Project ya UDART imeshakufa

Project ya UDART imeshakufa

chinatown

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
1,232
Reaction score
1,107
Naiangalia project ya UDART kwa jicho la tatu naona inakufa. Pamoja na support kubwa ya Serikali bado hawa jamaa (management ) wameshindwa kujiongeza kabisaa.

Imagine if were you unaondolewa washindani wako katika biashara unabaki peke yako halafu unashindwa kufanya huduma unategemea nini?

Wateja ( pamoja na mimi) wanalalamika kukaa muda mrefu vituoni lakini utawala hauna ufumbuzi.

Wametoa namba za customer care hazipokelewi kabisa(nadhani kwenye hili wanamridhisha mheshimiwa kama vile wafanyabiashara wanavyobandika siku ya TRA kuwa yeye analipa kodi while not)

Hawa jamaa hawajui;
1. Muda gani ni peak/rush hours magari yawepo barabarani
2. Madereva kuanza kazi muda tofauti tofauti kutasaidia kumaliza kazi muda tofauti
3. Hawapo systematic katika kuyaondoa magari kwenye main port zao yanaweza yakaongozana magari hadi sita yanayoelekea upande mmoja
4. Overtime/motisha nahisi kwao wanaogopa kufanya.

Nimeona nchi za wengine walioanza kufanya hizi projects kwenye miji yao mikubwa;
1. Magari yanafanya kazi masaa 24/7 ila yanapungua barabarani jinsi muda unavyozidi kuyoyoma na siku za weekends
2. Sio lazima magari yote yaanzie mwanzo kupakia abiria kunakuwa na mawasiliano kati ya head office/port na vituoni kuangalia wingi wa abiria na kutuma gari
3. Dereva anayefanya vizuri mfano kuwahi, attendance, ukarimu/costomer care anakuwa rewarded
 
Umenena vema, na kikubwa kitakachowaua mapema ni kuondolewa washindani!
Watashindwa kbs kuwa wabunifu, Wateja tunashuhudia Huduma mbovu kbs na ni vile tu hatujui ndani kuna nn,
1: Yale magari wanayotumia yanatumia diesel kiasi gani kwa km 1!?
2: kiasi cha diesel kinachotumika na Pesa inayopatikana vinawiana!? MF: daladala LA kawaida likitumia Mafuta ya 120,000 huwa jumla linategemewa limeingiza around 350,000. Ambapo mwenyenalo anapata around 140, au 150,000. Kinachobaki ni posho ya dereva na konda, hii ni kwa Eicher na Tata za milango miwili.
3: na huenda wamepigwa kwa kupewa injini zenye matumizi makubwa ya Mafuta tofauti na kinachopatikana.

Eti usiku hakuna usafiri, sijui watz hawatakiwi kufanya kazi usiku!!
 
Yan pamoja na kuondolewa washindani wao ambao ni daladala bado kampuni inakufa taratibu,management inabidi ijitafakari upya ili kuondoa kero zilizopo.
 
Naiangalia project ya UDART kwa jicho la tatu naona inakufa. Pamoja na support kubwa ya Serikali bado hawa jamaa (management ) wameshindwa kujiongeza kabisaa.

Imagine if were you unaondolewa washindani wako katika biashara unabaki peke yako harafu unashindwa kufanya huduma unategemea nini?

Wateja ( pamoja na mimi) wanalalamika kukaa muda mrefu vituoni lakini utawala hauna ufumbuzi.

Wametoa namba za customers care hazipokelewi kabisa(nadhani kwenye hili wanamlizisha mheshimiwa kama vile wafanyabiashara wanavyobandika siku ya TRA kuwa yeye analipa kodi while not)

Hawa jamaa hawajui;
1.Muda gani ni peak/rush hours magari yawepo barabarani
2.Madereva kuanza kazi muda tofauti tofauti kutasaidia kumaliza kazi muda tofauti
3.Hawapo systematic katika kuyaondoa magari kwenye main port zao yanaweza yakaongozana magari hadi sita yanayoelekea upande mmoja
4.Overtime, motisha nahisi kwao wanaogopa kufanya.

Nimeona nchi za wengine walioanza kufanya hizi projects kwenye miji yao mikubwa;
1.Magari yanafanya kazi masaa 24/7 ila yanapungua barabarani jinsi muda unavyozidi kuyoyoma na siku za weekends
2.Sio lazima magari yote yaanzie mwanzo kupakia abiria kunakuwa na mawasiliano kati ya head office/port na vituoni kuangalia wingi wa abiria na kutuma gari
3.Dereva anaye fanya vizuri mfano kuwahi, attendance, ukarimu/costomer care anakuwa rewarded
Kupakia abiria Mbezi Luis halafu wanashushwa Kimara terminal halafu tena abiria hao hao wanapakiwa tena kuwapeleka mjini.Au abiria wanapakiwa mjini halafu wanashushwa Kimara halafu magari hayo hayo yanawapakia abiria hao hao kuwapeleka Mbezi Luis.Hiki kitendo ni moja ya ukatili uliopitiliza na ni aibu kwa taifa.Shilingi mia nne ( 400 ) zinazokatwa kama nauli ni wizi mtupu
 
Hawa jamaa hawana schedulers makini, hawana ubunifu na kibaya zaidi hawafikirii nje ya box.

Haiwezekani kwa Jiji kama Dar ambalo watu wake wanafanya kazi masaa 24/7 halafu wewe ambaye umepewa njia bila mshindani unafunga huduma saa 4 usiku. akili za wapi hizi?

Halafu utakuta zile daladala za kuiba zinazoingia barabarani kuanzia saa 7 usiku zinaitwa magendo. Magendo gani wakati watu wanahitaji usafiri?

Serikali itafute kampuni makini kuhudumia wananchi.
 
Daah ikifa 'afu' waruhusu zile njia za mwendo kasi zipite gari zetu raia wa kawaida itakua mzuka kishenzi aiseee.
 
Hivi wa tz hawa wanaosimamia kampuni hili niwazalendo kweli?
hahahaa hata waliongia mkataba na hii kampuni si wazalendo , serikali inalipwa sh 10M kila siku , wakati huo huo sirikali imeivest shs 300 Bil, kwa hiyo payback period ni miaka mia , sasa siulize je hiyo miundo mbinu itadumu kwa miaka mia ? Wakati hiyo kampuni kila siku wanaingiza zaidi ya shs 100.
 
Hali ya huu mradi ni mbaya sana kwa sasa.
Kabla hawajaenda kuwekeza pesa nyingine nyingi kwenye awamu zingine za mradi huu inabidi warudi kurudisha hali nzuri angalau kwa kiwango walicho anza nacho.

Sasa gari hakuna na miundombinu ibakufa kwa kasi huku mapato yakiibwa kwa kasi ya ajabu ktk mfumo wao wa ticket.

Kuna baadhi ya vituo mfano Kibo unapewa ticket yenye QR Code kama kawaida lakini hau-scan unaambiwa pita pembeni. Sasa hapo si mtu anaweza chapisha au kudurufu ticket feki au anaweza kuokota ticket ambazo hazikunjwa ovyo na mteja akaziuza tena?

Kipindi cha mwanzo baada ya kuondoka Maxcom wakaanza kutumua ticket za kawaida ndio palikuwa na wizi wa kutisha.
Pale kituo cha kariako Msimbazi kuna makatisha ticket alikuwa ticket moja anakata vipande hadi vinne(4), akikupa kimoja ukimuuliza kwanini unipe kipande anakuambia wewe nenda tu hakuna shida.
Wakati wa kutoka hakuna mtu anakuuluza.

USHAURI:
Serikali iingilie kati kuboreshwa mfumo wa electronic ticketing, kila kituo ufanye kazi.

Warejeshe kadi, ikuwezekana wateja wote watumie kadi pekee.

Mabasi yaongezwe.

Mabasi yafanye kazi usiku wote hata kama yabaki mabasi 2 au 3 kwa kila route kuanzia saa 6 usiku au hata ikilazimu nauli kuwa 1000/- kuanzia saa 6:30 usiku.

Mabasi yaondoke kwa kupishana vituoni hasa mchana yanapokuwa yamepunguzwa.

Kujaza sana watu kutokana na upungufu wa magari ni kero kwa abiria lakini ni hasara kubwa mno kwa wenye mabasi. Gari zinaharibika sana. Inaweza kuwa hasara kubwa kwa kampuni kuliko hasara ya mafuta na wafanyakazi kama yakiongezwa mabasi.

[HASHTAG]#MHESHIMIWA[/HASHTAG] MAGUFULI INGILUA KATI PESA YETU YA UMMA TUTAKAYO LIPA TULIKOKOPESHWA FEDHA YA MRADI ITAENDA BURE. NA NI AIBU KUFELI KWA MRADI HUU.
 
Kwa mtaji huohuo Na vitendea kazi hivyo hivyo akiletwa CEO Mkenya UDART itakuwa imara. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, sisi tuna laana ya kutokuwa serious.
Kila jambo tunaloanzisha Lina mwisho mbaya kwa sababu ya laana ya mwenge.
Isaya : Mlango 50

11 Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Kulala kwa huzuni maana yake hamtafanikiwa.
 
Back
Top Bottom