Programu ya kampeni za Hillary Clinton yadukuliwa

Programu ya kampeni za Hillary Clinton yadukuliwa

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
Maafisa wa upelelezi nchini Marekani wamesema kuwa programu ya komputa inayotumiwa na jopo linalosimamia kampeni ya Bi Hillary Clinton imedukuliwa.

Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi Clinton walisema kuwa wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika kompyuta hiyo.

Awali kamati ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa.

Vyombo vya habari Marekani vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.

Shirika la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema kuwa linaendelea na uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha udukuzi huo dhidi ya kompyuta za chama cha Democratic.

Juma lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.

Chanzo: BBC
 
Hii vita ya cyber ni kubwa na ngumu kuliko vita ya drones na swords za ISIS, sababu za kumuwinda snowden zinazidi kuwa nyingi
 
Back
Top Bottom