Kama tarehe ya clip hiyo ni Desemba 28, 2012, Nchemba alidai kuwa nayo Januari Mosi au Pili 2013. Ukitazama sawasawa tarehe hizo utagundua kitu. Ni tofauti ya siku nne au tano tu. CCM imefilisika mikakati ya propaganda kiasi kwamba sasa wanafanya mambo ambayo hawadhani kuwa wapo wenye akili na uelewa zaidi yao. Kwa hiyo walikaa nayo wakisubiri wakati ambao wao walidhani ni muafaka. Kwa hiyo walipomteka Kibanda ndipo wakaanza kusemasema. Akaanza Ridhiwani akikejeli: "Na hii nayo mtasema ni RAMA?" Kina Nape naye akapokea kijiti na kuliendeleza.
Wakaandaa mazingira ya kutaka kuwafanya Watanzania wababaike. Wakaanza kuhusisha tukio la kutekwa Kibanda na Mbowe na kisha Chadema. Kwa kuwa walikuwa wamejiandaa, ndipo ghafla Bukoba Boy akazuka Machi 13, akafungua akaunti na siku hiyo hiyo akatumbukiza clip hiyo. Punde tu habari zikasambaa kwa kuwa walikuwa wamejiandaa. Na haraka sana polisi, ambayo iliwahi kusema haifanyi kazi kwa mitandao ya kijamii, sasa ikala matapishi yake. Ikaanza kufanya kazi kwa mitandao ya kijamii. CCM Wamefilisika. Watafute njia nyingine ya kuwadanganya Watanzania.