Project 2015: Mwinyi haoni uharaka wa Katiba Mpya

Inaonekana hata Cover la Katiba yenyewe hujaiona, potelea mbali maana wengi wa watanzania hawajaiona! Je hujawahi kusikia watu wanadai mgombea binafsi) (Haki ya mtu kuchaguliwa kiongozi bila kupitia vyama? Ukubwa wa mamlaka ya Rais ikiwemo tija ya uteuzi wa wabunge 10 wa viti maalumu! Kuhoji kisheria matokeo yaliyo tangazwa na tume ya uchaguzi? Kazi wa wakuu wa wilaya? nk nk.

Kwenye red nimeshindwa ku-comment kwa sababu hujatoa source wala hujasema walikuwa wanataka nini kibadilishwe ndani ya katiba hii mbofu mbofu! Nakumbuka miaka ile walichoma mabucha ya nguruwe Dar na Mwanza wali vunja mabanda ya nguruwe na kuwauwa huku damu za wanyama hao zikiwarukia kwenye kanzu zao lakini hawakuzivua wala kuzitupa!

Usitake kuhusisha hitaji la katiba mpya na masuala ya kidini kama mtu aliefilisika kifikra. Katiba mpya ni HITAJI la watanzania wenye kuipenda nchi yao yaani wazarendo wa kweli.

Nimecehka sana, japo umeongea kwa ghadhabu....
Kwahiyo walirukiwa damu siyo? Halafu bado wanasendelea kuzivaa hizo kanzu?
Haki ya nani elimu muhimu........maana wangesoma wasingethubutu kuuwa nguruwe kwa mikono yao!
 
ASALAM ALYEKUM WADAU?nimesoma gazeti moja katika mtandao lina habari ya mzee mwinyi amenukuliwa na CUF akisema haoni haja ya katiba mpya eti ya sasa inafaa.
Katika taifa letu hili lilopoteza muelekeo nilidhani yeye ndiye kiongozi pekee anaye weza kukemea viongozi na kuwashauri vyema kuhusu nhitaji la jamii.

Mzee wetu anadai haoini haja ya kudai katiba mpya anataka taifa tumeeleweje?hajui kila kitu kina wakati wake na huu ndio wakati haswa wa mabadiliko ya katiba na nchi nzima inajadili mabadaliko hayo kwa ustawi bora wa taifa letu? hakumbuki alivyokuwa madarakani akaunda tume na matokeo ya tume yalisema kuwepo kwa mahitaji ya katiba mpya, leo imepita zaidi ya miaka 18 tangu apokee taarifa hiyo ya tume na bado andahani hitaji la zaidi ya miaka 18 nyuma ambalo halikuwahi fanyiwa kazi limekwisha?limekwishaje wakati yeye ni miongoni mwa wale walionyonga hitaji hilo na leo akisema hakuna hitaji anatakan tumueleweje?
 
Sababu tunataka sasa ni kuwa tumechoka kutawaliwa na ccm. Hii katiba iliundwa kukidhi matakwa ya ccm. Sasa tuna vyama vingi. Ni wakati wa kuwa na katiba mpya ambayo ilitakiwa kuundwa tangu vyama vingi viliporuhusiwa.
 
Nyie na utani! Watu wengi wa bara na pwani hutaniana sana. Bahati mbaya makao makuu ya nchi hayako pwani yako bara. Kama hujui kitu kidogo kama hiki basi katiba itakuwa ni tatizo kubwa kwako aheri tuiache. Ama sivyo tutumie 2011 kuelimishana juu ya katiba kabla ya watu kama wewe kupanda gari hili la mabadiliko.

Sidhani kama mzee mwinyi anaelewa katiba kiasi hicho. Kumbuka Uraisi ni taasisi mambo mengi alikuwa anafanyiwa na watu/wataalamu. Tumweke tu katika kundi la wananchi wanaotakiwa kuelimishwa kuhusu katiba. Naamini alivo mzee wa hekima akielewa atapanda gari la mabadiliko Kama wengine tulivopanda.
 
kwenye katiba mpya tuta rejea kinga ya raisi aliyemaliza muda wake. Hawa jamaa wana kinga kama vile Mungu, Hawashitakiwi hata kama walitenda makosa ya kuhujumu nchi au kumwaga damu isiyo na hatia. NADHANI HILO NDILO LINAMSUMBUA MZEE WETU. Anafikiria zaidi ubinafsi kuliko masilahi ya kizazi cha sasa na kijacho. Kwenye katiba ijayo hatutasubiri sijui Ocampo, sijui ICC, tutashughulika na mtu hapa hapa. Kama wenzetu Zambia - Chiluba anaulamba na raisi mwingine hatafanya madudu kama yale aliyofanya.

Tunataka katiba itayolinda maslahi ya nchi na rasilimali zetu. Watu wadogo tu sasa hivi wana dhamana ya kuamua mambo ya rasilimali kwenye katiba mpya tutapendekeza mfumo wa kuangalia rasilimali zetu kwa ajili yetu na kizazi kijacho. WATU WANAKOMBA KILA KITU BILA HATA AIBU!

Wazee walietenda kistaarabu watalindwa na katiba mpya, Hivo Mzee Mwinyi kama hakutenda jambo baya asiwe na wasiwasi.
 
Personal attacks kwa mtoa hoja haziongezi hadhi la jukwaa hili.
Lakini maoni kwamba "why new constitution now" yanasikitisha. In fact new constitution imecheleweshwa. Mapendekezo ya Ripoti ya Jaji Nyalali yalishauri vyama vingi vianze na katiba mpya na kufuta au kurekebisha sheria kandamizi zipatazo arobaini. Lakini wapi yakafanyika marekebisho ya hapa na pale ili chama tawala kiendelee kupeta. Hivyo nani haoni kipengere kinachokataza kuhoji matokeo ya uchaguzi ya uraisi yanaruhusu jinai kutendeka? Matokeo ya uchaguzi kuchakachuliwa na kitendo hicho kuwa halali! Vizazi vijavyo vitatucheka kama tutaendelea na katiba kama hii yenye vitu vinavyo vinaruhu jinai ndani ya katiba au kuwa na sheria nje ya sheria. Na wala siyo tu kuondoa vipengele vibovu, bali linaliohitajika ni kutengeneza new framework inayoanzia na constitutional principles ambazo kutakubaliana nazo.

Hao wanaosema wanatafakari nini kifanyike kushughulikia katiba wawe na ujasiri wa kumteua Prof Issa Shivji kuwa mwenyekiti wa tume ya mchakato wa kuondaa katiba mpya. Prof huyu ameji-distinguish sana katika michango yake katika suala hili. Nakumbuka sana mchango wake tangu mwaka 1992 wakati alipo alivyopendekeza maboresha ya mapendekezo ya Jaji Nyalali
 
Back
Top Bottom