA HAPA

  ANGALIZO: MAWAKILI WA BW. MAHIMBO INASEMEKANA WATAFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU KUHUSIANA NA UTATA HUU. TUTAWALETEA HABARI ZAIDI KADI ZITAVYOPATIKANA

  © Michuzi | Tuesday, September 07, 2010[​IMG][​IMG] | Permalink | Mtumie Rafiki Yako |


  Maoni: 0
   
 15. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi lipi la kupewa kipaumbele kwa maslahi ya Taifa? Wizi wa EPA, Deep Green na Radar au ukwapuaji wa "mke" wa mtu? CCM is using diversionary tactics. Wajinga ndio waliwao!
   
 16. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,387
  Likes Received: 3,142
  Trophy Points: 280
  yaani unaangalia tbc na channel ten?......................angalia mlimani tv ndiyo wakweli........channel ten madrasa tu.............
   
 17. F

  Froida JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kuona mwanaume mzembe kama huyu hata kama anataka kumchafulia Dr. S laa au hajaridhika na mahusiano kati ya Josephine na Slaa, amechelewa sana kwani ukweli angeweka wazi siku ya kwanza tuu alipotangwazwa basi, pia angetuambia jitihada zake kama alizifanya kumtafuta mkewe,kama ndugu waliambiwa,walisemaje ,mke alisemaje,hadithi kwenye gazeti na maneno yake kwenye luninga inaonekana hakukuwa na mawasiliano kabisa,lazima kuna sababu ambayo anaficha.
  Jamii ya Tanzania hawaoni kosa lolote la Dr Slaa,wengi tumeamini ni mchezo mchafu wa CCM waliouandaa mahsusi ukioongozwa na MAKAMBA kwa sababu makamba nchii anaonekana ni Debe tupu,nadhani hii propaganda imeanguka mweleka wa pwaaaaaaaaaaaaaaa,hakuna jipya

  DR.SLAA asijibu kabisa habari hizi amwachie josephine na familia yake wajibu lakini kama kesi itapelekwa mahakamani basi nadhani hapo ndio ngoma nzuri inapokuja itakuwa hatuzungumziii swala liliko mahakamani,huku akiendelea kumwaga sela ambazo kwa kweli sasa hivi imekuwa mwiba kwa CCM.
  Prof. Lipumba alizushiwa hayo hayo na mkewe Georgina mwaka 2000 ,hata mapicha yakawekwa wakimuita Kimada mpaka leo wako wote sidhani safari hii kama itafanya kazi hiyo propaganda
   
 18. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  I doubt kama wataipeleka mahakamani kwa sababu wanajua ikishatua huko hawatakuwa na la kuongelea.Huyu jamaa anaonyesha bayana ni chapombe.Ama kweli Kikwete na mtandao wake ni mafioso.Yani hata aibu hawaoni!
   
 19. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  MICHUZI+JeyKei (banned but now with a new name)+Habari Leo=MAFISADI
   
 20. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwa vile wewe unaokota makopo basi kila mtu atafuata mkumbo wako?Hajaanza kuokota makopo Tambwe Hizza aliyeapa hadharani kuwa akijiunga na CCM basi analala na mama yake itakuwa Dkt Slaa?
   
Loading...