Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
TANZANIA inaweza kunufaika zaidi na sekta ya mafuta na gesi asilia ikiwa wazawa ndio watakuwa na fursa ya kutosha ya ajira na kusimamia sekta hiyo, FikraPevu inaripoti.
Hali hiyo itategemea pia ufanisi katika programu mbalimbali za elimu ambazo serikali imezianzisha, ikiwa ni pamoja na kusisitiza kwa vitendo ufundishaji wa masomo ya sayansi ambayo yanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu pamoja na wanafunzi wengi kutoyapenda.
Tanzania imekuwa ikitafiti uwepo wa mafuta na gesi asilia kwa zaidi ya miaka 60 sasa na katika miaka yote hiyo, imefanikiwa kugundua uwepo wa gesi asilia kwa wingi na kuifanya kuwindwa na wawekezaji wa kimataifa.
Pamoja na ugunduzi wa rasilimali hiyo, bado inakabiliwa na upungufu mkubwa wa wataalamu kwenye sekta hiyo, hali ambayo inaonyesha kwamba kuna mahitaji makubwa ya elimu ya ufundi ambayo inaweka msisitizo kwenye stadi maalumu na maarifa ambayo yanahitajika hasa kwenye shughuli mbalimbali za utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia nchini.
Soma zaidi hapa => Programu za elimu zitawapa wazawa fursa za ajira katika sekta ya gesi na mafuta Tanzania | Fikra Pevu